Dalili za kushindwa mradi wa BRT ziko wazi

Nadhani wanatakiwa kuongeza Magari...

Pia ukaguzi wa mara kwa mara ufanyike kuona kama kuna baadhi ya Magari yanakaa yard bila kutoa huduma...ni mradi mzuri iwapo mapungufu yake yatafanyiwa kazi.

Pia waongeze udhibiti kwani wale walioko kwenye vijigeti wanachakachua risiti haswa.
 
Ile biashara wanaendesha kihasara au muendeshaji anapiga hela za watu
 
Ukitaka kujua kwamba tunakurupuka jiukize
Mwendo kasi
Frayover ubungo
Frayover tazara
Teni mwendo kasi kwenda Moro

Hakuna tunachofanya kwa mafanikio
Hakuna kukurupuka jamaa ni result oriented yeye ni kazi tu hakuna maneno, kinachotakiwa pale ni kutafuta mtaalamu wa queuing system mabasi hayana uratibu mzuri hata kidogo, ni uratibu tu unaotakiwa. Inaonekana kuna madereva wa madaladala wameajiriwa bila kupewa semina elekezi
 
Inabidi uwe unawahi mapema, kwani ukifika kituoni saa 1245 kunakuwa afadhali vinginevyo ni mieleka kila mahali
Sio suluhisho la tatizo lililopo mkuu.
1. Ili usafiri uitwe reliable inabidi asilazimike mtu kulala kituoni.
2. Kila mtu akiwahi huo muda unaosema wewe, hapo kituoni hali itakuwa ile ile.
3. Muanzisha mada hakuomba ushauri juu ya yeye afanyeje, ameizungumzia hali ya utendaji kwa ujumla

Kuna watu wanajitumbukiza kwenye issues nzito za maafisa elimu huku kazi zao zimelala.
 
Nilitakaga kupanga nyumba Kimara, ila baada ya kupigwa vipepsi na kuminywa mbavu kwenye kugombania basi ikabidi tu nibaki huku niliko...
 
Tumekaa kituo cha kimara in dk 50 sasa sioni kinachoendelea,watu ni wengi anaingia mmoja mmoja kwa taratibu sana huku machine zikishindwa kusoma ticket,hapa wafanyakazi kila mmoja yupo busy na simu anachati,je ni kweli tutaweza kuendesha viwanda??
We are not ready to address our challenges. Very sad. Tumekaa kupokea mishahara tu
 
Hapana uo mradi haujashidwa mm binafsi niriwahi kufika pale nikaongea mengi na msemaji Mr.Deus akasema kinachosababishia huo mradi changamoto ni kuwa siasa hasa kwenye suala la nauli serikali inawapangia wakati wao operating cost zinakuwa kubwa kuliko wanachokipata mkuu
 
Majanga, hadi system imezidiwa...Poleni sana ndugu... DART inabid waboreshe mfumo wao, uendane na mahitaji ya watu
Naona namba inakushinda sasa mkuu,"it is very easy to be number one,but it is not easy to remain number one!"
 
Inabidi uwe unawahi mapema, kwani ukifika kituoni saa 1245 kunakuwa afadhali vinginevyo ni mieleka kila mahali
asa kila mtu ana ratiba yake, mie nifike mida hiyo wakati sehemu nayoenda sihitajiki huo muda.

usafiri unatakiwa kuwa wa uwakika muda wote. na siyo kwa muda fulani. hizo ni dalili za kushindwa.
 
Huu mradi una ufisadi mkubwa sana,hata Rais anafahamu kuwa Simon Kisena ambaye ndiyo mmiliki wa huu mradi ni tapeli na fisadi mkubwa.

Rais alipokuwa Mwanza kwenye uwanja wa Furahisha aliagiza mali za Nyanza Cooperative Union(NCU) zilizochukuliwa kifisadi na Kisena zirudishwe na TAKUKURU wachunguze uwizi huo.Ile New Era Ginnery ni ya huyuhyu tapeli Kisena.

Alipomaliza kutapeli kanda ya ziwa,akahamia Dsm...Akamuingiza mjini yule muhindi wa magari ya HEICHER,akampa lundo la magari kwa utapeli,mpaka leo Muhindi anaramba cha moto.

Kwa sasa anatoa magari machache ili kuepuka ghalama za mafuta na kulipa madereva,Rais anajua uwizi huu kuanzia kwa rafiki yake Marehemu Didas Masaburi,Mama Firts Lady and Co.

Anchoogopa na kufukua makaburi,lakini hakuna ufisadi mkubwa kama uliopo DART,tatizo ni kwamba ufisadi huu ulishupaliwa na UKAWA na kina KUBENEA,Mzee anaona akiukomalia,basi kuna watu watapata sifa kuwa wao ndio waanzilishi,na yeye kuwapa sifa watu wengine hataki kabisa
huyu mzee angeweza kufanya kazi na wapinzani angefanikisha mambo mengi sana, ila tatizo ndiyo hilo hataki huo ushirikiano matokeo yake mengine anabidi ayapotezee.
 
Ni tatizo la muda mfupi tu, systems down, litatengamaa
 
Back
Top Bottom