Dangote aongoza kwa utajiri Afrika, Mo Dewji ashika nafasi ya 16

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mfanyabiashara maarufu nchini Mohammed Dewji (Mo) ametajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 20 wa Afrika kwa ripoti ya mwaka 2020 licha ya utajiri wake kupungua kwa Dola milioni 300 (Sh692.67 bilioni).

Katika orodha hiyo ya jarida mashuhuri la Forbes kwa mwaka huu limemtaja Mo mwenye miaka 44 kama bilionea namba 16 huku mfanyabiashara wa saruji, sukari na unga (Aliko Dangote wa Nigeria) akiongoza orodha hiyo.

Utajiri wa Mo umetajwa kufikia Dola bilioni 1.6 (Sh3.69 trilioni) na anayeshikilia namba moja utajiri wake ni Dola bilioni 10.1 (Sh23.31trilioni) naye utajiri wake ukiwa umepungua kutoka bilioni 10.3 (Sh23.78 trilioni) mwaka jana.

Katika orodha ya jarida hilo mwaka jana Mo ambaye ni raia wa Tanzania anayefanya biashara mchanganyiko alikuwa nafasi ya 14 akiwa na utajiri wa Dola bilioni 1.9 (Sh4.3trilioni) hivyo kwa mwaka huu ameshuka nafasi tatu.

“Imepungua Dola milioni 300 (Sh692.67 bilioni), lakini nina watu 32,000 na mwaka huu natarajia kuwekeza Sh500 bilioni hapa hapa nchini na uwekezaji huo utatoa ajira 100,000 kwa Watanzania,” alisema Mo baada ya ripoti hiyo akiwa ndiye Mtanzania pekee aliyeingia katika orodha hiyo.
 
Simba inapunguza utajiri wa MO au ile kutekwa, next time mstoe rekodi hizi January mnajua venye tumepigika.... msitutie majaribuni.
 
Matajiri wa Tanzania wanafaidi sana, sijui ni wangapi wameingia katika stock market ili kuwafaidisha watu wengi zaidi na huyu Mo anapenda kujisifu kuwapa watu wengi ajira lakini sidhani kama anajali kuhusu mishahara na mazingira ya kazi. Pure capitalism and selfishness at its level best
 
Matajiri wa Tanzania wanafaidi sana, sijui ni wangapi wameingia katika stock market ili kuwafaidisha watu wengi zaidi na huyu Mo anapenda kujisifu kuwapa watu wengi ajira lakini sidhani kama anajali kuhusu mishahara na mazingira ya kazi. Pure capitalism and selfishness at its level best
Kuhusu mafao ni makubaliano kaka wanasema kama unaona ndogo unatafuta pazuri zaidi...ila in reality Mo ndo anaongoza kwa kuajili watu wengi zaidi afrika mashariki na kati.Nadhani kilichomahusha ni serikali kukamata soko la korosho maana ndo alikua anacontrol akmost 90%
 
Back
Top Bottom