Daniel Yona - leo unaamua kuzungumza?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,597
40,372
Nipashe:

Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Bw. Daniel Yona, amejitetea kuwa hakukataa kuhojiwa na Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza zabuni tata ya kampuni ya Richmond, kwa maelezo kuwa alikuwa safarini India.

Jana, vyombo vya habari vilimkariri Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Bw. Emanuel ole Naiko naye akiituhumu kamati hiyo kwamba ilikuwa na nia ya kumkomoa.

Akizungumza na Nipashe jana kwa njia ya simu, Bw. Yona ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini katika serikali ya awamu ya tatu, alijitetea kuwa hakuwapo nchini kuanzia Desemba 4 hadi 24 mwaka jana wakati kamati hiyo iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe, ikitafuta ukweli juu ya Richmond.

``Nilikuwa India na niliporudi hawakunitafuta tena, nikajua wameridhika, nikaendelea na shughuli zangu,`` alisema.

Akiwasilisha ripoti ya Richmond bungeni mapema mwezi huu, Dk. Mwakyembe, alisema:``... Pamoja na Kamati Teule kutumia vyombo vya habari kuwatia moyo watu wenye ushahidi kuhusu suala hili ili wajitokeze na kuieleza hakuna shahidi hata mmoja aliyekuja kwa hiari yake mwenyewe bila kupelekewa hati ya kuitwa.``

(Lowassa, Yona, Karamagi, walikuwa wanasubiri waitwe na wasipoitwa wanasema hawakuitwa, lakini wangeweza kujipeleka wenyewe? Je wangerudishwa?) M. M

Aidha alisema mashahidi wote waliowaletea maelezo kimaandishi kwa njia ya simu au barua, hawakuweka majina yao wala anuani zao, hivyo kuipa Kamati Teule wakati mgumu kufuatilia kauli zao.

Ilimtaja Bw. Yona kuwa alipelekewa hati za kuitwa mbele ya kamati lakini hakufika kwa maelezo kwamba alikuwa nje ya nchi.

Katika ripoti ya tume hiyo, waziri huyo wa zamani alituhumiwa kuhusika na kuipa kampuni ya Richmond Development Company LLC haki maalum ya kipekee (exclusive right) ya miezi 18 kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta.

``Ndugu Yona alitakiwa na Kamati Teule atoe maelezo kuhusu msingi wa uamuzi wake wa kuipa Richmond haki maalum ya kipekee (exclusive right) ya miezi 18 kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza mwaka 2004 wakati huo akiwa Waziri wa Nishati na Madini,`` ilisema sehemu ya ripoti hiyo.

Alipohojiwa juu ya kilichomsukuma kutoa hati ya kipekee kwa kampuni ya Richmond kujenga bomba hilo, Bw. Yona alisema maelezo juu ya kutoa hati hiyo yanaweza kupatikana kwa Kamishna wa Nishati katika wizara hiyo, Bw. Bashiri Mrindoko.

Katika ripoti hiyo ilielezwa kuwa Bw. Mrindoko aliishauri serikali kufuta mkataba na kampuni ya Richmond ya kujenga bomba hilo ambalo hadi sasa halijulikani hatma yake.

Waziri huyo alieleza kuwa hayupo serikalini na hawezi kuzungumzia tena hoja za serikali na hivyo akashauri kuwa Kamishna Mrindoko atoe ufafanuzi.

Katika ripoti ya Kamati ya Bunge, ilibaini kuwa Bw. Mrindoko ndiye aliyepinga kutolewa zabuni ya ujenzi wa bomba la mafuta kwa Richmond, japo Bw. Yona aliwapa hati ya kipekee ya ujenzi huo.

Jitihada za kumtafuta Bw. Mrindoko zinaendelea.

Wakati huo huo, Mjumbe wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza zabuni tata ya Richmond, Bw. Lucas Selelii, amesema wanaoituhumu kamati hiyo kuwa imewaonea na kuwazushia, wajiandae kutoa maelezo mbele ya Kamati ya Maadili na Haki za Bunge.

Bw. Selelii ambaye ni Mbunge wa Nzega (CCM), akizungumza na Nipashe jana kwa njia ya simu kutoka jimboni kwake, aliwaonya wanaoikashifu Kamati kukumbuka kuwa, Bunge limeweka taratibu na kanuni za kushughulikia wakosoaji kama hao.

Kuhusu madai ya Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) kuwa Kamati hiyo ina chuki dhidi ya Wamasai wa Monduli, alisema inashangaza kusikia kauli kama hizo.

Alisema TIC ni chombo cha umma kilichohusika na uwekezaji wa Richmond na kilistahili kuhojiwa ili kupata taarifa muhimu.

Alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa TIC, Bw. Emmanuel ole Naiko, kujibu hoja za msingi zilizoibuliwa na kamati badala ya kujitetea kuwa kuna mpango wa kuangamiza Wamasai wa Monduli.

Alisema kamati ilipouliza hoja ya mtaji wa mwekezaji wa Richmond, TIC haikuwa na maelezo na pia taarifa nyingine zikiwemo za majina ya wakurugenzi hazikupatikana kituoni hapo.

Alisema kituo hicho kilitoa jina la Mohamed Gire pekee kuwa mkurugenzi na kushindwa kujibu hoja za msingi zilizoibuliwa na kamati hiyo.

``Wajibu maswali makubwa yanayoibuka kama Richmond ni kampuni feki au la, waeleze kuwa kupitia Dowans inalipwa Sh. milioni 152 kila siku, waseme mkataba wake ulisainiwa na kuongezwa muda licha ya ukweli kuwa wakati huo mabwawa ya maji yalikuwa yamejaa na kumwagika,`` alishauri.

Bw. Selelii, alisema hakuna haja ya kusema kiongozi alidanganywa au hakuhojiwa kwa kuwa Kamati iliwaita wahusika lakini pia imeibua maswali mengi ambayo yanahitaji kupatiwa majibu.

Alitaka TIC ijibu hoja za wakurugenzi wamiliki wa Richmond, itoe taarifa za usajili wake na kumtaja aliyefika kuisajili kituoni hapo na pia izungumze iwapo kampuni ya uchapishaji ilistahili kupewa cheti cha kuzalisha umeme.

Katika shutuma zake juzi, Bw. ole Naiko alisema liitwa kwenye Kamati hiyo Desemba 3, mwaka jana na kujibu maswali yote chini ya kiapo akijua kamati inafanya kazi yake kwa nia njema lakini alianza kushangaa kwamba labda ilikua inamtafuta kwa kuihusisha TIC baada ya kuitwa mara kadhaa tena akitakiwa awasilishe vitabu vyote vya wageni kaunzia 2006 hadi 2007.

``Nilihisi kwamba kulikuwa na hila ya kutuhusisha na sakata hili angalau kwa kushindwa kutekeleza agizo la kamati. Kesho yake viliwasilishwa mbele ya Kamati na Mkurugenzi wa Huduma Bw. Mbilinyi.

Hata hivyo, nilimwandikia Katibu wa Bunge nikilalamika ``sumons`` za namna hii ambazo zilikuwa zinaashiria nia mbaya ya kunitafutia kosa. Sikujibiwa.``

Alisema taarifa ya Richmond ilipowasilishwa Bungeni alishtuka pale TIC iliposhutumiwa kuwapa Richmond cheti cha uwekezaji haraka na baada ya kupinga taratibu zake yenyewe na alizidi kushangaa zaidi kusikia kuwa ofisa mmoja wa TIC alitoa taarifa kwenye kamati hiyo bila kuijulisha menejimenti.

``Mkurugenzi wetu wa huduma alipopeleka kitabu mbele ya kamati aliambiwa kwamba Richmond mliwapokea kwa zulia jekundu ``red carpet`` yeye akawajibu sisi ni wajibu wetu kuwapokea wawekezaji wote vizuri lakini hili la kutandika zulia silijui.``

Mkurugenzi huyo alisema walikaa kimya ili wasijibishane na kamati lakini tatizo lilitokea baada ya baadhi ya jamaa na ndugu wa karibu kutaka kujua ukweli wa TIC kuhusika na mkataba na kama watawajibishwa kama kamati ilivyotoa hukumu kwamba wote waliohusika na Richmond wawajibishwe.

``Tumeona tusikae kimya bali tuelimishe jamii ukweli kama nilivyosema hapo awali kuna ishara za makusudi zilizofanywa ili kuihusisha TIC na sakata la Richmond.

Jumamosi iliyopita pale Monduli Askofu Michael Laiser alitahadharisha Watanzania wasihusishe Richmond na watu wanaotoka Monduli.

Hatari hii ni kujenga chuki kwa watu kutoka Monduli na tunaweza kutumbukia kwenye maangamizi ya kimbari `ethnic cleansing`.``

Alisema TIC ilitoa cheti cha uwekezaji baada ya vyombo vingine ikiwemo serikali kuisajili Richmond na kuhoji kituo kingekuwa na kigezo gani cha kuwachelewesha ama kuwanyima?

My Take:

Sasa yawezekana sisi Watanzania ni mbumbumbu, au hatujachangamka kiakili au vyovyote vile wanavyotufikiria lakini mtu kama Yona kweli anaweza kusimama na kusema anaonewa? Yaani yeye alisubiri aitwe tena, halafu aseme ameenda kijijini, halafu asubiri aitwe tena, aseme ni mgonjwa... kweli sheria itafanya kazi kweli. Hivi si Mtikila ilitolewa hati ya kumkamata na hata Mrema yalitaka kumkuta hivyo hivyo?

Hivi hawa watu wanafikiria nini? Nadhani kuna tatizo kubwa liko mbele yetu.
 
``Nilikuwa India na niliporudi hawakunitafuta tena, nikajua wameridhika, nikaendelea na shughuli zangu,`` alisema.

This guy is full of himself! Yaani mtu unapata taarifa kuwa ulikuwa unatafutwa na Kamati Teule ya Bunge kwa ajili ya issue of National interest, halafu unarudi na kukaa miguu juu ukisubiri wakutafute! My foot!! Why didn't he announce his arrival from India and let the Committee decide whether to summon him or not:confused:
 
Na huyu naye amerudia yale yale maneno ya Mkapa? Lakini hawa mbona wanatuchezea hawa?

Mzee Es wanatuchezea kwa kuwa wanajua hakuna lolote litakalo wafika maana kuna wakubwa zaidi na mikono yao ndani RDC na ndiyo chanzo cha Kiburi .So soma between the line kwamba wana anza kusafishana mkuu huoni maajabu ?
 
..Richmond walisaini memorandum of understanding na serikali ili kujenga bomba la mafuta DSM -- Mwanza.

..Wakapewa miezi 18 kukusanya nguvu na kuanza kazi za ujenzi. miezi 18 ilipofika ikadhihirika kwamba hawana uwezo mkataba wao ukafutwa. sasa hivi nadhani amepatikana mwekezaji toka Uarabuni.

..Katika kipindi hicho Yona alikuwa waziri, Msabaha alikuwa naibu, na Rutabanzibwa Katibu Mkuu.

..Yona alipaswa kwenda kutoa maelezo mbele ya kamati. Lakini kama alikosekana Yona, basi kamati ilipaswa kumhoji Msabaha, na baadaye Rutabanzibwa.

..Hata kama Kamati ilishindwa kuwapata hao wote, bado ilipaswa kutafuta nyaraka zinahusiana na negotiations na mkataba wa bomba la mafuta toka wizarani.

..Mwenye attachments za Ripoti ya Dr.Mwakyembe atupatie tuone mahojiano ya Kamati na Msabaha na Rutabanzibwa kuhusu Richmond na mradi wa bomba la mafuta.

..Kamati ya Dr.Mwakyembe imependekeza Bashiri Mrindoko achukuliwe hatua kwa kutokumshauri Katibu wake Mkuu Mwakapugi kuhusu uwezo wa kifedha wa Richmond.

..Kabla ya hapo Mrindoko aliandika barua kwa niaba ya Katibu Mkuu Nishati [Mwakapugi] ya kusitisha mkataba wa Richmond wa ujenzi wa bomba la mafuta.

NB:

gazeti limekosea linapodai Mrindoko alipinga mkataba wa bomba la mafuta. kilichotokea ni kuvunjika kwa mkataba baada ya grace period ya miezi 18 kupita. Mrindoko ndiyo aliandika barua ya kuvunja mkataba kwa niaba ya Katibu Mkuu/Wizara/Serikali.

Exclusive Rights ni jambo la kawaida ktk miradi mikubwa kama huo. huwezi kusaini mkataba wa mradi kama huo kwa wawekezaji zaidi ya mmoja.
 
Huyu, akajieleze na kujitetea huko kwenye tume ya Pinda. Anajitetea na hajui anajitetea nini, si maajabu haya jamani.
 
JokaKuu.. kuna mambo unayoyasema ni muhimu sana lakini yanashindwa kujibu maswali kadhaa.

a. Unaweza kuipa kampuni ya uwekezaji mradi mkubwa exclusive rights, wakati kampuni yenyewe haipo kisheria? Kabla ya serikali kuingia mkataba mkubwa si lazima iridhike kuwa yule anayeingia mkataba siyo tu ana uwezo wa kuingia mkataba huo bali pia yupo kisheria?

b. Kama baada ya miezi 18 wameshindwa kufanya walichotakiwa kufanya kwenye mradi wa mafuta, hata kuleta toroli la mchanga au sepetu walishindwa inakuwaje mwezi mmoja baadaye wanakubaliwa kuingia mkataba mwingine mkubwa?

c. Unapoitwa na Mahakama au Kamati Teule ya Bunge haijalishi nani mwingine ameitwa. Hivyo kuitwa Msabaha, Rutabanzibwa, n.k haviondoi au kupunguza umuhimu wa kuitwa Yona. Kila mtu anasehemu yake ya kujibu na ndio maana Sheria ya Haki, Madaraka na Kinga ya Bunge inasema kuwa kama mtu anashindwa kutokea baada ya kuitwa rasmi, basi Bunge linaweza kutoa amri kwa afisa yeyote wa Polisi kumkamata mtu huyo na kumfikisha mbele ya chombo hicho au anaweza kufunguliwa kesi mahakamani.

Nimesema wiki chache zilizopita, subirini muone watu wanatiwa Pingu. Bunge letu ni goi goi katika kutenda lakini likipewa glucose lina nguvu, na wanayoyafanya kina Lowassa na watu wake wa A21 ni kuwapa kina Sitta Glucose ya kuwashughulikia.
 
wanasheria,naomba msaada. Hivi unapoitwa mahakamani kwa kuletewa taarifa rasmi toka mahakamani au kwenye tume iliyoundwa kihalali na chombo ambacho ni mhimili wa serikali,na hukuwepo wakati unahitajika na unaporudi,Je sheria haikutaki ukaripoti kule hili ujue nini kinaendelea? Kwa kutumia common sense tu bila sheria kukutaka,nafikiri ni busara ukafika eneo la tukio na kujua kulikoni?
Yona na Mkapa wanajua hakuna sheria wala chombo chochote kinachoweza kuwabana ndiyo maana wanakuwa na kiburi. we subiri
 
Huo ni ujanja wa form two sas mtu mzima napokuwa anautumia tunahoji kama ni timamu wa akili au lah!

Alikuwa India na aliporudi hakureport ila kasubiri report imemlipua ndo anakurupuka!Mwacheni tuu ataitwa kujitetea juu ya Kiwila alafu utasikia yuko Nje.

Alafu mkuu wa kaya nae watu kama hawa ni kuwatia adabu tuu,hatuwezi kuwa na watu vihiyo apa kusumbua akili za watu.Tuna mambo mengi ya msingi ya kufanya
 
Mwanakijiji said:
JokaKuu.. kuna mambo unayoyasema ni muhimu sana lakini yanashindwa kujibu maswali kadhaa.

a. Unaweza kuipa kampuni ya uwekezaji mradi mkubwa exclusive rights, wakati kampuni yenyewe haipo kisheria? Kabla ya serikali kuingia mkataba mkubwa si lazima iridhike kuwa yule anayeingia mkataba siyo tu ana uwezo wa kuingia mkataba huo bali pia yupo kisheria?

b. Kama baada ya miezi 18 wameshindwa kufanya walichotakiwa kufanya kwenye mradi wa mafuta, hata kuleta toroli la mchanga au sepetu walishindwa inakuwaje mwezi mmoja baadaye wanakubaliwa kuingia mkataba mwingine mkubwa?

c. Unapoitwa na Mahakama au Kamati Teule ya Bunge haijalishi nani mwingine ameitwa. Hivyo kuitwa Msabaha, Rutabanzibwa, n.k haviondoi au kupunguza umuhimu wa kuitwa Yona. Kila mtu anasehemu yake ya kujibu na ndio maana Sheria ya Haki, Madaraka na Kinga ya Bunge inasema kuwa kama mtu anashindwa kutokea baada ya kuitwa rasmi, basi Bunge linaweza kutoa amri kwa afisa yeyote wa Polisi kumkamata mtu huyo na kumfikisha mbele ya chombo hicho au anaweza kufunguliwa kesi mahakamani.

Nimesema wiki chache zilizopita, subirini muone watu wanatiwa Pingu. Bunge letu ni goi goi katika kutenda lakini likipewa glucose lina nguvu, na wanayoyafanya kina Lowassa na watu wake wa A21 ni kuwapa kina Sitta Glucose ya kuwashughulikia.

Mwanakijiji,

..serikali inalazimika kujiridhisha kuhusu uhalali wa chombo chochote kile inachoingia nacho mkataba. katika hii mikataba ya Richmond kulikuwa na uzembe wa waziwazi.

..kama ulivyoeleza Richmond hawakupaswa kupewa mradi mwingine hasa baada ya kudhihirika kwamba ni wababaishaji ktk ule mradi wa bomba la mafuta.

..nakubaliana na wewe kwamba Yona alipaswa kutoa maelezo yake kwa kamati ya Mwakyembe. Lakini ni nini wajibu wa kamati hiyo ktk kutafuta ukweli baada ya Yona kushindwa kutokea?

..kwa mtizamo wangu kama Yona alishindwa/alikataa kutoa maelezo kwa kamati ya Mwakyembe, basi kamati ilipaswa kumshughulikia kwa kutumia ushahidi wa Dr.Msabaha, na Patrick Rutabanzibwa.

..kama kamati imemhukumu Lowassa bila kumtaka maelezo, kwanini imeshindwa kumhukumu Yona bila kutoa ushahidi wake kwa kamati? Kama maelezo ya Msabaha yalitosha kumhumkumu Lowassa, kwanini maelezo ya Msabaha,Rutabanzibwa,na Mrindoko, hayatoshi kumhukumu Yona?

NB:

Nimesoma mahojiano ya AG Mwanyika mbele ya kamati. Sikuona kamati ilifaidika vipi na mahojiano yale. Nadhani hata Dr.Mwakyembe alikata tamaa akaamua kukatisha mahojiano yao na Mwanyika.
 
Yona ni Yona bwana.Dawa yake ni yule aliyemnyang'anya jimbo la same basi, maana pale ni kweli alizidiwa maarifa.
 
Back
Top Bottom