Daniel Chongolo fuatilia tuhuma hizi za CCM kata ya Wazo mkoani Dar es Salaam

Anonymous

Senior Member
Feb 3, 2006
125
321
Zipo tuhuma za ufisadi mkubwa wa kuuza VITALU 48 vya kujenga vibanda vya biashara kwenye eneo la CCM Kata ya Wazo lililopo jirani magereji Tegeta Wilayani Kinondoni.

Wanaotuhumiwa kushirikiana kufanya ufisadi huo ni pamoja na Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Bwana James Mgego na viongozi wa kata hiyo, waliomaliza muda wao.

Viongozi hao wa Kata ni Mwenyekiti Yusuf Chunda, Katibu Dennis Liheta na Mwenezi Deo Kamugisha.

Aidha Bwana Mgego, ameamua kuwapigania viongozi hao kwa kuwapigia kampeni ili warudi kwenye nafasi kwaajili kuficha ufisadi huo walioufanya.

Katibu huyo wilaya kila baada ya siku mbili lazima afike kwenye kata hiyo, ili kufanya mazungumza na baadhi wa makatibu wa tawi ili kuwashawishi wawafanyie kampeni viongozi hao wa kata wanaotuhumiwa kufanya ufisadi huo.

Inadaiwa kuwa tayari viongozi hao wamemzawadia Katibu wa Wilaya kiwanja cha kujenga nyumba katika eneo la Nakarekwa ili awapiganie warudi kwenye nafasi zao.

WanaCCM Kata ya Wazo, tunamwomba Bwana Mgego arejeshe heshima ndani ya chama na si kujenga ujira binafsi na maslahi ya watu wachache ambayo baadaye itaigharimu chama ndani kwa ndani.

Ni sisi Makada watiifu, wakereketwa na wafurukutwa wa Chama Cha Mapinduzi.

“KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI”
 
Asante ila usije kuwa unagombea na wewe umeanza kuwachafua wengine.

Nitafika eneo hilo.

Kidumu chama cha Mapinduzi
 
CCM uchaguzi ndani ya chama chenu umekaribia mmeanza kusagiana kunguni.

Hiki chama kwa uzandiki na ufitini, hakijambo.
 
Huyoo Katibu wa CCM wilaya nasikia kazi yake umalaya tu analala na makatibu wa matawi hatari......
 
CCM kila mtu mwizi.

Bosi wenu amekula Bilioni 7 za shooting eti alichangiwa na wadau
 
Hata uchaguzi ule wa wenyeviti serikali ya mitaa kuna maeneo walioitishwa wahuni ambao wako kwenye Magenge ya majangili wa kuvamia maeneo ya watu huko pemebezoni mwa mji.

Genge la wahuni wanaweka mhuni mvamizi mwenzao ili awe anawalinda Kwa kukwamisha maaamuzi ya Serikali toka Viongozi wa juu katika kuwapatia wananchi na wamiliki halali wa maeneo.

Hilo Chongolo analijua sababu aliwahi kuwa DC Kinondoni.

Na maeneo yenye hao Viongozi wahuni bila shaka anayajua.
 
Back
Top Bottom