Danadana za CCM: Mahakama ya Mafisadi sasa yaitwa Mahakama ya wahujumu Uchumi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,490
54,884
Nmeshangaa sana. leo bungeni wamepeleka marekebisho ya Sheria kuhusu Uhujumu Uchumi. Tatizo linakuja pale Fisadi Polisi anapokamatwa na Polisi Mwengine.

Mfano mimi nimeona Fisadi bado taarifa nampelekea Polisi ambao Takwimu imeonesha kwamba Polisi ndio wanaongoza kwa kupokea rushwa wakifuatiwa na Mahakimu. Bado nina na Mashaka na dhamira ya dhati.

Tatizo linakuja Rais anapokua Katika Kesi. Yaani Jaji mkuu lazima ashauriane na Serikali/Rais kabla ya kuchukua hatua yoyote katika kuteua jaji au kusikiliza kesi ya Kifisadi. Kwanini Rais ahusishwe? kwani naye ana uzoefu wa Kisheria? Kisa tu ni Sera yake ndo ahusishwe?

Sio Vizuri rais kuingilia Maamuzi ya Jaji Mkuu.

separation of powers ipo wapi? Mimi naona bora hii mambo ya Mafisadi Wangeachia Mahakama wajipange kama walivoanza.

Naomba Nimshauri Rais Magufuli.

Rais Kama unataka Ufanikiwe katika Utawala wako bila kutumia nguvu sana, RUDISHA BUNGENI RASIMU YA WARIOBA. Utakuwa umemaliza Mchezo.

Huku nyuma kuna kitabu Kiliitwa Mfalme. Sijui kama bado vinapatikana.
 
Ulitaka watuhumiwa wakamatwe na RedBrigade wale wanaovaa mawani za kuchomea?
 
Dhamira ya Serikali ni njema katika kupambana na Mafisadi kwa hiyo ni vyema MH. RAIS JPM ajulishwe kwan ni yeye tu ndiye mwenye dhamana ya Uongozi baada ya kuaminiwa na kuchaguliwa na wananchi hivyo maamuzi ya Hovyo yanaweza kupunguza imani waliyonayo juu yake.
 
Unamanisha Kuwa Polisi Wakimkamata Mzee wa Vijisenti,Akitaka Kupandishwa Kizimbani,Jaji Mkuu Itabidi Kwanza Alonge na Serikali,Halafu Ateuliwe Jaji Then Ndio Serikali Itoe Go-ahead ya Kesi Kuanza?Ahahaha!
Inshort:Unamanisha Muhimili wa Mahakama Inabidi Uupigie Magoti Muhimili wa Serikali Ili Uweze Kuwashitaki na Kisha Ndio Uwafunge Ao Mafisadi?Ahahaha
 
Tuunde pia mahakama ya kuchunguza ununuzi wa nyumba za serikali back in days.
 
Unamanisha Kuwa Polisi Wakimkamata Mzee wa Vijisenti,Akitaka Kupandishwa Kizimbani,Jaji Mkuu Itabidi Kwanza Alonge na Serikali,Halafu Ateuliwe Jaji Then Ndio Serikali Itoe Go-ahead ya Kesi Kuanza?Ahahaha!
Inshort:Unamanisha Muhimili wa Mahakama Inabidi Uupigie Magoti Muhimili wa Serikali Ili Uweze Kuwashitaki na Kisha Ndio Uwafunge Ao Mafisadi?Ahahaha
Mfalme kama kachanganyikiwa vile au?

Angefuta bunge, mahakama, mpaka mawaziri abaki yeye na Jaaliwa waendeshe hayo mambo yao wenyewe
 
Wataalam wa sheria wanaelewa zaidi kuliko wewe usiyemwanasheria, consult kwanza kabla ya kuja na conclusions based on assumptions
 
Back
Top Bottom