Dar, Arusha, Mwanza Na Mbeya, Yako Wapi Mageuzi?

IsayaMwita

JF-Expert Member
Mar 9, 2008
1,127
140
Iweje CCM washinde mijini? jamani tunaamini huku mijini ndiko kuna uelewa mkubwa, magazeti mengi, Redio za kutosha na TV!!!!!!!!

Mijini ndiko kunafukuzwa wamachinga, watu kubomorewa majumba, hebu inakuweje jamani?

Waandishi wote wanaishi mijini.

Wasomi wote wanaishi mijini...................., jamani nielezeni kuna nini? ama CCM huku mjini wanafavya kamchezo gani? ina maana hata wewe uliwachagua ccm 2005?

JF nisaidieni kuna nini basi hatupati kufanya mapinduzi huku mjini na badala yake yake mapinduzi yanafanyika kule Karatu, Tarime,Mpanda na Bariadi?

Jamani kuna nini huku Arusha, Mwanza, Dar na hata hapa Mbeya?
 
Watu wa mijini, mna tatizo gani? ni nani kawaroga? mbona mnaishia maneno bila matendo? iweje huku mjini hamna dhamira ya kweli? iweji watu wasiosoma(hawajaelimika) ndiyo wafanye mageuzi ya kisiasa na ninyi wasomi mnaokaa mijini hamjafanya chochote? maneno tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.............., Mbona hatuna mbuge yoyote toka katika miji hiii niliyoitaja? tunaona watu kule vijijini ndiyo wanaofanya kweli

Hebu inakueje jamani??????????????
 
Mwita,

Ukitaka kujua ni kwa nini CCM inashinda chaguzi rudi nyuma kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995. Hapa Dar majimbo yote yalichukuliwa na wapinzani hasa NCCR, lakini usalama wa taifa wakafanya vitu vyao, uchaguzi ukarudiwa na ushindi ukaenda CCM. Kule Mbeya mjini Mwaiseje, Katibu Mkuu wa NCCR (kwa sasa) alikuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia chama chake cha NCCR.

Kwa maoni yangu Watanzania wana mwamko wa kisiasa sana. Sehemu kubwa ya matatizo ni CCM. Hawa jamaa, amini usiamini wanaiba kura. Kinachowasaidia sana ni kuwa tume ya uchaguzi inateuliwa na rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, vyombo vyote vya dola vinafanya kazi kufuata matakwa ya CCM, kila wakati Bunge linapovunjwa kuelekea uchaguzi mwingine wabunge wote hupewa milioni 20 (wabunge wengi ni wa CCM na fedha hizo hutumika kugawa takrima). Aidha CCM inatumia fedha za umma kama za BOT kufanyia kampeni. Mbali na haya yote CCM ina mbinu nyingi za kuhujumu uchaguzi. Kumbuka pia semo wa Sumaye, "Mtu akitaka biashara yake ifanikiwe, ajiunge na CCM." Msemo huu si maneno matupu CCM inautumia kwa vitendo. Wafanya biashara na wafanyakazi wasiofanya matakwa ya CCM wanadhibitiwa na serikali ya CCM.

Kwa ujumla, uwanja unaotumiwa wakati wa uchaguzi haujawa tambarare. Hata refa au mwamuzi wa mchezo huwa anatoka upamde wa timu mojawapo ya zinazocheza uwanjani, timu ya CCM. Hata mtandao uliokwisha kujengeka wakati wa chama kimoja kwa kiasi fulani unaisaidia CCM.

Kwa kiasi fulani hii ndiyo hali inayofanya CCM kuendelea kutawala. Siyo kwa sababu watu wanaingu mkono, bali kwa sababu wana mbinu nyingi chafu wanazozitumia kupora kura na kujitangaza washindi.
 
Siku zao zaja,pale ambapo tutawaambia Polisi ana usalama wa taifa kwamba wachague kuwa nasi ama kuwa na mafisadi.Hapo ndipo moto utawaka
 
Positioning ya yama vya Upinzani katika miji husika ni tatizo kubwa sana... na kama hali itaendelea kuwa katika hali hii basi ni kwamba tutaendelea kuwa Wapinzani tu lakini hatuna meno. Kama tutakuwa tunasubiri Mwaka 2010 ili tuweze enda katika miji husika na kutangaza sera zetu basi ni dhahiri hatutawang'oa CCM.

Vijijini imekuwa ni rahisi kidogo kupambana na CCM kwa kuwa wananchi wa huko are feeling like they are left out and CCM wameweka concerntration kubwa zaidi katika miji mikuu yenye watu wengi. Kwa hiyo nadhani ili kuwang''a CCM inabidi tubadili mwendo na kuwafikia watu zaidi.
 
Iweje CCM washinde mijini? jamani tunaamini huku mijini ndiko kuna uelewa mkubwa, magazeti mengi, Redio za kutosha na TV!!!!!!!!

Mijini ndiko kunafukuzwa wamachinga, watu kubomorewa majumba, hebu inakuweje jamani?

Waandishi wote wanaishi mijini.

Wasomi wote wanaishi mijini...................., jamani nielezeni kuna nini? ama CCM huku mjini wanafavya kamchezo gani? ina maana hata wewe uliwachagua ccm 2005?

JF nisaidieni kuna nini basi hatupati kufanya mapinduzi huku mjini na badala yake yake mapinduzi yanafanyika kule Karatu, Tarime,Mpanda na Bariadi?

Jamani kuna nini huku Arusha, Mwanza, Dar na hata hapa Mbeya?

Isayamwita hebu jiulize inakuwaje Moshi Ndesamburo anawaendesha puta CCM.
Kila kitu ni strategies tu.CHADEMA ilipoamua kujiimarisha Moshi iliona njia pekee ni kuweka mtu ambaye anaweza kukiuza chama kwa wananchi na kupambana na nguvu za CCM.

Jimbo la Moshi ni lulu kwa wapinzani na CCM wanalionea gere sana.Uchaguzi wa 2005 CCM kupitia kwa mlezi wa chama hicho mkoani Kilimanjaro walichangisha zaidi ya miliono 300 za 'kulikomboa' jimbo la Moshi.Wafanyabiashara walitoa mipesa kwa ahadi kedekede za CCM.

Hata hivyo wao CHADEMA walikuwa wameshajiwekea rekodi nzuri ya maendeleo hivyo hawakuwa na kazi kubwa ya kuwapiga kumbo CCM.Kwenye kampeni za Ndesamburo alikuwa anajigamba kutokana na rekodi nzuri ya uwajibikaji kwa wananchi na aliwaambia waziwazi wapiga kura wake kuwa pesa za CCM wazichue na kuzitafuna lakini kura wasiwape.

Kama Moshi wameweza sisi katika miji mingine tunaweza kama tukijipanga kulingana na mazingira husika.Dar es Salaam kwa mfano, wengi wetu ni wakereketwa sana wa mageuzi lakini linapokuja suala la uchaguzi tunawaachia wazee na akina mama.Kada mbalimbali za watu kama makonda, madereva wa daladala, waalimu, wauguzi, wanafunzi, wamachinga na kadhalika ni jeshi kubwa sana kama likiamua kusema hapana kwa njia ya kura.

Haya ndiyo makundi yanayoanzisha maandamano kila mara kudai haki na maisha bora kwa kila mtanzania.Kama makundi haya yakipiga kura na kudhamiria kuing'oa CCM hata kama CCM wakipanga kuiba kura itakuwa ngumu.

Strategies za CCM ni nyingi na kwa kuwa wao ndio walioshikilia dola wanakuwa na uwanja mpana wa kufanya watakalo.Kwa mfano sasa hivi Kikwete ameshaanza kampeni za uchaguzi ujao.Ziara zake mikoani zina lengo la kuweka mambo sawa.Huu ni utaratibu ambao upinzani nao wanatakiwa kuuanzisha.Pale waliposhindwa CCM wao lazima waoneshe wanaweza kwa vitendo.

Jambo jingine ni ubinafsi wa vyama vya upinzani.Linapokuja suala la uchaguzi ni muhimu vyama vikaacha kutugawanya badala yake wakapeana nafasi katika kusimamisha wagombea majimboni.Vyama viachiane majimbo kulingana na nguvu ya chama na mtu husika kusudi upinzani ujipatie wabugne wengi mjengoni.

Mikakati haianzi 2010 ndugu zangu, inaanza leo tena sasa.
Tusiwe mahiri wa kulalamika na kuandamana na kusahau kuwa njia sahihi na nzuri ya kuibana CCM ni sanduku la kura.Hata wakiiba kura hawatadumu milele.
Mungu husikia kilio cha wanyonge na kamwe hataacha mwovu adumu milele. Meseji senti!
 
Mwita,

Ukitaka kujua ni kwa nini CCM inashinda chaguzi rudi nyuma kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995. Hapa Dar majimbo yote yalichukuliwa na wapinzani hasa NCCR, lakini usalama wa taifa wakafanya vitu vyao, uchaguzi ukarudiwa na ushindi ukaenda CCM. Kule Mbeya mjini Mwaiseje, Katibu Mkuu wa NCCR (kwa sasa) alikuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia chama chake cha NCCR.

Kwa maoni yangu Watanzania wana mwamko wa kisiasa sana. Sehemu kubwa ya matatizo ni CCM. Hawa jamaa, amini usiamini wanaiba kura. Kinachowasaidia sana ni kuwa tume ya uchaguzi inateuliwa na rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, vyombo vyote vya dola vinafanya kazi kufuata matakwa ya CCM, kila wakati Bunge linapovunjwa kuelekea uchaguzi mwingine wabunge wote hupewa milioni 20 (wabunge wengi ni wa CCM na fedha hizo hutumika kugawa takrima). Aidha CCM inatumia fedha za umma kama za BOT kufanyia kampeni. Mbali na haya yote CCM ina mbinu nyingi za kuhujumu uchaguzi. Kumbuka pia semo wa Sumaye, "Mtu akitaka biashara yake ifanikiwe, ajiunge na CCM." Msemo huu si maneno matupu CCM inautumia kwa vitendo. Wafanya biashara na wafanyakazi wasiofanya matakwa ya CCM wanadhibitiwa na serikali ya CCM.

Kwa ujumla, uwanja unaotumiwa wakati wa uchaguzi haujawa tambarare. Hata refa au mwamuzi wa mchezo huwa anatoka upamde wa timu mojawapo ya zinazocheza uwanjani, timu ya CCM. Hata mtandao uliokwisha kujengeka wakati wa chama kimoja kwa kiasi fulani unaisaidia CCM.

Kwa kiasi fulani hii ndiyo hali inayofanya CCM kuendelea kutawala. Siyo kwa sababu watu wanaingu mkono, bali kwa sababu wana mbinu nyingi chafu wanazozitumia kupora kura na kujitangaza washindi.

Mtu wa Mungu,

Katika uzoefu wangu wa chaguzi barani Africa utaona mijini ndiko mageuzi hufanyika kwa kiasi kikubwa, lakini hapa nyumbani mambo si hivyo, hebu nini kifanyike jamani?
 
Tuliodhani kuwa ni wanamageuzi wametugeuka. Angalia akina Lamwai, Kabourou, Tambwe Hiza,....
 
Isayamwita hebu jiulize inakuwaje Moshi Ndesamburo anawaendesha puta CCM.
Kila kitu ni strategies tu.CHADEMA ilipoamua kujiimarisha Moshi iliona njia pekee ni kuweka mtu ambaye anaweza kukiuza chama kwa wananchi na kupambana na nguvu za CCM.

Jimbo la Moshi ni lulu kwa wapinzani na CCM wanalionea gere sana.Uchaguzi wa 2005 CCM kupitia kwa mlezi wa chama hicho mkoani Kilimanjaro walichangisha zaidi ya miliono 300 za 'kulikomboa' jimbo la Moshi.Wafanyabiashara walitoa mipesa kwa ahadi kedekede za CCM.

Hata hivyo wao CHADEMA walikuwa wameshajiwekea rekodi nzuri ya maendeleo hivyo hawakuwa na kazi kubwa ya kuwapiga kumbo CCM.Kwenye kampeni za Ndesamburo alikuwa anajigamba kutokana na rekodi nzuri ya uwajibikaji kwa wananchi na aliwaambia waziwazi wapiga kura wake kuwa pesa za CCM wazichue na kuzitafuna lakini kura wasiwape.

Kama Moshi wameweza sisi katika miji mingine tunaweza kama tukijipanga kulingana na mazingira husika.Dar es Salaam kwa mfano, wengi wetu ni wakereketwa sana wa mageuzi lakini linapokuja suala la uchaguzi tunawaachia wazee na akina mama.Kada mbalimbali za watu kama makonda, madereva wa daladala, waalimu, wauguzi, wanafunzi, wamachinga na kadhalika ni jeshi kubwa sana kama likiamua kusema hapana kwa njia ya kura.

Haya ndiyo makundi yanayoanzisha maandamano kila mara kudai haki na maisha bora kwa kila mtanzania.Kama makundi haya yakipiga kura na kudhamiria kuing'oa CCM hata kama CCM wakipanga kuiba kura itakuwa ngumu.

Strategies za CCM ni nyingi na kwa kuwa wao ndio walioshikilia dola wanakuwa na uwanja mpana wa kufanya watakalo.Kwa mfano sasa hivi Kikwete ameshaanza kampeni za uchaguzi ujao.Ziara zake mikoani zina lengo la kuweka mambo sawa.Huu ni utaratibu ambao upinzani nao wanatakiwa kuuanzisha.Pale waliposhindwa CCM wao lazima waoneshe wanaweza kwa vitendo.

Jambo jingine ni ubinafsi wa vyama vya upinzani.Linapokuja suala la uchaguzi ni muhimu vyama vikaacha kutugawanya badala yake wakapeana nafasi katika kusimamisha wagombea majimboni.Vyama viachiane majimbo kulingana na nguvu ya chama na mtu husika kusudi upinzani ujipatie wabugne wengi mjengoni.

Mikakati haianzi 2010 ndugu zangu, inaanza leo tena sasa.
Tusiwe mahiri wa kulalamika na kuandamana na kusahau kuwa njia sahihi na nzuri ya kuibana CCM ni sanduku la kura.Hata wakiiba kura hawatadumu milele.
Mungu husikia kilio cha wanyonge na kamwe hataacha mwovu adumu milele. Meseji senti!

Mzee wa Gumzo.

sasa tunafanyeje hapa? haiwezekani hata kidogo tuwe kimya huku CCM wakiendelea kushinda huku mijini jamani,,,,,,,,,.............., haiwezekani,
Ni kwanini jamani tumebakiza maneno tu?,

Pamoja na CCM kutuibia mapesa yetu ..............., watanzania wa mjini tuna nini humu vichwani mwetu?
 
Tuliodhani kuwa ni wanamageuzi wametugeuka. Angalia akina Lamwai, Kabourou, Tambwe Hiza,....

Tusiwalaumu hawa jamaa, mazingira ya wakati ule hayakuruhusu, kwani utakumbuka jinsi Malando alivyofanywa,Kaburu yeye alihaidiwa mengi hakika akajikuta anasariti, anayenifurahisha ni Tambwe, hakika yale maneno aliyokuwa akiyatumia kukiponda Chama cha CCM, KWELI SIASA NI MCHEZO MCHAFU
 
Inabidi uelewe siasa za sehemu hizo zina tawaliwa na Icon wa sehemu hizo, sasa kioo cha jamii wa Sehemu hizo akiwa Chichiemu, wengi wa watu wanafuata mkumbo kutokana na uelewa mdogo au elimu ndogo.
Eg Dar , ni kweli uchaguzi wa 1995 NCCr walishinda ndio usalama wa taifa ukafanya vitu vyake, lakini chaguzi zilizo fuatta ccm inatumia tactic ya divide and rule, kwa kuwadanganya wananchi wa baadhi ya sehemu kuwapa vyeo viongozi wao, kwa Arusha na Kilimanjaro kuanzia U PM na wizara zinginezo, na keki zingenezo, kwa wenzetu ambao bado wamelala basi wabunge wao watadanganywa kwa kupea wizara ya Utamaduni na michezo etc etc, na vitumbua, wakati aliye shinda ingawa wote wako hiyo ccm anachukua Ngombe mzima at a cost of Vitumbua.
Sasa ukirudi katika hizo siasa za divide and rule angalia DSM ingawa kuna wasomi wengi , lakini wapiga kura wengi kule Temeke, Ilala, Kinandoni nk ni akinanani?
na angalia walio shinda this time toka sehemu hizo
Abasa Mtemvu temeke, Ilala/Kinondoni Zungu type, Ukongo wafugaji wa kuku wa Mayai, Kigamboni-Mwinyi, Kawe na Ubongo zilikuwa ni marginal areas zingeweza kwenda upinzani au CCm
na ukitilia maanani uchaguzi wa 2005 licha ya fedha nyingi kutumika watu walikuwa na matumaini mapya na JMK.
Ukienda Arusha ni jimbo ambalo kwa kiasi fulani limefaidika na hizo siasa za Divide and rule za kupeana vyeo, sumaye alitoka huko kwa miaka 10 ya Mkapa, na Sasa hivi alitokea Lowasa, Nagu, etc , Kilimanjaro kutokana na uelewa wao CCm wamejua jinsi ya kuwashika Vingunge wa sehemu hizo kwa hila na Ghiliba, za Projects kupelekwa huko, Vyeo na Opportunity zingine.
Ukienda Mza naona huko uelewa wa watu wengi ambo ni wapiga kura ni mdogo, wakionyeshwa video ya rwanda , basi hawataki kusikia wapinzani, pia wakidanganywa kwamba Mbunge wao atapewa uwaziri , basi wanampigia, wakijua wasipo fanya hivyo basi jimbo lao litakosa waziri.
na zaidi ya hapo wanaosimama upande wa upinzani MZa hawana Financial Muscles, hivyo wakipigwa push kidogo tu, wanaanguka. Hivyo basi wengi wanao sima sehemu hizo za Mza hawana leadership qualities na uwezo wa kipesa. Hivyo hakuna wanao wachukulia seriously
Mbeya Icon wa huko Gibbons Mwaikambo walisha muondoa Mapema, Sasa aliye Baki Mwandosya Mwakyusya wapo CCm , wanawakatia katia hiyo keki ili waweze kuwa-controll
 
Hivi sisi Watanzania tunaelekea wapi? iweje CCM watutawale kwa miaka 50? na ndiyo maana wanatufanya wanavyotaka, wanachukua wanapopenda, sawa, hebu akili zetu zina matunda?
 
Isayamwita hebu jiulize inakuwaje Moshi Ndesamburo anawaendesha puta CCM.
Kila kitu ni strategies tu.CHADEMA ilipoamua kujiimarisha Moshi iliona njia pekee ni kuweka mtu ambaye anaweza kukiuza chama kwa wananchi na kupambana na nguvu za CCM.

Jimbo la Moshi ni lulu kwa wapinzani na CCM wanalionea gere sana.Uchaguzi wa 2005 CCM kupitia kwa mlezi wa chama hicho mkoani Kilimanjaro walichangisha zaidi ya miliono 300 za 'kulikomboa' jimbo la Moshi.Wafanyabiashara walitoa mipesa kwa ahadi kedekede za CCM.

Hata hivyo wao CHADEMA walikuwa wameshajiwekea rekodi nzuri ya maendeleo hivyo hawakuwa na kazi kubwa ya kuwapiga kumbo CCM.Kwenye kampeni za Ndesamburo alikuwa anajigamba kutokana na rekodi nzuri ya uwajibikaji kwa wananchi na aliwaambia waziwazi wapiga kura wake kuwa pesa za CCM wazichue na kuzitafuna lakini kura wasiwape.

Kama Moshi wameweza sisi katika miji mingine tunaweza kama tukijipanga kulingana na mazingira husika.Dar es Salaam kwa mfano, wengi wetu ni wakereketwa sana wa mageuzi lakini linapokuja suala la uchaguzi tunawaachia wazee na akina mama.Kada mbalimbali za watu kama makonda, madereva wa daladala, waalimu, wauguzi, wanafunzi, wamachinga na kadhalika ni jeshi kubwa sana kama likiamua kusema hapana kwa njia ya kura.

Haya ndiyo makundi yanayoanzisha maandamano kila mara kudai haki na maisha bora kwa kila mtanzania.Kama makundi haya yakipiga kura na kudhamiria kuing'oa CCM hata kama CCM wakipanga kuiba kura itakuwa ngumu.

Strategies za CCM ni nyingi na kwa kuwa wao ndio walioshikilia dola wanakuwa na uwanja mpana wa kufanya watakalo.Kwa mfano sasa hivi Kikwete ameshaanza kampeni za uchaguzi ujao.Ziara zake mikoani zina lengo la kuweka mambo sawa.Huu ni utaratibu ambao upinzani nao wanatakiwa kuuanzisha.Pale waliposhindwa CCM wao lazima waoneshe wanaweza kwa vitendo.

Jambo jingine ni ubinafsi wa vyama vya upinzani.Linapokuja suala la uchaguzi ni muhimu vyama vikaacha kutugawanya badala yake wakapeana nafasi katika kusimamisha wagombea majimboni.Vyama viachiane majimbo kulingana na nguvu ya chama na mtu husika kusudi upinzani ujipatie wabugne wengi mjengoni.

Mikakati haianzi 2010 ndugu zangu, inaanza leo tena sasa.
Tusiwe mahiri wa kulalamika na kuandamana na kusahau kuwa njia sahihi na nzuri ya kuibana CCM ni sanduku la kura.Hata wakiiba kura hawatadumu milele.
Mungu husikia kilio cha wanyonge na kamwe hataacha mwovu adumu milele. Meseji senti!

Hakika tukianza mikakati sasa tuwe na mitazamo ya mbele tuwe na mikakati jamani, haiwezekani hawa jamaa wakaendelea kututesa, kutunyanyasa, hapa tuwe na mitizamo chanya
 
Positioning ya yama vya Upinzani katika miji husika ni tatizo kubwa sana... na kama hali itaendelea kuwa katika hali hii basi ni kwamba tutaendelea kuwa Wapinzani tu lakini hatuna meno. Kama tutakuwa tunasubiri Mwaka 2010 ili tuweze enda katika miji husika na kutangaza sera zetu basi ni dhahiri hatutawang'oa CCM.

Vijijini imekuwa ni rahisi kidogo kupambana na CCM kwa kuwa wananchi wa huko are feeling like they are left out and CCM wameweka concerntration kubwa zaidi katika miji mikuu yenye watu wengi. Kwa hiyo nadhani ili kuwang''a CCM inabidi tubadili mwendo na kuwafikia watu zaidi.

Mizozo,

Nahisi kama watu wa mijini hawana shahada za kupigia kura, kwani watu wenye uelewa ni hawahawa wa mijini, sasa iweje washindwe kuwaweka wapinzani ktk madaraka?

Tazama pale kenya vyama vya upinzani vimeshinda kwa kishindo, iweje huku nyumbani jamani? kuna nini hapa? hapana nimegundua yawezekama jamaa wanatuwangia si bure.
 
isayamwita,

..vyama vya upinzani mara nyingi vimesimamisha wagombea dhaifu.

..pale ambapo wapinzani wamemsimamisha mgombea mwenye credentials/sifa ambaye hata CCM wanamtamani huwa wanashinda.

..Dr.Walid Kaborou aliporudi toka USA, CCM walitaarifiwa wamchukue haraka lakini wakasuasua. matokeo yake akaenda Chadema na kushinda uchaguzi.

..Dr.Wilbroad Slaa alishinda kura za maoni za CCM. Mkapa akamfanyia roho mbaya kumtoa na kumsimamisha kada wao wa siku nyingi Patrick Qorro. Slaa alihamia Chadema and the rest is history.

..wapinzani hawana fedha, mtandao, na organisation, waliyonayo CCM. katika hali hiyo wapinzani wahakikishe wagombea wao wanang'ara kuliko wale wa CCMkwa sifa za elimu, uzoefu wa kitaalamu, na uwezo wa kujieleza na kupambanua hoja.
 
Ukitaka kuona divide and rule at work, angalia huu mgomo wa Junior Doctors muhimbili etc, serekali inasema imetumia Ma daktari Bingwa, hivyo impact ya Mgomo wa junior doctors unakuwa Mdogo, au Junior Doctors na Nurses etc.
Na Ujue CCm indirectly inatumia mpaka udinina ukabila katika hiyo divide and rule.
Kwa hiyo wapinzania wakita washinde lazima wafanye utafiti wa Strengths zao, weakness zao, opportunities walizonazo na threat zidi yao.
 
Tofauti na wanavyofikiria walio wengi, mimi naamimi kuwa ni wasomi ndio wametuangusha.

Angalia wasomi wetu wanavyopigana vikumbo kugombania makombo wanayotupiwa na mafisadi wa CCM.

Angalia wasomi wanavyohangaika kugombania vyeo kwenye chama cha mafisadi kufikia hata kusahau taaluma zao.

Angalia wasomi wanavyochangamkia kila siku kukaa karibu na mafisadi wa CCM ili mambo yao yawanyokee.

Angalia wasomi wanavyoziba masikio yao wasiweze kusikia wananchi wakililia mkate kwani wao wanatupiwa keki na mafisadi ndani ya CCM.

Maprofesa, mainjinia, wanasheria, waalimu, madaktari, mahasibu etc -wote wamewaacha kwenye mataa wamachinga, wakulima, mama ntilie, wavuvi wadogowadogo etc kwa sababu wamepata hifadhi kwenye mbuga za akina Nkapa, Rostamu, Edwadi, Andrea na wenzao wengi tu - wanakokula na kusaza.

Watapata wapi ari na muda wa kutumia usomi wao kuleta mabadiliko. Hongera kwa wazalendo walioamka na wanafanya kweli kama Tarime, Babati na kwingineko.
 
..i dont know much about Mbowe(Chadema),namjua kwa kumuona tuu na Billicanas,hebu start topic yake afanyiwe vetting (kuanzia familia yake,elimu yake,mahawala zake,madeni na biashara zake kama anaendesha kwa kufuata sheri na analipa kodi? na msisahau personal character zake maana kuendelea kusupport wapinzani tusiowajua ndio mwanzo wa kufa upinzani na kuweka mafisadi na kujikuta tuna support kina Mtikila,Lowassa,Karamagi na matapeli wengine wa mjini...vipi IQ yake mlio karibu naye? ni smart kweli kuongoza nchi au chama kubwa kama Chadema?
 
Mtu wa Mungu,

Katika uzoefu wangu wa chaguzi barani Africa utaona mijini ndiko mageuzi hufanyika kwa kiasi kikubwa, lakini hapa nyumbani mambo si hivyo, hebu nini kifanyike jamani?

Mwita,

Nakubaliana nawe kabisa, lakini huko wanakofanikiwa huenda vyama vinavyotawa havijabobea katika mbinu chafu. Pia huenda huko kwingine vyombo vya dola vinakuwa havifungamani na upande wowote. Hapa kwetu CCM imebobea katika hila na mbinu chafu zinazowawezesha kupata kura kwa njia yoyote ili kuendelea kutawala kwa mabavu. Kitu kingine kinachotuponza hapa nyumbani ni hili wazo la "amani" bandia. Kutokana na hali hiyo watu wakitishiwa kidogo tu kuwa mkichagua wapinzani nchi itaingia katika vita wanaogopa. Mahali pengine watu walipata uhuru kwa mtutu kwa hiyo hawatishiki na kitu cha namna hiyo.

Sasa tufanyeje kuondokana na utawala wa kibabe wa CCM? Kwa maoni yangu ni kuwa pamoja na kuhamashisha watu waunge mkono vyama vya upinzani, ni vizuri pia ku-campaign kwa ajili ya:

(a) Tume huru ya uchaguzi.

(b) Mgombea binafsi.

(c) Kushawishi watu walio na uchungu na nchi lakini walio safi wanaokubalika ili wagombee na tuwaunge mkono.

(d) tupenyeze baadhi ya wana mageuzi ndani ya CCM ili tuweze kupata data zao na kujua mikakati yao kabla hawajaitekeleza. Katika hili inapasa wanamageuzi wengine wagombee ubunge kupitia CCM.

(e) Kudai mali na vitega uchumi vyote (isipokuwa ofisi za CCM) vilivyoanzishwa kwa michango ya wananchi wote wakati wa chama kimoja virudidishwe serikalini.

(f) Ikiwezekana vyama vyote vya upinzani vikubaliane kupata mtu neutral wa kugombea urais ili akichaguliwa kazi yake iwe ni kuandaa mazingira ya ushindani wa vyama vingi. Hoja yangu hapa ni kuwa rais huyo awe ni wa mpito na kazi yake kubwa iwe ni kurekebisha katiba yenye kukidhi mazingira halisi ya vyama vingi tuliyo nayo.

(g) Kama wazo (f) haliwezekani, basi tuwahamasishe wananchi wote kufanya maandamano ya amani nchi nzima ili kulazimisha kuundwa kwa katiba mpya itakayokidhi mazingira ya sasa ya nchi yetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom