Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,890
- 939
DANIEL CHONGOLO, KATIBU MKUU WA CCM
CHONGOLO AKEMEA WATENDAJI WA SERIKALI WANAOCHELEWESHA KUIDHINISHA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI
CHONGOLO AKEMEA WATENDAJI WA SERIKALI WANAOCHELEWESHA KUIDHINISHA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Godfrey Chongolo, akiambatana na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kukagua miradi na shughuli za maendeleo mkoani Dar Es Salaam, amekemea vikali tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali wanaohusika na kuidhinisha fedha za miradi ya ujenzi kutofanya hivyo kwa wakati licha ya Serikali kutenga na kuwepo kwa fedha za miradi hiyo.
Katibu Mkuu ameyasema hayo akiwa katika ukaguzi wa ujenzi wa soko la kisasa la Tandale Manispaa ya Kinondoni ambapo ujenzi huo unaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 8.7 ulianza tangu mwezi Septemba, 2019 ukiendelea nje ya muda uliotarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2020, jambo linalosabisha kero kwa wananchi kutokana na adha ya kukosa mahali pa kufanyia biashara kama ilivyokuwa hapo awali.
Kaimu mhandisi wa Manispaa ya Kinondani Mkerewe Tungaraza akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mradi huo, ameeleza kuwa, Kuchelewa kwa mradi huo, kumetokana na kuchelewa kwa hati za malipo na kusababisha hasara kwa serikali kwa kumlipa mkandarasi Shilingi Bilioni 2.5 nje ya makubaliano ya mkataba kutokana na nyongeza ya muda wa mkataba huo.
Ziara hii ni muendelezo wa Utekelezaji wa Maelekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mwezi Aprili Mwaka huu katika Mkutano Mkuu Maalum kwa Chama kutembelea na Kukagua Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025.
Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
13 Agosti, 2021