DAR: Amuua mtoto wa mdogo wake kwa kipigo, aufunga mwili kwenye ndoo kisha kuutupa Ubungo

Hapo kuna mengi ya mambo yaliyoingiliana na kuivuruga kabisa saikolojia ya huyo muuwaji!

Chanzo huenda ni kuadhibu mtoto kwa nia njema, sasa baada ya kugundua kaua, ndiyo hivyo vipande vingine vya mnyororo vikajiunga.

seriously kabisa eti kumuadhibu mtoto wa miaka 2?
Kwa mtazamo wangu mtoto wa miaka 2 hastahili kuadhibiwa kwa kipigo
 
Yaani ukikutana nae njiani unaweza dhani Ni wale wamama wa samaki katoka ferry kuchukua samaki kumbe kabeba maiti.Huyo mtu Ni muuaji wa kukusudia kabisa... ANYONGWE.
 
Jeshi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Mwanamke mmoja kwa tuhuma za mauaji ya Mtoto wa Mdogo wake aliyekuwa na umri wa miaka miwili (2) na miezi minne. Mtuhumiwa huyo LATIFA BAKARI (33), mkazi wa Mabibo aliachiwa mtoto huyo na mdogo wake kwa lengo la malezi na Tarehe 05/04/2022 mtuhumiwa alifanya mauaji hayo baada ya kumpiga kupita kiasi mtoto huyo.

Baada ya kubaini kuwa mtoto huyo amefariki baada ya kipigo, mtuhumiwa tarehe 06/4/22 aliuchukua mwili wa mtoto (marehemu), kuukunja, kuuweka kwenye ndoo ya plastiki kisha kuudumbukiza kwenye kiroba na kwenda kuutupa eneo la River Side UBUNGO.

Baada ya majirani kutomuona mtoto huyo kama ambavyo si kawaida walitoa taarifa Polisi, Polisi ilimuhoji kwa kina mtuhumiwa akakiri mauaji hayo na kwenda kuwaonesha Polisi mwili wa mtoto huyo ulipokuwa. Mwili huo umepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya mifumo ya kisheria kukamilika.

Muliro J. MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
Huyu muuaji anawakilisha roho za unyama mwingi kuliko kiumbe yoyote hapa Duniani waliyonayo wanawake wengi sana kwa watoto ambao sio uzao wa tumbo Lao.

Yani mwanamke kumpenda mtoto wa mwanamke mwenzake kwa kuishi nae na kumpa mapenzi sawa na mtoto wake wa kumzaa waga ni vigumu sana kwa akina mama wengi.
 
Jeshi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Mwanamke mmoja kwa tuhuma za mauaji ya Mtoto wa Mdogo wake aliyekuwa na umri wa miaka miwili (2) na miezi minne. Mtuhumiwa huyo LATIFA BAKARI (33), mkazi wa Mabibo aliachiwa mtoto huyo na mdogo wake kwa lengo la malezi na Tarehe 05/04/2022 mtuhumiwa alifanya mauaji hayo baada ya kumpiga kupita kiasi mtoto huyo.

Baada ya kubaini kuwa mtoto huyo amefariki baada ya kipigo, mtuhumiwa tarehe 06/4/22 aliuchukua mwili wa mtoto (marehemu), kuukunja, kuuweka kwenye ndoo ya plastiki kisha kuudumbukiza kwenye kiroba na kwenda kuutupa eneo la River Side UBUNGO.

Baada ya majirani kutomuona mtoto huyo kama ambavyo si kawaida walitoa taarifa Polisi, Polisi ilimuhoji kwa kina mtuhumiwa akakiri mauaji hayo na kwenda kuwaonesha Polisi mwili wa mtoto huyo ulipokuwa. Mwili huo umepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya mifumo ya kisheria kukamilika.

Muliro J. MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
Huyu anastahili kifo na yeye
 
IMG_6267.jpg
 
Back
Top Bottom