DAR: Amuua mtoto wa mdogo wake kwa kipigo, aufunga mwili kwenye ndoo kisha kuutupa Ubungo

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,021
1,609
Jeshi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Mwanamke mmoja kwa tuhuma za mauaji ya Mtoto wa Mdogo wake aliyekuwa na umri wa miaka miwili (2) na miezi minne. Mtuhumiwa huyo LATIFA BAKARI (33), mkazi wa Mabibo aliachiwa mtoto huyo na mdogo wake kwa lengo la malezi na Tarehe 05/04/2022 mtuhumiwa alifanya mauaji hayo baada ya kumpiga kupita kiasi mtoto huyo.

Baada ya kubaini kuwa mtoto huyo amefariki baada ya kipigo, mtuhumiwa tarehe 06/4/22 aliuchukua mwili wa mtoto (marehemu), kuukunja, kuuweka kwenye ndoo ya plastiki kisha kuudumbukiza kwenye kiroba na kwenda kuutupa eneo la River Side UBUNGO.

Baada ya majirani kutomuona mtoto huyo kama ambavyo si kawaida walitoa taarifa Polisi, Polisi ilimuhoji kwa kina mtuhumiwa akakiri mauaji hayo na kwenda kuwaonesha Polisi mwili wa mtoto huyo ulipokuwa. Mwili huo umepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya mifumo ya kisheria kukamilika.

Muliro J. MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
 
Jamani mtoto wa miaka miwili kakosa Nini kikubwa hicho Hadi auawe kwa kipigo au alilazimishwa kuishi nae? Kwa kweli tunaipenda Sasa sio kabisa loh
 
Sijui aliwaza nn naumia sana kuuwa watoto Kuna lijamaa linaitwa Putin linauwa watoto kila siku

USSR
Kweli kabisa, sijui yale mengine ya kule magharibi mwa Ulaya na Marekani kwanini yanaitwa Malaika ilihali yenyewe ndiyo yameua Watoto wengi sana duniani huko Yemeni, Vietnam, Syria, Iraq, Afghanistan na Libya lakini Putin ndiye anarundikiwa ushetani wao wote
 
Back
Top Bottom