Daniel Kabisi Afariki Dunia

Pezzonovante

JF-Expert Member
May 1, 2008
638
41
Mtanzani Afariki South Africa, Alikuwapo Huko Tangu Mwezi Wa Kwanza Akisoma Shahada Ya Pili,pia Alikuwa Akifundisha Chuo Kikuu Cha Tumauni Huko Iringa, Kwa Mujibu Wa Tarifa Anatalajiwa Kupelekwa Leo Tanzania Kwa Mazishi,jamaa Mlioko Huko South Ebu Tupeni Zaidi.
 
Ebwana huyu jamaa namfahamu,tulikua nae Makerere University akisomea Sheria.Ni mtu wa watu,aliwahi kua Mwenyekiti wetu wa wanafunzi wakitanzania kule chuoni.
Kukusahihisha hakua akifundisha Tumaini bali RUAHA UNIVERSITY.
R.I.P DANIEL KABISSI,umeacha pigo kwa Makerereans wenzio na hata kwa TAIFA lako.
Umeondoka ukiwa mbichi bado na taifa likiwa lakuhitaji uwanoe vijana wake pale chuoni kwako.
 
ebwana Huyu Jamaa Namfahamu,tulikua Nae Makerere University Akisomea Sheria.ni Mtu Wa Watu,aliwahi Kua Mwenyekiti Wetu Wa Wanafunzi Wakitanzania Kule Chuoni.
Kukusahihisha Hakua Akifundisha Tumaini Bali Ruaha University.
R.i.p Daniel Kabissi,umeacha Pigo Kwa Makerereans Wenzio Na Hata Kwa Taifa Lako.
Umeondoka Ukiwa Mbichi Bado Na Taifa Likiwa Lakuhitaji Uwanoe Vijana Wake Pale Chuoni Kwako.
Sawa Kabisa Kasoma Uganda,pia Juzi Aliowa Dada Wa Kiganda Wana Miaka Miwili Sasa, So Julisha Jamaa Pia Asante Kwa Masahihisho.
 
Ni simanzi,majonzi yasiyo na kifani kwetu wote Watanzania tuliofamu ndugu yetu Kabisi,
Kwetu tuliobahatika kuwa naye chuoni Makerere
Kwetu zaidi wana LUMBOX solidarity na Lumumbists kwa pekee.
Binafsi nilibahatika kuwa nae kwa ukaribu zaidi pale LUMUMBA Hall kwa mda wa miaka miwili na hata kusoma nilikuwa nasomea chumbani kwake kwani palikuwa na mazingira ya utulivu, mpangilio mzuri na kwa kweli ni sikitiko kubwa sana kwangu binafsi
Tulivumilia mengi sana,migomo ya kila mara pale,chakula kibovu mess,tear gas,kukimbizwa na askari wakati wa migomo,matatizo ya kukosa maji mara kwa mara pamoja na kuibiwa vifaa vya eletronics kama redio na TV tulipokuwa likizo.
KABISI alikuwa mcheshi si kwa Watanzania wenzake tu bali naamini,viongozi wa LUmumba Hall tukianza na Warden,custodians,wapishi,wafanya usafi pamoja na majirani wa LUMBOX SOLIDARITY
Kama si jitihada na msimamo dhabiti wa ndugu yetu KABISI (TAZAMA) chama cha wanafunzi MUK na Mbarara UN kisingelikuwa na nguvu yoyote
Upatikanaji wa vyumba
Ela ya kujikimu kutoka bodi ya mikopo
Kwa ujumla Dani alikuwa mtetezi wa maslahi yetu chuoni

Nasikitika sana nyota iloanza kuchomoza imetokomea kabla ya walio wengi kufaidika

Sie tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi na kazi ya mola haina makosa


Kwa wale wanafuatilia huu msiba kwa karibu tunaomba mtujulishe yanayojiri
 
Daniel Kabissi alifariki dunia huko South Africa siku ya jana kama aliyenihabarisha alizipata habari sahihi.
inasemekana aliugua ini kwa muda mfupi.
Alikuwa akifundisha Ruaha University kama mwajiriwa na huko Tumaini University kama part timer.
Ni kweli alioa dada mmoja mganda ambaye walitoka naye makerere na kufunga ndoa mwaka jana.
alikuwa south africa akisoma masters ya laws ambayo alitarajiwa kumaliza mwezi wa kumi na moja mwaka huu.
Nikipata taarifa zaidi from my sources nitawataarifu ila so far bado maiti ipo south africa na ninasikia wako mbioni kuuleta mwili wa marehemu.
Kwa nilivyomfahamu mimi alikuwa mtu wa watu, mcheshi, mkarimu na mchapa kazi. katika kufundisha ni mmoja kati ya walimu wazuri - hayo ni maneno ya baadhi ya wanafunzi wake.
bwana ametoa na bwana ametwaa.
 
Itei, mimi makerere pia huyu jamaa alimaliza miaka hipi? PM me and we can try to get in touch. Nimefundishwa na Kina Prof. Kakooza na Dr. Onyango
 
Bwana Ametowa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana liimidiwe. Osagefye amepumzika. Fellow Makererean, Northcorte Hall aka Bachelor Boyz/ Military Guyz
 
Daniel Kabissi alifariki dunia huko South Africa hapo jana kwa mujibu wa habari nilizozipata.

Alikuwa akisoma masters ya laws huko na alitarajiwa kumaliza mwezi wa kumi na moja mwaka huu.

Mwaka jana Alioa dada mmoja mganda ambaye walitoka naye huko Makerere.

Yeye ni mwajiriwa wa Ruaha Univeristy iliyoko Iringa na pia alikuwa akifundisha Tumaini University kama part timer.

Inasemekana aliugua ini na ndiyo chanzo cha kifo chake.

Alikuwa mtu wa watu, mkarimu, mpigania haki na mchapa kazi. Alikuwa mmoja kati ya walimu bora wa sheria katika mji huo wa iringa.

Hadi sasa inasemekana maiti bado iko south na nikipata habari zaidi nitawajulisha.

Bwana ametoa na bwana ametwaa.
 
Daniel Kabissi alifariki dunia huko South Africa hapo jana kwa mujibu wa habari nilizozipata.

Alikuwa akisoma masters ya laws huko na alitarajiwa kumaliza mwezi wa kumi na moja mwaka huu.

Mwaka jana Alioa dada mmoja mganda ambaye walitoka naye huko Makerere.

Yeye ni mwajiriwa wa Ruaha Univeristy iliyoko Iringa na pia alikuwa akifundisha Tumaini University kama part timer.

Inasemekana aliugua ini na ndiyo chanzo cha kifo chake.

Alikuwa mtu wa watu, mkarimu, mpigania haki na mchapa kazi. Alikuwa mmoja kati ya walimu bora wa sheria katika mji huo wa iringa.

Hadi sasa inasemekana maiti bado iko south na nikipata habari zaidi nitawajulisha.

Bwana ametoa na bwana ametwaa.
 
amesharudisha pesa za EPA?

Is it really fair to speak of the decesed this way, I thought we are first passing our condolences, we really ought to have even a pinch of humanity when it comes to death.
aah ukifiwa utajua uchungu wa kuambiwa maneno kama haya wakati msiba ni mbichii.

May Daniel rest in Perfect peace.
 
Taarifa rasmi kuhusu Daniel Kabisi kutoka Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal (UKZN), Afrika Kusini kama ilivyotolewa leo asubuhi:

Memorial Service Daniel Kabissi - PMB

It is with regret that we announce to the University community the passing away of Daniel Kabissi, a Master's Law student on the Pietermaritzburg campus. He had been seriously ill and passed away on Saturday 16 August at the Midlands Clinic. Our condolences go out to his wife Stella Nyana, family and friends.

The Memorial service will be held :
TODAY 19 August 20008
Denison TV Room
18h00

Napenda kutoa pole kwa wafiwa wote, pamoja na Jumuiya ya waTanzania wasomao UKZN.
 
Ndugu Watanzania Wenzangu, Poleni sana kwa kuondokewa na Mpendwa Mtanzania Mwenzetu Daniel Kabisi. Mke wake, Wazazi wake, Ndugu zake, Jamaa zake, Marafiki zake, nasi wote tulimpenda sana lakini Aliye muumba alimpenda zaidi.
Daniel Kabisi ametangulia, nasi tutafuata wakati utakapowadia.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe (Ayubu 1:21). Amen.
 
Back
Top Bottom