Dalili za kushindwa kwa ccm hizi hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dalili za kushindwa kwa ccm hizi hapa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by makoye2009, Oct 18, 2010.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Kwa mtu anayefuatilia kwa karibu kinyang'anyiro cha Uchaguzi wa mwaka huu ni wazi kwamba chama Twawala CCM(Chama cha Mafisadi au Majambazi) mwaka huu kimechezeshwa mchakamchaka kiasi kwamba kimeonekana kuporomoka na kukosa mvuto kwa Wa-tz walio wengi na hakina uhakika kama kitaingia Ikulu.

  Zifuatazo ni dalili ambazo ziko wazi kabisa na zina ashiria kuwa CCM imeshindwa kuhimili uwanja wa Kampeni labda tu kama watatumia mbinu chafu za na za kiujanjaujanja ili kiendelee kushika madaraka.

  1. CCM ukiwasikiliza kwa sasa hawazungumzi sera badala yake wameanza kueneza uzushi na uongo kuwa vyama vya upinzani VIKO TAYARI DAMU KUMWAGA DAMU ILI VIINGIE IKULU. Wakti huohuo CCM wenyewe wakiwachokoza kwa kuvuruga mikutano ya wapinzani. Mpaka sasa CCM wameshamwaga damu kule Musoma-Mara,Hai-Kilimanjaro kwa kuwakata na mapanga wafuasi wa CHADEMA.
  2. CCM kuwatumia REDET na SYNOVATE kutengeneza kura za maoni za uongo kuwahadaa Watanzania kuwa CCM na Kikwete bado wanakubalika. Ni mtu asiye makini tu ndo anaweza kukubaliana na maoni hayo kuwa watu 2600 nchi nzima kati ya watu milioni zaidi ya 40 wahojiwe halafu watoe mwelekeo wa Uchaguzi Mkuu. Ni uongo wa mchana kweupe.
  3. Kutumia vyombo vya Usalama kuwatisha Wapiga kura na Vyama vya Siasa kwa kuwalazimisha kukubali matokeo yatakapotangazwa na Tume bila ya kujali kama yatakukwa halali au haramu.
  4. Tambwe Hiza kusema kuwa CCM watashinda kwa asilimia 55 (55%) alipohijiwa na Shirika la Utanganzaji la Uingereza-BBC. Huku ni kuweweseka. Kinana anasema watashinda kwa asilimia 80%,Synovate 61%,REDET 71.2%,Tambwe Hiza 55%!!!!!Huu ni mkanganyiko tosha wa kudhihirisha kuwa CCM mwaka huu hawana chao,labda waibe kura!!!
  5. Kura za maoni za TCIB zinaelekea kutoa mwanga halisi wa matokeo yatakavyokuwa. Kwamba CHADEMA wanaongoza kwa upande wa vyama na Uraisi kwa asilimia 48% na 45% kwa pamoja. Mnyumbulisho wa TCIB umeonekana wa kisayansi zaidi na ulikwenda mbali zaidi kwa kuangalia mikoa 15, na katika kila mkoa jimbo moja, na katika kila jimbo kata mbili. Bado wakachanganua marika ya watu waliohojiwa kwa maana ya Wazee na Vijana ambayo ndio makundi makubwa 2 ya wapiga kura kitu ambacho kinadhihirisha hali halisi ilivyo kwenye majimbo.
  6. Kikwete kuendelea na kampeni mpaka siku ya mwisho kinyume na maelekezo ya Daktari na Chama chake kuwa alipashwa apumzike hasa baada ya kuanguka Jangwani kwa madai ya kuelemewa na Saumu kali akiwa kwenye mfungo. Hofu ya kushindwa imemfanya aendelee kutetea chama na kiti cha Urais bila kujali au kuangalia afya yake.
  7. Kikwete kuendelea kumtumia Mnajimu na Mpiga ramli Sheikh Yahya Hussein kuwatisha wapinzani kuwa anamlinda kwa kutumia Nguvu za Giza yaani Majini. Ati alipoanguka pale Jangwani ilikuwa ni dalili za ushindi!!!!!! Kikwete aliaanza kumtumia Sheikh Yahya tangu ulipoanza mchakato wa uteuzi wa Mgombea Urais ndani ya CCM yenyewe kwa kuwatisha wana-CCM wenyewe kuwa atakayepingana naye atakufa kifo cha ghafla.
  Ukijumuisha sababu hizo zote unaweza kuuona udhaifu wa Kikwete na chama chake chake cha CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2010. Kwamba mwaka huu wamekabwa koo kisawasawa kiasi kwamba hawajui wafanye nini na hivyo wamebakia kutapatapa kama mfa maji.

  Nawasihi CCM waache longolongo,wakae pembeni, wawape nafasi Watanzania kupitia Sanduku la Kura wachague Viongozi wanaowapenda wenyewe. Wakifanya hivo sisi Watanzania na wapenda demokrasia wote duniani tutawaheshimu.

  Lakini kama wataamua kwa makusudi kuibaka demokrasia(democracy raping) kwa kulazimisha matokeo yasiyokuwa matakwa ya Watanzania basi CCM watakuwa wanaendelea kujichimbia kaburi ambalo Uchaguzi wa 2015 watagaragazwa vibaya saaana.

  Nawasilisha.
   
Loading...