Daniel Chongolo: Bodaboda na bajaji hawawezi kuondolewa katikati ya jiji la Dar es Salaam

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
CHONGOLO: BODABODA NA BAJAJI HAWAWEZI KUONDOLEWA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo Kwa upande wa zoezi linaloendelea la kuwapanga watu wa bajaji na bodaboda mkoa wa Dar es salaam kuwa watu hao, hawawezi kuondolewa katikati ya jiji hilo.

Chongolo ameyasema hayo, leo tarehe 22 Aprili, 2022 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ilala.

amesema kuwa, hao ni watu muhimu hawawezi kuachwa kwa sababu wanajitafutia riziki halali, ambapo amewasihi watu waache kutoa taarifa za kupotosha umma kuwa wanaondoshwa mjini.

“Kinachofanyika sio kuwazuia bodaboda na majaji wasiingie mjini bali ni kuwaratibu ili kuwawekea vituo rasmi zitavyoweza kutambulisha watu wanahitaji kutumia usafiri huu”, Katibu Mkuu Ndg. Chongolo amesisitiza

Ndg. Chongolo amesisitiza kuwa waendesha bajaji baadhi yao ni watu wenye ulemavu, ambao ni kundi maalum linalopata mikopo inayotolewa na Halmashauri asilimia 10, hivyo lazima waheshimiwe kwa kuwaweka eneo maalum kwa ajili yao ili wasigombanie abiria na watu wengie wasiokuwa na ulemavu.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Ndg. Chongolo ametumia mkutano huo kuwakumbusha majukumu wajumbe wa kamati za siasa za ngazi zote wakiwemo viongozi wa Jumuiya ambapo kwa sasa kwa tathimini iliyopo Kamati hizo hazitekelezi majukimu sawasawa hasa kusimamia ajenda za wananchi.
 
Attachments

  • VID-20220422-WA0025.mp4
    9.1 MB
  • VID-20220422-WA0024.mp4
    13.3 MB
Ukatibu Mkuu Ni mzuri naona Mheshimiwa dc wa zamani anazidi ku gain
 
Siku hizi vibajaji ndiyo vimekuwa daladala za mjini?

Serikali iingilie kati maana bajaji kwa kuongeza tozo katika chombo hiki cha biashara ili kuongeza mapato ya serikali pia kudhibiti wingi wa bajaji unaleta "uchafuzi" wa hewa, miundimbinu, ajali na vurugu ktk uendeshaji kwa vyombo vingine.

Lazima kuwepo na idadi maalum inayoruhusiwa ya pikipiki na bajaji za biashara zinazopewa leseni katika kila halmashauri, manispaa na jiji kwani bila udhibiti wa idadi ipo siku usafiri wa umma wa mabasi ya mwendokasi ukiogharimu mabilioni ya fedha na miundombinu yake , daladala na teksi zitakufa kabisa.
 
CCM KWA KULETA SIASA, SASA UTAUA MADHUMUNI YA UANZISHWAJI WA MRADI WA UMMA WA USAFIRI WA KASI YAANI DART

Bajaji kukwamisha nia nzuri ya serikali kuwa na mradi mkubwa wa mabilioni ya shilingi uliogharamiwa kama mkopo kujenga miundo mbinu ya barabara za usafiri wa mwendokasi pia mamia ya mabasi ya mwendokasi kukosa faida iliyotarajiwa ipatikane katika mradi huo wa mfano Kusini mwa Afrika .

Historia Miradi iliyotekelezwa na DART :

Katika kukabiliana na changamoto ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) tayari wamekamilisha ujenzi wa awamu ya kwanza km 20.9 ambao utoaji huduma ulianza rasmi Juni, 2016. Aidha, Mradi huuulizinduliwa rasmi na Mhe. Dr John Pombe Joseph Magufuli. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 25 Januari, 2017.

Kuanza kwa utekelezaji wa Mradi kumesaidia kurahisisha huduma ya usafiri ambapo hadi sasa watu tarkriban 200,000 hupata huduma ya usafiri kwa kila siku na tayari zaidi ya watu 1000 wamepata ajira kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART)

Usanifu wa awamu ya II na III umekamilika ambao umegharimu jumla ya Dola za Kimarekani milioni 289.91. Ujenzi wa awamu ya II ambao utajumuisha Kituo Kikuu katika maeneo ya Mbagala na barabara za juu (flyover) unatarajia kuanza rasmi mwishoni mwa mwaka 2018 fedha za mradi huo zimepatikana (Dola za Kimarekani Milioni 141.71)

Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Benki ya Dunia inaendelea na jitihada za kukamilisha usanifu wa awamu ya IV, V na VI wa mfumo wa DART ili kuweza kukamilisha ujenzi wa barabara zote kwa ujumla km 141.1.

Jedwali Na.23: Utekelezaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) katika Jiji la

Dar es Salaam Januari 2016 hadi Juni, 2018.

Awamu
Jina
Urefu (km)
Maelezo
I​
Barabara ya Morogoro (Kimara – Kivukoni), Barabara ya Kawawa (Morocco – Magomeni), Msimbazi – Kariakoo.
20.9​
Utoaji huduma ulianza Mei, 2016 na huduma inaendelea kutolewa.
II​
Barabara ya Kilwa, Kawawa, Magomeni – Chang’ombe
20.3​
Zabuni za ujenzi wa kumpata Mkandarasi zimetangazwa tarehe 12 Februari, 2018 (Majengo) na tarehe 05 Mei, 2018 (Barabara); Ujenzi unatarajia kuanza Mwaka huu 2018. Aidha Fidia inatarajiwa kulipwa kabla ya kuanza ujenzi.
III​
Barabara ya Nyerere, Uhuru, Bibi Titi, Azikiwe
23.6​
Usanifu umekamilika
IV​
Barabara ya Bagaomoyo – Tegeta Sam Nujoma,
25.9​
Usanifu unatarajia kuanza kufanyika kupitia Benki ya Dunia
V​
Barabara ya Mandela na Barabara mpya
22.8​
Usanifu unatarajia kuanza kufanyika kupitia Benki ya Dunia
VI​
Barabara ya Mwai Kibaki na Barabara mpya mbili.
27.6​
Usanifu unatarajia kuanza kufanyika kupitia Benki ya Dunia
JUMLA
141.1

Mafanikio ya Mradi wa DART

Katika kipindi cha Mwaka 2016/17- Mei 2018 mradi wa umepata mafanikio yafuatayo :-

Kuanza rasmi tarehe 10 Mei, 2016 kutolewa kwa Huduma ya Mpito kupitia mtoa huduma kampuni ya UDART wakazi wamenufaika na huduma Idadi ya abiria imeongezeka kutoka wastani wa 76,000 kwa Mwaka 2016 hadi 200,000 mwaka, 2018;

Huduma hii imepunguza msongamano wa magari barabarani katika eneo la Mradi awamu ya kwanza Kimara na Kivukoni ilikuwa ikichukua zaidi ya saa mbili kwa kutumia mabasi ya DART inachukua dakika 40 tu na hivyo kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi wa kila siku;

Mradi umefanikiwa hadi sasa umetoa ajira kwa watu zaidi ya 1,000 ikihusisha madereva, mafundi wa karakana, watumishi wa UDART, Watumishi wa kampuni ya ukusanyaji wa nauli; ulinzi na usafi wa vyoo, maegesho, madaraja ya watembeao kwa miguu katika mfumo wa DART;

Mradi umetoa fursa za kibiashara katika ushoroba wa mradi wa DART awamu ya kwanza ikiwemo fursa ya maegesho ya magari katika eneo la Kimara Mwisho;

Wafanyakazi na wafanyabiashara wanawahi kufika kazini na hivyo kuongeza tija na ufanisi. Kwa upande wa wanafunzi wameondokana na adha ya kunyanyaswa kwenye daladala;

Mabasi yanayotumika kwenye mfumo wa DART yana injini ambazo ni rafiki kwa mazingira;

Walemavu, akina mama wajawazito na wazee wamepewa kipaumbele katika mfumo wa DART;

Mradi umesadia kuboresha mandhari ya Jiji la Dar es Salaam; na

Mradi umefanikiwa kupata tuzo mbili za Kimataifa kuhusu utunzaji Mazingira na Usafiri endelevu.

Source : Miradi Inayosaidia Kupunguza Msongamano katika Jiji la Dar es Salaam
 
Jigjiga Town, Somali Region
Ethiopia

Mji mkubwa mashariki ya nchi ya Ethiopia wenye bajaji nyingi kuliko usafiri mwingine wa umma

CHONGOLO: BODABODA NA BAJAJI HAWAWEZI KUONDOLEWA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo Kwa upande wa zoezi linaloendelea la kuwapanga watu wa bajaji na bodaboda mkoa wa Dar es salaam kuwa watu hao, hawawezi kuondolewa katikati ya jiji hilo.

Chongolo ameyasema hayo, leo tarehe 22 Aprili, 2022 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ilala.

amesema kuwa, hao ni watu muhimu hawawezi kuachwa kwa sababu wanajitafutia riziki halali, ambapo amewasihi watu waache kutoa taarifa za kupotosha umma kuwa wanaondoshwa mjini.

“Kinachofanyika sio kuwazuia bodaboda na majaji wasiingie mjini bali ni kuwaratibu ili kuwawekea vituo rasmi zitavyoweza kutambulisha watu wanahitaji kutumia usafiri huu”, Katibu Mkuu Ndg. Chongolo amesisitiza

Ndg. Chongolo amesisitiza kuwa waendesha bajaji baadhi yao ni watu wenye ulemavu, ambao ni kundi maalum linalopata mikopo inayotolewa na Halmashauri asilimia 10, hivyo lazima waheshimiwe kwa kuwaweka eneo maalum kwa ajili yao ili wasigombanie abiria na watu wengie wasiokuwa na ulemavu.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Ndg. Chongolo ametumia mkutano huo kuwakumbusha majukumu wajumbe wa kamati za siasa za ngazi zote wakiwemo viongozi wa Jumuiya ambapo kwa sasa kwa tathimini iliyopo Kamati hizo hazitekelezi majukimu sawasawa hasa kusimamia ajenda za wananchi.
CCM sasa inaingilia uendeshaji wa Jiji la DSM.
Maovu ya bajaji na bodaboda sasa wa kulaumiwa ni Chongolo na CCM yake.
 
Siku hizi vibajaji ndiyo vimekuwa daladala za mjini?

Serikali iingilie kati maana bajaji kwa kuongeza tozo katika chombo hiki cha biashara ili kuongeza mapato ya serikali pia kudhibiti wingi wa bajaji unaleta "uchafuzi" wa hewa, miundimbinu, ajali na vurugu ktk uendeshaji kwa vyombo vingine.

Lazima kuwepo na idadi maalum inayoruhusiwa ya pikipiki na bajaji za biashara zinazopewa leseni katika kila halmashauri, manispaa na jiji kwani bila udhibiti wa idadi ipo siku usafiri wa umma wa mabasi ya mwendokasi ukiogharimu mabilioni ya fedha na miundombinu yake , daladala na teksi zitakufa kabisa.

Nakumbuka waliondoa vipanya na daladala hususan Morogoro Rd kwa utetezi kwamba were not suitable kwa kazi ya kubeba abiria. Badala yake bajaji na bodaboda zimechukua nafasi everywhere all the way. Hawana nidhamu vituoni, barabarani, everywhere. Are we moving forward or backward?
 
Aliyetoa tamko hawaruhusiwi kuingia mjini ni wao. Anayekuja kutetea wasiondolewe mjini ni wao.
Siasa za nchi zetu ndo zinafanya kila mtu atamani kuwa mwanasiasa.mana wanasiasa ndo Mungu watu . Wanafanya chochote na wanaamua chochote.
 
CCM haina dira na ni saulifu kuwa walianzisha mradi wa mamia ya million za dola za Kimarekani ili jiji la Dar es Salaam kuwa na usafiri wa ufanisi na bora wa aina ya mabasi ya mwendokasi.

Je kweli CCM wataweza kuwa na wazo pia la kuanzisha mradi wa treni za mjini unaoenda sambamba na mabasi ya mwendokasi, ikiwa CCM tayari inaturudisha nyuma tupande bodaboda na bajaji kama ndiyo usafiri rasmi wa umma katika mji mkubwa kama wa Dar es Salaam na majiji mengine nchini Tanzania ?
 
Fisiem ni kirusi kama cancer!
Tatizo dogo tumor itagharamikiwa operations, radiation, chemotherapy, kisha haifanyi Check up wala follow up, tumor Ile ikipotea, inarudi na tumor 900+...! Ugonjwa unaorudi unasambaa Kwa Kasi ya ajabu!
 
Ni uelewa mdogo kudhani kwamba njia pekee ya kujenga uchumi wa walemavu ni biashara ya bajaji. Hata kama inaathiri watumiaji wengine wa barabara za CBD.
 
23 May 2022
Dar es Salaam, Tanzania

DC wa Ubungo kuhusu matumizi bora na sahihi ya miradi ya miundombinu ya usafiri ikiwemo barabara za mwendokasi express highway

“TUSILAZIMISHE KUFA KWA AJALI, WIKI HAIISHI” MAAGIZO YA DC KHERI KWA TANROADS

Back
Top Bottom