CCM ilivyo sasa imepungukiwa na upeo wa kuona mambo na kudhani kuwa wao ndio wenye hati miliki ya kuongoza nchi hii na Rais lazima atoke ndani ya CCM ndio maana badala ya kutatua kero za wananchi wao kwa sasa wanaangalia nani rais ndani ya CCM 2015 ikiwa juzi tuu tumetoka kwenye uchaguzi na wao ndio wanaongoza serikali, hii ni dharau kubwa kwa Watanzania na inaonyesha jinsi ambavyo hawako tayari kuachia madaraka kwa amani tena hawana tena uwezo wa kusoma alama za nyakati. Hata ule ushauri wa bure wa Majidi Mjengwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo lililopita hawakuona.Nasisitiza tena CCM isiendelelee kujidanganya kuwa inaweza kuendelea kuwadanganya watanzania kwa kuendelea kuwaibia kura. Kama CCM inadhamira ya kweli ya kulinda amani ya Tanzania lazima kuwe na tume huru chini ya Katiba mpaya 2015 na haki lazima itendeke na ionekane ikitendeka vinginevyo mnamuandalia Ocampo kazi na ofisi yake huenda ikawa Arusha 2016.