Dalili za wanawake wanaosaliti ndoa zao……………!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Dalili za wanawake wanaosaliti ndoa zao hazitofautiani sana na zile za wanaume. Kuna maelezo ya kitaalamu kwamba, mwanamke anapotoka nje ya ndoa yake, inakuwa rahisi sana kubainika au kufumaniwa kuliko ilivyo kwa mwanaume. Hii inatokana na ukweli kwamba, hisia zinakuwa na nafasi kubwa sana kwa mwanamke, kwani mwanamke huishi kwa hisia zaidi kuliko mwanaume. Bado nasisitiza kwamba, haipaswi na siyo sahihi mtu kuchukulia dalili hizi kama ushahidi wa mpenzi wake kutoka nje ya ndoa. Uchunguzi kufuatia dalili ni muhimu sana.

Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya dalili zinazoweza kuoneshwa na mwanamke ambaye anatoka nje ya ndoa yake:

1. Kuchelewa: Kuna wakati mwanamke anaweza kuaga kwamba anakwenda saluni au kusuka, badala ya kurejea kwa muda ambao umezoeleka, anachukua muda mrefu hata mara tatu zaidi. kuna wakati kwenda sokoni huchukua saa kadhaa bila kujali soko liko umbali gani. Kama ni mara moja sawa, lakini ikishakuwa zaidi ya mara moja, huenda kuna tatizo la kukosa uaminifu.

2. Kubadili maeneo: hebu chukulia kwamba, mwanamke amezoea kwenda soko fulani la karibu, hospitali fulani ya karibu, saluni fulani ya karibu na hata nyumba fulani ya ibada ya karibu. Unapoona anahama maeneo ya karibu ya huduma na kwenda ya mbali, bila sababu ya msingi, huna budi kuanza kutuhumu mwenendo mbaya. Siyo lazima kuhama kokote kuwe na mwenendo mbaya, lakini kama kuhama kwenyewe kunatia shaka kwa sababu maelezo ya kuhama huko hayana mashiko, mwanaume ana kila sababu ya kuchunguza kama hakuna usaliti unaofanywa.

3. Ununuzi usio wa kawaida: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake kwa ajili ya kupata fedha, basi atakuwa na mabadiliko makubwa katika mtindo wake wa manunuzi.atakuwa ananunua vitu vya thamani kubwa kuliko uwezo wake, atakuwa na fedha nyingi tofauti na ambazo angekuwa nazo na pengine kumiliki mali kama nyumba kwa siri.

4. Kuzungumzia kuachwa: Kuna wakati mwanamke anaweza kuwa anatoa kauli za kuonesha kwamba, kama mwanaume anaona vipi , wanaweza kuachana. Kama kila penye ugomvi kidogo tu mwanamke anakimbilia kusema, ‘kama ni kuachana, tuachane tu' hiyo inaweza kuwa ni dalili mbaya kwa mwanamke anayetoka nje ya ndoa kwa sababu hana tena upendo na mumewe. Lakini pale ambapo mwanaume ni mkorofi, kauli kama hizi zinaweza kutolewa, hata kama mwanamke hatoki nje ya ndoa yake. Kwa hiyo kabla ya kumtuhumu, mwanaume anatakiwa awe mkweli kwa nafsi yake kuhusu anavyomtendea mkewe.

5. Kusitisha uaminifu: Mwanamke anayetoka nje ya ndoa, mara nyingi husimamisha kumwamini mumewe, yaani hayuko tayari kushiriki masuala ya siri, ambayo wanandoa huwa wanashiriki. Husita kumshirikishamumewe kwenye mambo yake mengi. Lakini pia husita kumuomba mumewe ushauri, kama alivyokuwa akifanya siku za nyuma.

6. Kuacha kuvaa pete: Kuna sababu nyingi ni kwa nini mwanamke anaweza kuacha kuvaa pete yake ya ndoa. Moja ya sababu hizo ni kusalitiwa na mumewe au ndoa yake kuwa kwenye misukosuko mikubwa sana. Lakini nje ya misukosuko mikubwa ya ndoa, sababu nyingine inayoweza kumpelekea mwanamke kuvua mara kwa mara au moja kwa moja pete yake ya ndoa, ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa yake.

7. Kuonesha wasiwasi: kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake , ni lazima atakuwa na wasiwasi na mashaka yasiyo na sababu mbele ya mume wake. Anaweza kuonesha kutotulia kwa aina fulani kama kwamba, anahofia kuna siri nitatoka au kuna kitu ambacho tayari mume wake anakijua dhidi yake. Mara nyingi wasiwasi na mashaka humtawala sana mwanamke anayetoka nje , hasa katika hatua za zake za awali za kutoka nje.

8. Kuanzisha vurugu: Kuna wakati mwanamke anayetoka nje ya ndoa huanzisha vurugu za makusudi na mumewe. Lengo la kuanzisha vurugu hizo ni ili apate nafasi ya kujifanya amezira na kuondoka nyumbani kwa muda. Huo muda anapoondoka nyumbani kujifanya kakerwa na vurugu hizo ndiyo muda ambao anautumia kwenda kwa hawara yake
 
si nia yangu wanaume wawe wachunguzi, bali nimeweka viashiria kama angalizo kwa wale wenye mashaka na uaminifu kwa wenza wao..........

wanawake wengi wa siku hizi wako hivyo...awe ana cheat or not....

Sasa hapo kazi ipo....lol
 
Hiyo namba 1 waifu wa mjombaangu anayo sana hiyo acha nianze kukachunguza, kanajifanya kanaenda saluni , kwanza kanachelewa, halaf kakiludi manywele yako vile vile kanajifanya kuna mteja kamaliza mafuta saluni kameambiwa kalejee tena sku ya pili, na mjomba nalo utaona linacheka tu limeriziika.
Wanawake bana!
 
hiyo namba 1 waifu wa mjombaangu anayo sana hiyo acha nianze kukachunguza, kanajifanya kanaenda saluni , kwanza kanachelewa, halaf kakiludi manywele yako vile vile kanajifanya kuna mteja kamaliza mafuta saluni kameambiwa kalejee tena sku ya pili, na mjomba nalo utaona linacheka tu limeriziika.
Wanawake bana!

duh....uswazi tunaita mjomba wako 'mume *****' lol
 
Mkuu TB mimi bata namchunguza bana! huo msemo wa bata ukimchunguza humli umeanzishwa na kinamama ili wapate kucheat.
Nimewashtukia long time.

hongera kwa ujasili....tatizo la kuchunguza sio 'kuchunguza tu'
tatizo la kuchunguza ni nini utafanya baada ya....
1.umegundua kitu na huna ushahidi..
2.umechunguza na umejua ukweli na unaumia..
3.umechunguza na amejua unachunguza na huna ulichopata..
3umechunguza na umegundua kitu na umeshindwa chukua maamuzi yaliyotegemewa ..lol
4 the list goes on lol
 
hongera kwa ujasili....tatizo la kuchunguza sio 'kuchunguza tu'
tatizo la kuchunguza ni nini utafanya baada ya....
1.umegundua kitu na huna ushahidi..
2.umechunguza na umejua ukweli na unaumia..
3.umechunguza na amejua unachunguza na huna ulichopata..
3umechunguza na umegundua kitu na umeshindwa chukua maamuzi yaliyotegemewa ..lol
4 the list goes on lol

Unajua siwezi chunguza from nowhere, nakusudia nikiona hivo viashiria basi nachunguza, yaani waifu atoke anakwenda saluni nywele zimetulia na akiludi manywele yamevutwa vutwa halaf niseme bata ukimchunguza haumli?
Nachunguza bana na nikigundua tu basi sku ya pili naanzisha sredi ya kutafta mchumba JF. Hapa ndio tunaona umuhimu wa jukwaa la love connect.
 
Mkuu TB mimi bata namchunguza bana! huo msemo wa bata
ukimchunguza humli umeanzishwa na kinamama ili wapate kucheat.
Nimewashtukia long time.
Safi mkuu mi nachunguza 100% lazima umchunguze bana
kama haliki basi acha utakula Uyoga.
 
hongera kwa ujasili....tatizo la kuchunguza sio 'kuchunguza tu'
tatizo la kuchunguza ni nini utafanya baada ya....
1.umegundua kitu na huna ushahidi..
2.umechunguza na umejua ukweli na unaumia..
3.umechunguza na amejua unachunguza na huna ulichopata..
3umechunguza na umegundua kitu na umeshindwa chukua maamuzi yaliyotegemewa ..lol
4 the list goes on lol

Ni kweli The Boss, katika mfululizo wa Thread zangu humu niliwahi kuandika thread moja hapa yenye kichwa cha habari kisemacho, "Umemfumania, sasa unasemaje" katika thread hiyo nilijitahidi kujibu baadhi ya maswali ambayo huenda aliyefumania yanaweza kumsaidia kufikia uamuzi mzuri, lakini pia ninaandaa thread itakayojibu maswali hayo uliyouliza, ili kuondoa ile dhana kwamba mtu akifumania ni lazima kuachana...........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom