#COVID19 Dar: Askofu Ruwai’chi aagiza mapadri wote kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19

Naona umeamua kuhubiri kabisa!. haya uliyoandika ndio tunayoyasikia kila uchwao huko makanisani,barabarani na kwenye vituo vya mabasi. Kama karama na vipawa vimetolewa kwa watu, Hao mapadre na makanisa yao kazi yao hasa ni nini?... Kukusanya sadaka?.
🤣 🤣 🤣Dah-Kuna maswali huwa mtu akiuliza yanazalisha maswali mengi sana juu ya competence ya mtu anayeuliza 🤣🙌🙌🙌🤣
 
Mwambie avae kofia sjui kobaragashia kinachimtosha vizuri aache kuvaa kofia za watoto wachanga, chanjo sio razima ni hiari nao wana hiari ya kukataa au kukubali aache mihemko au naye kapiga pesa pesa pesa pesa
 
Unapaswa kuelewa MUNGU aliwapa binadamu karama tofauti tofauti kupitia Roho wake Mtakatifu,Madaktari wamepewa karama ya uponyaji-Ni neema ya MUNGU katika kuendeleza uhai miongoni mwa wanadamu.MUNGU anasema tutumie utashi,akili pamoja na maarifa ili tusiangamie na upumbavu.MUNGU hupenda mwanadamu naye ajisaidie kwa njia mbalimbali na awajibike pia kwa mazingira yake.Swali ni je,Kwann tunaambiwa tumtegemee tu MUNGU kwenye magonjwa lakini kwenye CHAKULA tunaambiwa tumwombe MUNGU na tujitume kufanya kazi kwa bidii? Kwann tusijifungie tu ndani na kumwomba MUNGU ili chakula kishuke? Jibu ni kwamba-Maandiko yanasema asiyefanya kazi na asile,hivyo kutokufanya kazi kwa bidii hudhalisha mzizi wa dhambi-kwa sababu uvivu huweza kupelekea wizi na kifo kutokana na njaa.Rais wetu mpendwa aliyemtegemea MUNGU pasipo kuwajibika kibinafsi kwa mazingira yake leo yukwapi? TB Joshua aliyewaaminisha watu mambo ya uwongo kuhusiana na CORONA yukwapi? Penye Sala,juhudi na uwajibikaji MUNGU huonekana.
Udaktari sio karama ya uponyaji Ni kitu Cha kusomea

Karama ya uponyaji Ni uwezo unaopewa na Mungu wa kuponya bila kusoma popote
 
Ficha ujinga mkuu,sala ya kuombea janga la CORONA iliidhinishwa na TEC na ilikuwa inasaliwa makanisa yote katoliki Tanzania.Sasa ulitaka waje wakusalie na huko msikitini kwako wakati wewe siyo mroma?
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Askofu anatoa agizo mapadre wote wachanjwe? Hata Papa hajatoa agizo popote! Kiukweli hilo agizo linastua sana! Seems ukichanja unatamani kila mtu achanje na wala si tu kwa nia njema bali kibinadamu tuna hulka hiyo.

Askofu hili haupo sawa. Mapadre watakupinga waziwazi na kuingiza Kanisa kwenye mgogoro ambao hukuutegemea. Kwanza unawaambia waache "utoto" kweli? Unafikiri kwa nafasi yako ya uaskofu maana yake umezidi mapadre wote akili?

Nimesikiliza hiyo hotuba nikawa very disappointed na Askofu wetu huyu.

Chanjo ni hiari, kama serikali inasema ni hiari wewe kiongozi wa dini unasema lazima? Kesho serikali ikiongoza kwa imla utapinga wewe? Very disappointed
Waliochanjwa Chanjo ya COVID-19 wanawaona ambao hawajachanja Kama wanaelekea kufa very soon Wakati huo, ambao hawataki chanjo wanawaona waliochanjwa Kama watakufa au kuwa mazombie very soon.

By the way, Mhasham Askofu Yuda Thadei, kabla ya kutoa amri hiyo ambayo kimsingi inaingilia haki ya Uhuru wa kuamua juu ya miili yao kwa Mapadre, anatakiwa aboreshe Miundombinu ya Hospitali ya Kumbukumbu ya Kardinali Rugambwa. Amri Kama hizo, Sasa zinagharimu maisha ya Mapadre wetu. Amri yake ya kwamba Mapadre wote watibiwe kwenye hospitali ya Kanisa yaani Cardinal Rugambwa Hospital imegharimu maisha ya Padre Haule kwa kukosa Mechanical Ventilators. Ni Bora waziache Parokia ziwe zinawapeleka Mapadre wao kwenye hospitali wanazotaka. Ni aibu hospitali Kama Ile kukosa Vent.

Amri za Mhasham zinatakiwa kuangaliwa upya.
 
Bila ya usalama wa afya zetu tutazidi kuwapoteza VIONGOZI WETU WASOMI.....

#ChanjoNiboraKulikoTiba
Viongozi Wasomi pekee hawana tija mkuu Cha muhimu ni kuwa na viongozi wasomi na wenye busara daima hata wasio na busara tuwaombee maana tayari wapo pale
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom