Dar: Aliyemuua mkewe na kuuchoma mwili kwa mkaa awatisha Wanahabari

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Mfanyabiashara Hamis Said anayekabiliwa na kesi ya kumuua Mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto ametoa vitisho ktk Mahakama ya Kisutu akidai atawafanyia kitu kibaya Wanahabari "Wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya Mahakama, sasa nitakuja kuishangaza Mahakama"
=====

Hamis Said Luongo(38) ambaye ni mshtakiwa wa mauaji ya mke wake, Naomi Marijani katika eneo la Gezaulole Kigamboni ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam nchini Tanzania kuwa atafanya kitu kibaya kwa waandishi wa habari ambacho mahakama hiyo haitakitarajia.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai leo Jumanne Agosti 13,2019 mbele ya Mahakama hiyo kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika.

Baada ya maelezo hayo, mshtakiwa Luongo alinyoosha kidole na kuiomba Mahakama hiyo kuwa kichwa chake kimechanganyikiwa hivyo atafanya kitu kibaya kwa waandishi wa habari ambapo Mahakama hiyo haitatarajia.

"Mheshimiwa nina kitu ambacho nataka nikueleze kuhusu waandishi wa habari ambao wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya mahakama, sasa nakueleza hivi nitakuja kuishangaza mahakama hii nitafanya kitu kibaya ambacho hamtakitegemea.”

"Kuna kesi ambayo inanikabili na sielewi hatima ya kesi yangu, hapa nilipo kichwa changu kimevurugika nina mawazo ya mtoto wangu na ninapofika hapa ndani nataka akili yangu itulie lakini hawa wapiga picha wananipiga picha sasa nawaeleza kuwa nitawafanya kitu kibaya ambacho Mahakama haitatarajia," amedai

Baada ya kauli hiyo, Wakili Wankyo alimueleza mshtakiwa huyo kuwa kupigwa picha ni hali ya kawaida na washitakiwa wote wanaofikishwa mahakamani wanapigwa picha na yeye siyo mtu wa kwanza hivyo awape uhuru waandishi wa habari wafanye kazi yao kuwa huru.

"Lengo la waandishi wa habari ni kutoa habari na kuwajuza wananchi hivyo awape uhuru wafanye kazi yao kuwa huru na kumbuka hii ni mahakama na hatujui kitu unachotaka kufanya ni kitu gani," amedai Simon.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 27, 2019 kwa ajili ya kutajwa.

Mshtakiwa huyo ameshitakiwa chini ya Kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhabu, sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Katika kosa hilo, mshitakiwa anadaiwa Mei 15, 2019 katika eneo la Gezaulole Kigamboni Dar es Salaam alimuua mtu anayeitwa Naomi Marajani.
 
Mfanyabiashara Hamis Said anayekabiliwa na kesi ya kumuua Mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto ametoa vitisho ktk Mahakama ya Kisutu akidai atawafanyia kitu kibaya Wanahabari "Wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya Mahakama, sasa nitakuja kuishangaza Mahakama"
kesi nyingine hiyo
 
Hakuzoea maisha ya mahabusu lazima akili iweuke kidogo
 
Sasa ana uhakika gani kama atashinda kesi ya mauwaji ili aje apambane na wanahabari huku uraiani...nahisi atakuwa na mental-disorder
Huyu jamaa siyo wa kawaida pamoja na yote hayo bado anatishia watu uhai wao?
 
Mfanyabiashara Hamis Said anayekabiliwa na kesi ya kumuua Mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto ametoa vitisho ktk Mahakama ya Kisutu akidai atawafanyia kitu kibaya Wanahabari "Wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya Mahakama, sasa nitakuja kuishangaza Mahakama"
Ni suala la muda tu
Atakuja kuwashangaza wafungwa wenzake alivyo mrembo huko gerezani
 
Hapana asidharauliwe akipata upenyo kidogo tu... Anaweza kuleta majanga makubwa.... Kumbuka hana cha kupoteza kwasasa kwahiyo si ajabu anapanga kuua tena
Wakimwachia upenyo itakuwa upuuzi wao.

Huyo ni psychotic. Ameshaonyesha kasoro kichwani kwa kupiga mkwara huo mbele ya vyombo vya dola. Anatakiwa awekewe shackles za mikono na visigino.
 
Mfanyabiashara Hamis Said anayekabiliwa na kesi ya kumuua Mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto ametoa vitisho ktk Mahakama ya Kisutu akidai atawafanyia kitu kibaya Wanahabari "Wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya Mahakama, sasa nitakuja kuishangaza Mahakama"
Anataka kujifanya yy ni Lori la mafuta! Kajizira huyo hana cha kupoteza ni kuwa makini nae kama makinikia
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom