Dalili za CCM kupatia OCAMPO kazi 2015 zinajionyesha wazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dalili za CCM kupatia OCAMPO kazi 2015 zinajionyesha wazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Oct 13, 2011.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  CCM ilivyo sasa imepungukiwa na upeo wa kuona mambo na kudhani kuwa wao ndio wenye hati miliki ya kuongoza nchi hii na Rais lazima atoke ndani ya CCM ndio maana badala ya kutatua kero za wananchi wao kwa sasa wanaangalia nani rais ndani ya CCM 2015 ikiwa juzi tuu tumetoka kwenye uchaguzi na wao ndio wanaongoza serikali, hii ni dharau kubwa kwa Watanzania na inaonyesha jinsi ambavyo hawako tayari kuachia madaraka kwa amani tena hawana tena uwezo wa kusoma alama za nyakati. Hata ule ushauri wa bure wa Majidi Mjengwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo lililopita hawakuona.Nasisitiza tena CCM isiendelelee kujidanganya kuwa inaweza kuendelea kuwadanganya watanzania kwa kuendelea kuwaibia kura. Kama CCM inadhamira ya kweli ya kulinda amani ya Tanzania lazima kuwe na tume huru chini ya Katiba mpaya 2015 na haki lazima itendeke na ionekane ikitendeka vinginevyo mnamuandalia Ocampo kazi na ofisi yake huenda ikawa Arusha 2016.
   
 2. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Bahati mbaya ndugu zangu na wengineo wooooote waliopo vijijini hawajaelewa...................
   
 3. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nadhani ni ndoto nzuri.
   
 4. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ocampo atapata kazi bila shaka!! Watu wa vijijini wataelewa tu, somo linaingia kupitia wanaelewa wala si ndoto ni kweli kabisa chama chetu chamapinduzi chajenga chuki siku hizi siyo kujenga nchi tena.
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,297
  Trophy Points: 280
  hao wa igunga waliopigia CDM ni wa mjini? naongelea watu 23,000 walioikataa CCM igunga.
   
Loading...