DANGOTE Mtwara; Mfanyakazi afariki Dunia baada ya kusagwa na mashine

sintah

Senior Member
Aug 18, 2013
187
190
Katika hali ya kushangaza mfanyakazi mmoja amekumbwa na mauti jana jioni baada ya kusagwa na mashine, inasemekana alikuwa pekee yake eneo hilo ambapo ni kinyume na taratibu za usalama, management inatumia nguvu kubwa kuzima hili tukio lisifahamike

Nitoe rai kwa vyombo vnavyohusika ikiwemo police na OSHA kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hili.
Ikumbukwe Dangote ni kiwanda kikubwa lakini swala la safety liko chini sana watu wanafanya kazi kimazoea sana alisikika mfanyakazi wa eneo hilo.

Marehemu atazikwa leo sa saba mchana na mpaka sasa hakuna aliewajibika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu awe faraja kwa familia iliyoondokewa na mpendwa wao.

Mazoea katika kazi yanaweza kuletwa na mtu mwenyewe, hasa sisi tunapenda kusimamiwa kila kitu.

Inawezekana kiwanda kina vifaa vya kujikinga ila mtu havai kwa mazoea yake binafsi.

Hili tukio halipaswi kuangaliwa kwa upande mmoja kwa sababu ya kutokea kifo, sisi wenyewe ni mashahidi mambo mengi tunafanya kwa mazoea.
 
Swala la usalam katika eneo la kazi ni la muhimu sana hasa kwa mfanyakazi mwenyewe... Mfanyakazi inatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia afya yako, inatupasa tuzingatie njia na namna mbalimbali za kuhakikisha tunakuwa salam eneo la kazi...

Tunatafta pesa kwa ajili ya mahitaji muhimu ya kila siku, moja wapo ya hayo mahitaji ni pamoja na gharama za matibabu pale tunapougua...

"Tusikubali kufanya kazi zinazohatarisha afya na usalama wetu"
 
Apumzike kwa amani marehemu
lakini baadhi ya watanzania walio wengi tuna tabia ya kudharau hizi safety gears nasemea expirience yangu nnapofanyia kazi yani mtu anapewa vitu vyote vya usalama afu havai tu kwa makusudi na anahisi anamkomoa mwajiri, inasikitisha sana
 
Cha kwanza apumzike kwa amani,hapo alipokuwapo mwenyewe kinyume na utaratibu aliamriwa kuwapo mwenyewe au yeye tu kwa mazoea alienda kufanya hiyo kazi mwenyewe?Mara nyingi maafisa usalama wa mahala pa kazi hutoa training mbalimbali na kila mahali kuna operation procedures ila mara nyingi watu hili hawazingatii,Usalama unapaswa kuzingatiwa na kila mfanyakazi,usipozingatia usalama muathirika mkuu ni wewe.Tukumbushane sisi kwa sisi,tusiangalie tu kupata mshahara mwisho wa mwezi,tuangalie mazingira ya kazi yapoje?
 
Back
Top Bottom