Dalili za chanjo ya ukimwi zaleta matumaini Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dalili za chanjo ya ukimwi zaleta matumaini Tanzania

Discussion in 'JF Doctor' started by Ngongo, Dec 16, 2008.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  UWEZEKANO wa kupatikana kwa chanjo dhidi ya ugonjwa hatari wa ukimwi unazidi kuongezeka baada ya matokeo ya awali ya chanjo ya majaribio kuthibitisha kuwa ni salama kutokana na watu waliohusika kwenye utafiti unaofanywa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (Muhas), kuonekana kuwa na ongezeko la vichocheo vya kinga dhidi ya ukimwi.


  Habari hiyo njema imekuja wakati dunia bado ikihaha kutafuta dawa ya kutibu ugonjwa huo unaodhoofisha kinga ya mwili ambao umekuwa ukichukua maisha ya watu wengi, hasa walio barani Afrika.


  Chanjo hiyo ya majaribio ilianza kutolewa Februari 20 mwaka jana, wakati mtu mmoja alipojitolea kupatiwa chanjo hiyo kwenye Kliniki ya Elimu ya Chanjo ya Kinga ya Maradhi ya Ukimwi (HIVIS).


  Akizungumza kwenye mahafali ya pili ya chuo hicho, makamu mkuu wa chuo, Prof Kisali Pallangyo alisema matokeo hayo yameleta msisimko kwa watafiti wa masuala ya chanjo ya VVU duniani kote.


  Hata hivyo, pamoja na matokeo hayo mazuri ya chanjo hiyo, Prof Pallangyo alisisitiza kuwa bado hakuna chanjo dhidi ya virusi vya ukimwi, hivyo ni lazima kila mtu azingatie njia zote sahihi za kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo.


  "Napenda kusisitiza kuwa bado hakuna chanjo dhidi ya virusi vya ukimwi na ni lazima kila mtu azingatie njia zote sahihi za kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi," alisema Prof Pallangyo.


  Mkurugenzi wa mipango wa HIVIS, Dk Muhammad Bakari alisema mafanikio ya chanjo hiyo katika hatua ya awali yamethibitishwa na kwamba majibu ya chanjo hiyo kutoka Sweden yanaonyesha kuwa dawa hiyo ya chanjo ina uwezo wa kutengeneza kinga imara zaidi kuliko matokeo ya chanjo zilizowahi kufanywa awali duniani.


  Dk Bakari alisema tatizo kubwa ni kasumba ambazo baadhi ya watu wanazo juu ya uhakika ambao watafiti wa chanjo hiyo wanao kuhusu nguvu ya chanjo hiyo.


  "Kuna watu wanaofikiria kuwa ili kutambua nguvu ya chanjo hii ni kuwapatia chanjo watu wenye virusi vya ukimwi. Hii ni njia chafu na isiyo na maadili na haiwezi kwa njia yoyote ile kutumika," alisema Dk Bakari.


  Alisema: "Chanjo hii ni kwa ajili ya kutambua usalama na matokeo ya chanjo dhidi ya virusi vya ukimwi kwa watu waliojitolea kupatiwa chanjo hiyo. Na itachukua majaribio mengi zaidi kabla ya kuanza kutumika ili tumika kutambua nguvu yake ya kukinga virusi vya ukimwi."


  Aliongeza kuwa muda huo ukifika watatumia kundi la wanaofungamana ikiwa ni hatua ya juu na ya hatari ya kupata uhakika wa chanjo hiyo. Alisema watatumia njia zote kuwakinga wahusika na virusi hivyo.


  Dk Bakari aliongeza kuwa kikubwa kinachowavunja moyo watafiti wa chanjo hiyo ni baadhi ya madaktari ambao kwa kukosa elimu ya kutosha juu ya chanjo, wanatoa taarifa za uongo kwa umma. Alisema hii ni kutokana na msukosuko na mkanganyiko walionao watu hao.


  Alitoa mfano, uvumi ulio mitaani kwamba chanjo hiyo hutumika kusambaza virusi vya ukimwi kwa watu waliojitolea, jambo ambalo alisema halina ukweli wowote na kutokana na uvumi huo wameongeza elimu kwa wanaojitolea juu ya hatua husika katika majaribio hayo.

  Source: Mwananchi
   
 2. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,903
  Trophy Points: 280
  Wasiwape watu matumaini yasiyokuwepo. Wafanye uchunguzi wa kina ili kuhakikisha wanachokisema kina ukweli badala ya kumpatia chanjo mtu mmoja tu na kutoa kauli inayoonyesha matumaini ya chanjo hiyo.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Chanjo ikipatikana mbona watu watakuwa kama kuku ktk yale majambozi.
  Ukimwi laiti nao ni discipline tosha,wengine ata Condomu hatuiamini as yaweza pasuka.
  Kisa cha kurisk matokeo yake mechi za kirafiki unazifuta zaidi ya kwenda na mwandani wako
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Dec 16, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Uharaka wa mawasiliano, watu kutokuwa na kazi au kutofuatlia kazia zao kwa dhati, kuwepo kwa vipodozi vya hali ya juu na mitindo ya mavazi ya kisasa ni sehemu ya vichochezi vya ngono. Siku hizi ni rahisi sana kukamilisha mipango hiyo kwa cellphone au compyuta bila kuonana. Vipodozi vingi na mitindo mingine ya mavazi ya akina dada huwachochea wanaume wasiokuwa na simile kuanza kuwafuatilia akina dada kuwashawishi kuhusu ngono. Kwa vile wote mwanamke na mwanamke wanakuwa na muda wa kufanya ngono wakati wowote, yaani hawana kazi, endapo mwanamke anayefuatiliwa naye ni maharage ya mbeya basi, kinachoweza kuwakinga waogope kufanya ngono hiyo ni UKIMWI. Kama woga wa ukimwi hautakuwapo, inawezekana usataarabu wa binadamu ukapungua sana katika jamii zetu ambazo watu wengi hawana kazi za kuwakeep busy.
   
 6. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu kichuguu

  Hesmima mbele..,

  Kama nimekupata vizuri ni kuwa unachukulia kuweko kwa IKIMWI ni positive force ya Kuijenga jamii na kuirudisha kunakotakiwa kibinadamu...tuseme na kimaadili.

  So unaona kuwa hakuna haja ya kudevelop chanjo ya ukimwi?

  Au nilivyokueleewa ni kuwa kuufuta UKIMWI bila kufuta wrong human traits, characters etc...ni kama kazi bure kwani tatizo litakalo kuwa limefutwa litajitokeza kwa namna nyingine?
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Dec 16, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Unfortunately nilijua kuwa maneno yangu yataeleweka kuashiria kuwa kuwepo kwa ukimwi ni jambo jema, la hasha. Nadhani ningemalizia kuwa tatizo ninaloona ni uwezekano wa kuongezeka kuzaliwa kwa watoto ambao baba zao hawajulikani. Nilichokuwa nasema ni kuwa ukimwi umesaidia kuwafanya watu wawe na discipline fulani ya kufanya ngono katika mtindo unaouzuia mimba hasa ukizingatia mazingira ya maisha ya sasa jinsi ilivyo rahisi kufanya ngono.

  Hata hivyo kuna mtu hapa pembeni mwangu ananiambia kuwa huenda ukimwi nao umechangia sana kasi ya watu kufanya ngono wakijua kuwa watatumia mipira na hivyo hakuna madhara yoyote. Kama dawa itapatikana, na hivyo kufanya wanaume wasipende kutumia mipira, basi wasichana wataanza kuwa makini ili wasipate mimba na hivyo kupunguza kasi ya ngono.
   
Loading...