Daniel Yona na Basil Mramba wapunguziwa adhabu ya kifungo

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
Mahakama imewapunguzia kifungo cha mwaka mmoja katika miaka mitatu ya mwanzo waliohukumiwa, sasa watatumikia miaka miwili. Inatokana na rufaa yao.

Chanzo: EATV
 
Kweli serikali yetu ya CCM full siasa nimeona hapa ktk habari kuwa Basili mramba na Daniel YOna waliohukiwa miaka mitatu jela kwa kuiingizia serikali hasara ya mabilioni ya pesa leo wamepungiziwa adhabu hyo kwa kupunguziwa mwaka mmoja na hvyo wanarudi kutumikia miaka miwili...tusishangae wakapungiziwa hadi ifike miezi 6
 
Mbona watuhumiwa wa escrow hawaburuzwi mahakamani, kesi yao ina ulakini fulani
 
Huu usanii wa serikali ya ccm sijui utaisha lini. Usishangae mwakani tutaambiwa wamepunguziwa tena mwaka mmoja.wakati kuna watu wana kesi za kijinga na nyingine za kusingiziwa wanaozea jela. Ipo siku,True freedom will come to our Nation .
 
Ccm limewashuka. Na kwa namna yoyote wametia mkono wao mahakamani ili hao kina Mramba wasiachiwe huru kwa hofu ya kujiunga ukawa na kumwaga mboga, ugali na maji ya kunawa. Mbona wangeumbuka parefu! Hao kina Mramba et al wasikate tamaa kwani ipo siku watayaweka hadharani yote ili mbivu na mbichi zijulikane.
 
Mbona watuhumiwa wa escrow hawaburuzwi mahakamani, kesi yao ina ulakini fulani
mtaje japo mmoja.

Mama Tibaijuka mbona hashikwi?
Mama Tiba unamshika kwa kupewe hela na rafiki yake ruge? tumia akili. yule amehukumiwa kwa kukiuka maadili ya utumishi wa umma kwani alitakiwa atoe taarifa tu kuwa amepewa kiasi fulani cha hela toka kwa fulani ndo maana akapumzishwa kwenye baraza la mawaziri. ukimpeleka mahakamani huyo anakushinda kesi na kumlipa fidia.
 
Mbona watuhumiwa wa escrow hawaburuzwi mahakamani, kesi yao ina ulakini fulani

Kwa sababu kesi za jinai hazina ukomo wa muda wa kufunguliwa mashtaka, hao waweke viporo, watashtakiwa na serikali ijayo, kama ilivyokuwa kwa akina Mramba na Yona. Kwa hii serikali iliyopo ni vigumu kwa sababu wale wa kuweza kuchukua hatua hiyo nao ni watuhumiwa.
 
Mwakani Lowassa akiwa rais wa JMT anaburuza mahakamani Kikwete na Muhongo kwa ajili ya wizi wa escrow
 
Back
Top Bottom