Dalili za kutapeliwa penzi lako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dalili za kutapeliwa penzi lako

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ZionTZ, Dec 22, 2009.

 1. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hizi ni dalili za kupigwa kibuti na mpenzi wako, zipo nyingi sana am sure of that, kama vipi wakuu mlioguswa/mnaojua zinginezo zileteni tuhabarishane mazee...


  [​IMG]
  A: Anapata kigugumizi kukutambulisha kwa rafiki zake na ndugu na inapotokea amebanwa hafikishi ujumbe kwa kiwango timilifu.

  B:Haoneshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleao, kwake ni kufuja pesa na anapokosa kupewa pesa ni mwepesi kulalamika na wakati mwingine kununa kabisa. Mtu wa kuangalia maslahi zaidi kuliko upendo.

  C:Anaahirisha mara kwa mara kukutana na wewe tena bila kukueleza sababu za msingi au kukutungia uongo wa dhahiri na kuusisitiza bila kuona aibu.

  D:Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanaume/mwanamke amtakaye sifa zake zinakuwa hazilingani na wewe. Anaweza kukuambia napenda kuishi na mwanaume/mwanamke mwenye gari au mwenye mwili mkubwa, sifa ambazo wewe huna!

  E:Hacheki kwa furaha hata kama ukimchekesha haoneshi furaha ya moyoni. Tena mara nyingine anakuwa mkimya na mshawishi mkubwa wa kuachana kutoka kwenye matembezi yenu ya jioni. “Aaah, mi nimechoka narudi nyumbani. Nitachelewa ”

  F: Anajaribu kukuunganisha na wanawake/wanaume wengine na haoni vibaya anaposikia unamfukuzia mwingine badala yake anakutia moyo wa kuendelea na usaliti wako. Hana wivu kabisa.

  G:Hajuti anapokukosea, mwepesi wa kujitenga, kutokuzungumza nawe na mwingi wa kukusukumia makosa hata kama yeye ndiye aliyekukosea.

  H:Msambazaji wa habari za udhaifu wako na mtu asiyekusifia mbele za wenzake. Si balozi mwema kwa familia yake, haishi kukuponda mbele ya wazazi na ndugu zake.

  I:Mwepesi wa kupokea na si wa kutoa mmiliki wa mali zako na mkumbatiaji wa mali zake pia. Msiri wa mipango yake na mtu anayependa kujua zaidi ya kwako kuliko wewe kujua yake.

  J: Hathamini uwepo wako na anakuchukulia kama mtu wa akiba. Hakumis unapokuwa haupo, hahisi upweke wala hakukumbuki unapokuwa mbali naye.

  K:Hakutii moyo unaposhindwa na mara nyingine hahuzuniki nawe unapokuwa una shida,. Hachukui huzuni yako kama yake, hakufariji na hakusaidii kutatua kilichokwama.

  L:Mhamasishaji wa uasi hasa wa watoto na ndugu, anayeweza kuchochea hisia za jamii ikuone mbaya, ikudharau na wakati mwingine ikutenge. Mwenezaji wa sifa zako mbaya.

  M:Hakupi kipaumbele katika maamuzi, anajiona yeye ndiye wa kwanza na wewe ni mtu wa kufuata hata unapopinga hasitishi dhamira yake ya kutenda.

  N:Humsisimui katika mambo ya faragha, anakuchukulia kama ndugu yake.


  O: Hakuhudumii tendo la ndoa mpaka siku amependa mwenyewe. Ni mwingi wa sababu za kuchoka kusingizia ugonjwa na mwenye kuhisi kero ya kucheza nawe mchezo wa kikubwa.

  P: Hazungumzii maendeleo yenu, mwepesi wa kushawishi vilivyopatikana viuzwe ili atimize hitaji lake. “Niuze simu yangu niende kuwaona wazazi, kama vipi tuuze hiki ili nijikwamue kimatatizo. Tapeli wa mali !”


  Q : Hataki kuambiwa ukweli na anapotokea akaambiwa anajitetea kwa kumtaja mwanaume/mwanamke mwingine. “Mbona fulani na fulani hawafanyiani hivi na mpenzi wake sisi tu!
  S: Hasamehe na kusahau. Kosa la mwaka juzi analijengea hoja.

  R: Mwepesi wa kutoa kauli za kutengana na asiyeogopa kuachwa. “Kama vipi kila mtu akae kivyake maana naona unaniboa tu, unadhani nitashindwa kuishi bila wewe”

   
 2. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  N:Humsisimui katika mambo ya faragha, anakuchukulia kama ndugu yake.

  hii 'N' kiboko, nimeikubali
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Baadaye inapelekea maambukizi ya ukimwi!
   
 4. g

  gasper mdee New Member

  #4
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tena c mdogo wa kukasirika hata kwa mambo yasiyo ya msingi na kuwa anapenda yeye afanyiwe mambo flani zaidi ya anavyokufanyia
   
Loading...