Damascus: Jeshi la Anga la Israel (IAF) limefanya mashambulizi ya Anga nchini Syria

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Sep 25, 2018
1,114
3,768
Msemaji wa Jeshi la Israel amesema kwamba Ndege za Jeshi la Israel F-16 zimefanya mashambulizi ya Anga katika mji mkuu wa Syria, Damascus.

Mashambulizi hayo yanasemekana yalilenga Vituo vya kijeshi vya wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran. Israel iliweka wazi kwamba uwepo wa Iran kijeshi nchini Syria Ni Mstari mwekundu kwa Israel.

Haya yanajiri huku Zaidi ya Wapalestina 120 wakijeruhiwa na Wengine 11 kuuawa baada ya Israel Kuvamia kwenye Msikiti wa Al-Aqsa siku ya Alhamisi Asubuhi. Zaidi ya Wapalestina 200 wamewekwa Mahabusu baada ya kile Israel inachokiita Ni Ugaidi unaofanywa na Magaidi wa Hamas dhidi ya Raia wa Israel.

State media say attack occurred before midnight, adding that some Israeli missiles were shot down by Syrian defences.

Source: Aljazeera
 
Israel hawekewi vikwazo,why?Israel wanasema uwepo wa wapiganaji wa Iran nchini Syria sio salama Kwa Israel!


Nadhani watu wanapaswa kumwelewa Putin pia Kwa kigezo hicho!
 
Ukiwa partner was USA unaweza chapa mtu yoyote kibao wakati wowote na usiulizwe na mtu
Israel yuko kote kote kwa Marekani, Uingereza na Russia vile vile kwani hao wote chimbuko lao ni Yakobo.

Wewe ukiona watu wanaopenda vita na ambao kwao vita ni sawa na "hobby" na asili ya majina yao ni sawa na yale ya kwenye Biblia basi utajua tu wana vinasaba vya nani, wala haisumbui hiyo.
 
Ukraine au mwingine yoyote hakuwahi kufanya shambulizi lolote ndani ya Urusi.
Iran amefanya shambulizi gani Israel?

Sababu tuliyoiona akiitoa Israel ni kuwa Iran ana wanamgambo Syria,jambo ambalo hawezi kukubali!

So Israel kaenda kushambulia nchi nyingine kisa Ina wanamgambo wa mahasimu wake!
 
Israel yuko kote kote kwa Marekani, Uingereza na Russia vile vile kwani hao wote chimbuko lao ni Yakobo.

Wewe ukiona watu wanaopenda vita na ambao kwao vita ni sawa na "hobby" na asili ya majina yao ni sawa na yale ya kwenye Biblia basi utajua tu wana vinasaba vya nani, wala haisumbui hiyo.
Leta ushahidi wa hili
 
Kwanini Israel na yeye asipige bomu moja kwa moja Tehran badala ya kuiharibu Damascus.?
 
Back
Top Bottom