Dangote akifunga kiwanda chake kipya cha kusindika nyanya kwa kukosekana malighafi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
xwp-1463345697795.jpeg.pagespeed.ic.wqRqW9MyrW.jpg

Dangote Tomato Processing Factory, kiwanda kipya kinachomilikiwa na tajiri namba moja Afrika, Aliko Dangote kimefungwa baada ya kukosekana kwa mali ghafi muhimu – nyanya.
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Abdulkadir Kaita, ameviambia vyombo vya habari kuwa baadhi ya mashamba ya nyanya yaliyopo kwenye majimbo ya Kano, Jigawa, Plateau, Katsina na
Kaduna, yameathiriwa na mdudu aitwaye Tuta Absoluta aliyeharibu nyanya kwenye mashamba yote na kupelekea upungufu mkubwa wa zao hilo.

Kaita alidai kuwa uzalishaji utaanza tena katika msimu ujao. Dangote Group, kampuni ya Dangote ilianzisha kiwanda cha kusindika nyanya kwa gharama ya dola milioni 20 katika jimbo la Kano mapema mwaka huu.
 
Amefunga kwa muda hadi ugonjwa utakapodhibitiwa au ndo ameachana na biashara hiyo na kufunga hicho kiwanda moja kwa moja!!?? Sijaelewa vizuri mkuu.
 
Mambo kama haya hunichanganya sana hasa pale ninapo soma mabandiko kadhaa yakihusu mafisadi kuficha pesa nchi za nje, ilhali Tanzania bado kuna fursa kubwa za uwekezaji kama huu mfano tunao uona hapa wa kilimo cha NYANYA na USINDIKAJI wa nyanya.
 
Mambo kama haya hunichanganya sana hasa pale ninapo soma mabandiko kadhaa yakihusu mafisadi kuficha pesa nchi za nje, ilhali Tanzania bado kuna fursa kubwa za uwekezaji kama huu mfano tunao uona hapa wa kilimo cha NYANYA na USINDIKAJI wa nyanya.
miradi kama hii itasaidia sana wananchi mkuu, maana wengi wanapenda kufanya kilimo lakini mazao hayana soko, dola milioni 20 ni hela ndogo sana kwa serikali ukilinganisha na faida itakayoleta
 
Back
Top Bottom