Damu ya watanzania itadaiwa mikononi mwa CCM na serikali zake tangu mwaka 1985 mpaka sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Damu ya watanzania itadaiwa mikononi mwa CCM na serikali zake tangu mwaka 1985 mpaka sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MWINUKA E, Apr 26, 2012.

 1. M

  MWINUKA E Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dira ya Watanzania ilipotea na Nuru ya matumaini kuzamishwa kwenye matope mazito tangu mwaka 1985. Tangu wakati huo viongozi wa chama na serikali za CCM wamekuwa wakiinufaisha ardhi damu ya wa-Tanzania wasio na hatia na wanaokufa kinyume na mpango wa Mungu kwa njia mbalimbali. Ni vyema tukaelewa kuwa umwagaji damu hasa isiyo na hatia huenda sambamba na laana. Hivyo kwa hoja hiyo miongoni mwa vyama vyenye laana ni CCM. Damu za wa-Tanzania zimemwagwa kwa njia zifuatazo ambazo zimegharimu maisha ya wa-Tanzania wengi sana:
  1. Vitendo vya Wizi, Ufisadi, rushwa vinavyofanywa na viongozi wa CCM na serikali zao.
  2. Uwajibikaji mbovu wa viongozi wa CCM na serikali zake.
  3. Makada wa CCM ambao ni professional kuwa polluted na itakadi za chama na kushindwa kabisa kutetea maslahi ya wa-Tanzania wanyonge e.g Dr Bana. na wengine wengi.
  4. Kuendeleza vitendo vya ubabe na kukumbatia utendaji mbovu wa viongozi wa chama na serikali zake

  Kwa ufupi haya ni baadhi ya maeneo ambayo yamegharimu damu za wa-Tanzania wengi sana na yanaendelea kugharimu damu ya wa-Tanzania. Hivyo ni wakati wa CCM kama chama kumrudia Mungu na kutubu kwa maovu waliyowatendea wa-Tanzania. Si wakati wa CCM kuwa na moyo mgumu kama wa farao wa misri kwa hili. Kama wataendelea kukaidi Mungu hatasita kuleta pigo ambalo kila mwana- CCM atalikumbuka kwa kuwa na Moyo mgumu. Moyo wa Farao ulikuwa mgumu hadi wazaliwa wa kwanza wa kila familia walipokufa katika kila nyumba. Hatupendi na si mapenzi ya Mungu CCM ifike huko.

  CCM inapasa itubu na isitende dhambi tena ya kumwaga damu ya Watanzania.
   
Loading...