Dar: Ajali tatu tofauti zimetokea barabara ya Mandela. Inasadikiwa watu wanne wamefariki dunia

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
index.jpg

1. Ajali ya kwanza.
Wadau mnaotumia barabara ya Mandela toka Buguruni au Kigogo eneo la tabata dampo karibu na puma imetokea ajali moja mbaya na kuua mwenda kwa miguu instantly... Hapo hapo. Semi trailer moja iliyokuwa ikitokea buguruni imemgonga mwenda kwa miguu huyo ambaye alipokuwa akivuka zebra nyuma kidogo ya kituo cha puma tokea bugurun aliiona semi trailer hiyo ikija kasi.

Pengine kwa imani ya kuwa alikuwa akivukia sehemu sahihi mvukaji huyo alipoona ile gari bado inakuja kwa mshtuko alisimama na kuinyooshea mkono pasipo mafanikio ilikuja mgonga na kumrushia kilipo kituo cha puma. Mwenda zake alifariki hapo hapo.

Kutokana na lile semi trailer kwenda kuziba barabara ikawa haiwezekani kuvuka kwa eneo lile hivyo trafiki wakaamua Kuwa magari yanayotoka buguruni yaingie kulia so iwe one way mpaka kwenye mataa yarud tena kushoto. Trafik hawakuweka tahadhali kwa waenda kwa miguu.

2. Ajali ya pili.
Bahati mbaya mwenda kwa miguu mmoja akiwa anavuka akatizama upande mmoja tu wa gari zitokazo ubungo pasipojua gari zitokazo bugurun nazo zinatumia barabara hiyo hiyo. Maskini mwenda kwa miguu huyo naye aligongwa vibaya sana na kufariki hapo hapo.

Mungu awarehemu waenda zao hawa. Na awatie nguvu ndugu na jamaa zao popote pale walipo.

3. Ajali ya tatu
Nikiendelea kuwapa taarifa kuna ajali ya tatu imetokea barabara hiyo hiyo nyuma kidogo ya lile daraja!(kama sikosei ni la mto msimbazi) watu wawili waliokuwa wamepakiwa mshkaki kwenye boda boda wamegongwa na kufariki papo hapo na hivyo kutengeneza ajali ya tatu.

Habari ambazo nmezisikia toka kwa askari wa doria mmoja anasema mahali hapo jana usiku walimkamata bibi kizee mmoja mida ya saa nane. Wakamwachia aende zake. Hivyo kuna imani za kishirikina kuwa inawezekana kulikuwa na hitaj la damu mahali hapo... Hayo ni maneno ambayo yamesemwa na askari mmoja wa doria.

Tahadhali kwenye zebra.
Tunapovuka kwenye zebra tusiwaamini sana madereva au magari kwa kuamini kirahisi kuwa pale ni sehemu salama kuvuka. Usivuke kama gari haijasimama na pia tusivuke kwa madoido sana. Madereva ni binadamu na vyombo vya usafiri tusiviamini sana.

Na watu wanne wamefariki dunia kwa eneo hilo siku ya leo ndani ya masaa yasiyozidi mawili. Bwana alitoa shetani ametwaa alaaniwe.

Picha zaidi

gari.jpg
 
Bongo hapa hakikisha unapovuka hakuna magari au yashasimama kuna madereva vichwa panzi..
Vilevile sijawah ona gari inasimama zebra ya hapo tabata karibu na puma huwa watu wanaaamsha tu kama vile zebra haipo
 
Break inaweza kufail, dereva ana ni binadamu kama ww unaweza kuta kalewa au ana stress zake so unapovuka sehem yenye zabra kuwa makini sana.
 
Halafu traffic wakipiga fain madereva kwa kutotii zebra watu wanakuja na kulaumu.


Nasema tena faini hazitoshi. Dereva akiua mtu kwenye zebra afungwe life sentence na akipitisha gari raia wapo kwenye zebra afungwe kfungo cha mwaka mmoja na faini ya tsh 400,000/=
 
Back
Top Bottom