Dalili za kifo cha chama cha siasa au kikomo cha serikali

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
1. Viongozi hupingana hadharani
2. Watu hukata tamaa na kuwa tayari kufanya lolote
3. Wasomi na wafanyakazi hujipambanua wazi kukipinga chama au serikali
4. Tofauti kubwa ya kipato kati ya matajiri na maskini
5. Familia za wanasiasa hujipanga makusudi kurithishana uongozi
 
1. Viongozi hupingana hadharani
2. Watu hukata tamaa na kuwa tayari kufanya lolote
3. Wasomi na wafanyakazi hujipambanua wazi kukipinga chama au serikali
4. Tofauti kubwa ya kipato kati ya matajiri na maskini
5. Familia za wanasiasa hujipanga makusudi kurithishana uongozi
6.Wakuu wa serikali kuamua kulipana fedha za nchi kibinafsi kwa kuneemesha familia zao!
7.Nchi inapokuwa inaongozwa na RAIS-KIVULI ambaye kwa nje anaonekana ni Mbunge tu wa Jimbo la Igunga!:A S thumbs_down:
8.kIONGOZI MKUU anapomteua MAMA MKWE wake kuwa MBUNGE wakati anajua wazi alikuwa na makashfa ya aibu!
9.Mkuu wa nchi anapotoa ahadi za thamani ya trilioni 100, wakati anajua wazi bajeti yake inategemea ufadhili kwa 90%
10.NK.
 
10. Kiongozi anapokuwa kimya kwa kila jambo la msingi linalowahusu wananchi
11. Kiongozi anapokuwa njia panda na kushindwa kutoa maamuzi ya busara,
akiwa kwenye kikao kimoja wajumbe wakisema ndiyo nae anakuwa
kwenye ndiyo na anapoingia kwenye kikao kingine wakisema hapana nae
anakuwa hukohuko (Refer vikao vya cc na wabunge wa ccm kwenye issue ya
dowans
12. Nchi inapoongozwa na Kauli na Semi za familia wakati siyo nchi ya kifalme
 
hii topic imenikuna sana....ngoja na mi niongeze ya kwangu.

0.1 Pale wananchi wanapotaka katiba mpya wakati ya zamani hawajui hata kipengele cha kwanza kinasemaje.
0.2 Pale wananchi wanapokatiwa umeme, halafu hawajui wala hawaulizi kwa nini kuna mgao wa umeme kipindi hiki.
 
Back
Top Bottom