Dampo Kuu la Bidhaa Feki za Kichina lipo Kariakoo, Kenya Uganda wamelifukia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dampo Kuu la Bidhaa Feki za Kichina lipo Kariakoo, Kenya Uganda wamelifukia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mgt software, Sep 14, 2012.

 1. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  Ukweli kwamba sasa wachina wamefikia pabaya hadi kufanya soko kuu kariakoo kuwa dampo la vitu feki la bidhaa vya kichina. Haya yameziilika siku za karibuni, baada ya kuona maroli mengi ya HOME SHOPPING CENTRE yakimwaga bidhaa hizi kama mchanga. Bidha hizi ni simu mbovu za kichina zenye majina sawa na origino, mikufu iliyopakwa rangi ya silver, viatu vya plastiki, nguo za plastiki, cover simu , midori inayodumu siku moja, hata mayai feki yapo, tiles feki, dish feki TV feki, na madaso kama vile majeans yaliyochana nakushona au kuachwa vile.

  Sio kwamba hawa watu hatuwapendi bali inabidi Watanzania tuwe macho kutokupokea bidhaa hizi mbovu. Police wa kitengo cha kuzuia magendo ndogo ndogo jijini, wananufaika sana na kukamata bidhaa hizo na kuwaachia baada ya kupata mlungula, police hao hasa ni wale wa pikipiki au gari, hupewa taarifa kuwa kuna kontain linaingia na kulizingira mpaka wanapoanza kupakua, likishakamata halipelekwi popote bali wanamalizana kijuu juu. Makontaina haya hupakuliwa barabara ya mwisho inayoelekea jangwani karibu na brewaries.

  TBS ni watu wakulaumiwa sana kwani maduka mengi yenye bidhaa hizo, yamekuwepo bila kupewa adhabu kali kama watoazo kwa wengine.

  Kenya na Uganda ni nchi ambazo ziko makini(unaweza ku google uone jinsi walivyowatimua na kuwafunga) kwa kuwa wako macho zidi ya bidhaa hizi. Kwa sasa kuna kiwanda cha yeboyebo mbovu, Betri za kutengeneza na karatasi, housingi za simu , nyembe na vijiko vinavyojikunja kwa sekunde.
   
 2. kisugujira

  kisugujira JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 769
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Watanzania ni wapole na wakarimu sana kwa wageni. Utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wetu unatia wasiwasi. Bidhaa zisizo na ubora (Fake) hazitoki nje ya nchi tu. Hata hapa nchini kuna viwanda vinavyotengeneza bidhaa zenye viwango vya chini kabisa kwa matumizi ya binadamu.

  Mfano mzuri upo pale Tabata Matumbi kwenye kiwanda cha Super Sippy Ltd. Kiwanda hiki kinatengeneza juice zisizo na ubora (Fake) kabisa ambazo hata wafanyakazi wake wanaogopa kuzinywa. Juice hizo ni za aina ya Chunky Pineapple, Chunky Orange, Chunky Mango na Beverages zingine.

  Cha kushangaza juice hizo hubadilika rangi hata kabla ya muda (Expiring Date) wake wa kuwa sokoni kuisha! Hizi Chunky juice zote hubadilika na kuwa kama uji wa sembe! Lakini cha kushangaza ni kwamba kiwanda hicho kinafahamika na mamlaka husika na kina certificates nyingi tu toka TFDA.

  Nawashauri wahusika (TFDA na TBS) kutumia muda mwingi na ipasavyo katika kukagua ubora wa bidhaa kabla na baada ya kutoka viwandani na nje ya nchi. Rushwa zinazotolewa na kupokelewa na baadhi ya watendaji katika ofisi hizi, itaendelea kutumaliza kwa kutuua kila siku. Tuwe wazalendo na tuipende nchi yetu na watu wake.
   
 3. Mkali Tozz

  Mkali Tozz JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh! Hata hao wauzaji nao watakua ni feki, sio watu orijino.
   
 4. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  wauzaji sio fake, ila TBS TDFA feki, kwani wanaajiri wakaguzi feki na , na mitambo ya feki ya kukaguria
   
 5. M

  Mwalufunamba JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kariakoo ni soko la kupitishia takataka ambazo tunazinunua na tunazipeleka nyumbani kwetu. Zikiisha kuwa nyingi nyumbani tunazipeleka kwenye madampo yaliyotengwa na jiji.

  Think more than twice unapotaka kununua kitu Kariakoo.
   
 6. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  .
  Hii ndio bongo bana. Hata mwathirika wa ukimwi anatengenezewa ARV's feki ili asije kufa kabla ya kuwatajirisha wenye uchu wa utajiri wa kichina.
  .
   
Loading...