Dalili zote zinaonyesha ushindi kwa CCM ni lazima

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Na Emmanuel J. Shilatu

Uchaguzi mdogo wa marudio wa Ubunge na Udiwani unatarajia kufanyika nchini Jumapili Agosti 12, 2018 ili kuziba nafasi zilizo wazi.

Pasipo kupepesa wala kumung'unya maneno dalili zote zinaonyesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaibuka na ushindi mnono.

Kwanza; Muundo wa Chama Cha Mapinduzi unaipa fursa ya kipekee na kubwa ya kuibuka na ushindi. Muundo wa CCM upo kuanzia ngazi ya shina yaani pale palipo na kaya ndipo CCM ilipoanzia. Karibu kila kaya kuna Mwana/Wana CCM tofauti kabisa na ilivyo miundo ya vyama vingine ambavyo havina mizizi wala mitawanyiko ya uhakika ya Wanachama wake. Kupitia muundo CCM itavuna kura nyingi kupitia Wanachama wake.

Pili; Sera imara za CCM ni nguzo ya ushindi. Kutokana na misingi imara iliyowekwa na waasisi wa Taifa hili tokea TANU na ASP hadi sasa CCM ambayo imeendelea kurithiwa na kudumishwa na awamu mbalimbali za uongozi, CCM ni chama pekee kinacho tumainiwa na Watanzania katika kudumisha umoja, upendo, mshikamano, amani, ulinzi na usalama wa Taifa hili. Sera safi za Serikali ya CCM ndizo nguzo za maendeleo na fahari ya Taifa letu la Tanzania.

Hata kitendo cha Wapinzani kujiondoa kwenye vyama vyao na kujiunga na CCM ni dalili tosha la wapinzani kukubali sera safi za Chama Cha Mapinduzi.

Tatu; Utekelezaji wa ilani ya uchaguzi. CCM ndio chama dola pekee ambalo ilani yake ina aminiwa na kuungwa mkono na Wananchi walio wengi na kuibuka kidedea kwenye chaguzi kuu. Uwepo wa ilani safi ya uchaguzi inayoeleweka, inayoungwa mkono na inayotekelezeka ni chachu ya Wananchi kuwa na imani na kuichagua CCM kwenye sanduku la kura. Maendeleo tunayoyaona hapa nchini ni kwa sababu ya uwepo wa ilani ya uchaguzi ya CCM inayojua hitaji, shida na daima ipo kutatua matatizo ya Wananchi wake.

Nne; Haiba ya viongozi wanaokubalika na kuuzika kwa jamii. CCM hufanya uteuzi wake kwa umakini kwa kuangalia nani ni nani kwa jamii, anakubalika vipi, mienendo yake ipoje, tabia zake zipoje, historia ya maisha yake ipoje nk. CCM kamwe haiwezi kumsimamisha mlevi, mpigaji vibao na mitama kwa Mama yake nk. Uzuri na umakini wa uteuzi wa mgombea wa CCM huleta ushawishi kwa wapiga kura kuichagua CCM.

Tano; Umoja na mshikamano uliopo CCM husaidia vilivyo ushindi. Siku zote CCM huamini na kusimama katika sera ya umoja ni ushindi ambapo huanza kushirikiana vilivyo nyakati zote kuanzia kwenye uchukuaji fomu, uteuzi, kampeni na uchaguzi. Hali hii ni tofauti kabisa upande wa vyama vya upinzani ambao wanasumbuliwa na tatizo kubwa la makundi na mpasuko wa kisiasa uliopo miongoni mwao ambapo suala la kusigana ni jambo la kawaida kwani huwa kuna pande ina mwaga ugali na nyingine inamwaga mboga. Kwa namna hiyo ushindi utatoka wapi kwa wapinzani?

CCM ipo chini ya Uenyekiti wa Kiongozi shupavu, mweledi, jasiri Dk. John Pombe Joseph Magufuli. Dalili zote zinaonyesha ushindi kwa CCM ni lazima.

*Shilatu E.J*
 
Wekeni tume huru basi ili tuamini maneno yako,refa (nec) mnateua wenyewe kisha mnajitapa kuna uchaguzi.
Ungekuwa unahitaji tume huru nadhani usingeingia kwenye mpambano.

Ni upumbavu kuingia kwenye mpambano wakati unajua refa hawezi kukupa ushindi hata kama utashinda!
 
Ungekuwa unahitaji tume huru nadhani usingeingia kwenye mpambano.

Ni upumbavu kuingia kwenye mpambano wakati unajua refa hawezi kukupa ushindi hata kama utashinda!
Kuiba kura na kutumia vyombo vya dola kubaki madarakan wakati mnajuwa refa ni wenu pia ni upumbavu.
 
Wekeni tume huru basi ili tuamini maneno yako,refa (nec) mnateua wenyewe kisha mnajitapa kuna uchaguzi.
Hakuna atakayekuwekea wewe tume huru Afrika,hakuna,tume huru inapiganiwa mlipata nafasi kipindi cha JK mkaenda kunywa juice na kuondoka,mkashindwa kudemand vitu vya msingi...
 
Uwepo WA upinzani ndo mafanikio ya CCM. Ibueni hoja CCM inazifanyia kazi na kupeta kwenye chaguzi.huko kwenye upinzani naona wingu tu.
 
Hakuna atakayekuwekea wewe tume huru Afrika,hakuna,tume huru inapiganiwa mlipata nafasi kipindi cha JK mkaenda kunywa juice na kuondoka,mkashindwa kudemand vitu vya msingi...
Unataka kusema nini?matakwa ya katiba na tume huru ni matakwa ya watanzania wa leo,sio ihisani ya jk wala ccm.
 
Unataka kusema nini?matakwa ya katiba na tume huru ni matakwa ya watanzania wa leo,sio ihisani ya jk wala ccm.
haya isubiri hiyo katiba yako iwapatie Tume huru mnayoitaka,Afrika hakunaga Tume Huru tume huru inapiganiwa.....
 
Back
Top Bottom