Damas Ndumbaro: Ukusanyaji wa maoni ya Sheria mpya ya Ndoa umekamilika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Fuatilia yanayojiri Bungeni leo Aprili 25, 2023 kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 13.



Uamuzi wa Serikali kuondoa Msamaha wa kodi kwenye Taulo za kike na Vishkwambi
Waziri Hamad Hassan Chande amesema serikali iliamua kuchukua uamuzi wa kufuta msamaha wa kodi ya VAT (mbali na hatua nyingine zilizochokuliwa) kwenye vishkwambi na taulo za kike baada ya baadhi ya wafanyabiashara kwenye kinyume na utaratibu uliyowekwa na kuhakikisha wafanyabiashara hao wanalipa kodi stahiki.

Waziri Chande ameyasema hayo baada ya kuulizwa swali na Mbunge Issa Mtevu alieuliza serikali imechukua hatua gani baada ya msamaha wa VAT aliotolewa kwenye vishkwambi na taulo za kike kutokuwa na tija.

Muswada wa Sheria mpya ya ndoa unakuja
Waziri wa Katiba na Sheria, Damas Ndumbaro amesema Serikali imekamilisha mchakato wa kukusanya maoni kwenye sheria ya ndoa umekamilika na Aprili 26, 2023 Kutakuwa na kongamano la mwisho la kupitia maoni hayo ambayo baadae yatapelekwa Bungeni kama Muswada.
 
Rubber stamp
Bunge la chama kimoja lililoasisiwa na mtu mmoja kwa sababu alitaka atutawale milele mungu akaingilia kati akamfyeka fyeeee
 
Sasa hayo maoni wameyakusanyia wapi? Wasije kua wamejifungia huko wenyewe wakajitungia wao wenyewe tu.
 
Lile ombi letu sisi akina alimbususu alikasusu la kuoa watoto wa miaka kumi na nne naomba ilo pendekezo lifutwe
 
Lile ombi letu sisi akina alimbususu alikasusu la kuoa watoto wa miaka kumi na nne naomba ilo pendekezo lifutwe
Hata hivyo kuolewa na miaka 18 ni upendeleo kwa mabazazi. Kimsingi, mwanamke alitakiwa aruhusiwe kuolewa na miaka 20 na mwanaume alitakiwa aruhusiwe kuoa akiwa na miaka 21!
Kama wataleta sheria inayoruhusu mwanamke kuolewa chini ya miaka 20 na mwanaume kuoa chini ya miaka 21, basi waweke clause inayosema kuwa in an event that a female patner or a male patner who entered into marriage before attaining that age can request a court to declare the marriage contract null or avoidable in an event that one patner feel his/ her life (wellbeing)is in danger or feels that he was coerced or if he/she feel that there was undue influence that caused that marriage to take place.
 
Back
Top Bottom