Dalili Za Asiyekupenda Kwa Dhati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dalili Za Asiyekupenda Kwa Dhati

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Yona F. Maro, Jul 23, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jul 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  2 : Anapata kigugumizi kukutambulisha kwa rafiki zake na ndugu na inapotokea amebanwa hafikishi ujumbe kwa kiwango timilifu.

  3 : Haoneshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleao, kwake ni kufuja mali na anapokosa kupewa pesa ni mwepesi kulalamika na wakati mwingine kununa kabisa.

  4 : Anaahilisha mara kwa mara kukutana na wewe tena bila kukueleza sababu za msingi Au kukutungia uongo wa dhahili na kuusisitiza bila kuona aibu.

  5 : Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanaume amtakaye sifa zake zinakuwa hayalingani na wewe. Anaweza kukuambia napenda kuishi na mwanaume mwenye gari au mwenye mwili mkubwa, sifa ambazo wewe huna!

  6 : Hacheki kwa furaha hata kama ukimchekesha haoneshi furaha ya moyoni. Tena mara nyingine anakuwa mkimya na mshiwishi mkubwa wa kuachana kutoka kwenye matembezi yenu ya jioni. “Aaah, mi nimechoka narudi nyumbani”

  7 : Anajaribu kukuunganisha na wanawake wengine na haoni vibaya anaposikia unamfukuzia mwingine badala yake anakutia moyo wa kuendelea na usaliti wako. Hana wivu kabisa.

  8 : Hajuti anapokukosea, mwepesi wa kujitenga, kutokuzungumza nawe na mwingi wa kukusukumia makosa hata kama yeye ndiye aliyekukosea.

  9 : Msambazaji wa habari za udhaifu wako na mtu asiyekusifia mbele za wenzake. Si balozi mwema kwa familia yake, haishi kukuponda mbele ya wazazi na ndugu zake.

  10 : Mwepesi wa kupokea na si wa kutoa mmiliki wa mali zako na mkumbatiaji wa mali zake pia. Msiri wa mipango yake na mtu anayependa kujua zaidi ya kwako kuliko wewe kujua yake.

  11: Hathamini uwepo wako na anakuchukulia kama mtu wa akiba. Hakumis unapokuwa haupo, hahisi upweke wala hakukumbuki unapokuwa mbali naye.

  12 : Hakutii moyo unaposhindwa na mara nyingine hauzuniki nawe unapokuwa una shida,. Hachukui huzuni yako kama yake, hakufariji na hakusaidii kutatua kilichokwama.

  13 : Mhamasishaji wa uasi hasa wa watoto na ndugu, anayeweza kuchochea hisia za jamii ikuone mbaya, ukudharau na wakati mwingine ikutenge. Mwenezaji wa sifa zako mbaya.

  14 : Hakupi kipaumbele katika maamuzi, anajiona yeye ndiye wa kwanza na wewe ni mtu wa kufuata hata unapopinga hasitishi dhamira yake ya kutenda.

  15 : Humsisimui katika mambo ya faragha, anakuchukulia kama ndugu yake.

  16 : Hakuhudumii tendo la ndoa mpaka siku amependa mwenyewe. Ni mwingi wa sababu za kuchoka kusingizia ugonjwa na mwenye kuhisi kero ya kucheza nawe mchezo wa kikubwa.

  17 : Hazungumzii maendeleo yenu, mwepesi wa kushawishi ilivyopatikana viuzwe ili atimize hitaji lake. “Niuze simu yangu niende kuwaona wazazi, maana kuna sherehe ya motto huko!”

  18 : Hataki kuambiwa ukweli na anapotokea akaambiwa anajitetea kwa kumtaja mwanaume mwingine. “Mbona Shabani (si jina halisi) anamfanyia hili, hamfanyii hivi mkewe”

  19 : Hasamehe na kusahau. Kosa la mwaka juzi analijengea hoja.

  20 : Mwepesi wa kutoa kauli za kutengana na asiyeogopa kuachwa. “Kama vipi kila mtu akae kivyake maana naona unaniboa tu, unadhani nitashindwa kuishi bila wewe”

  BRAZAK
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...penda akupendae, huu ni unyanyasaji wa kijinsia na usongo wa mawazo, no wonder wenye roho ndogo (kama lile kabila la kule kwenye mlima wa uluguru) wao huamua kujinyonga!
  View attachment 4183
   
 3. M

  Msindima JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Big up Shy! Article iko vizuri na imetulia.
  kwa kweli hayo ni ya kweli kabisa,Cha muhimu tuonapo dalili hizo its better ukaachana na hiyo relationship maana at the end of the day utakuja kujuta na utakua na maumivu makali na pia utakua umepoteza muda.
  So we have to take care.
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...alivyoorodhesha Shy, na ukichukulia kipengele kimoja kimoja utaona arrghh, si unaachana naye tu, Tatizo ni pale Mtu wako hakuwa hivyo awali,...baada ya mapenzi moto moto mpaka ndio anakuletea hiyo package ya nguvu!

  ...kutamka rahisi Msindima, lakini utekelezaji wake mnh! ushawahi kupenda huoni wala husikii?.... ni pale unapoona labda atabadilika, labda hujajitolea vya kutosha, labda umpe muda zaidi... Mapenzi ni Imani, ngumu sana kumuondoa mtu katika imani...

  Unless ulikuwa una beep mapenzi!
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Apr 8, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hasa wengine mbona hizo sifa wamedevelop wakati tayari weshaoa/olewa ina maana hakupendi tena au hakuwahi kukupenda?
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  NIMEKUBALI MKUU!
  umzikurupua wapi?
   
 7. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kwanza mbona Na.1 hamna?
  Pili, ukishapenda hayo yote huyaoni na hata ukiyaona uta-justify au kujiridhisha kwanini mpenzi wako anafanya hivyo. Utakuwa na sababu nzuri tu ambazo mwingine hawezi kuelewa. Matokeo yake we unawashangaa wanaokushangaa.
  "Mtu chake apendacho........................."
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ..that's what am talking about!...

  ghafla bin vuuu mara hataki kuongea na mama mkwe na wifi zake, hataki marafiki zako, hataki maendeleo yako, hataki..hataki..hatakiii tu!
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Amezikurupua?
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Definately!, na hapo kwenye ku justify anayokutendea ndipo unapoanza kuonekana zezeta/umekaliwa kichwani!

  ...there is no justification kwa yote hayo, rejea yote na hitimisho lake kisha justify na hili...

   
 11. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Je hii inalenga pande ipi hasa mwanamke/mwanamme au ni kwa wote.
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Apr 8, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hii bana wakati mwingine huwa haimaanishi kuwa hakupendi kuna mwingine anasema hivi kutokana na kero na uchungu anaoupata kutoka kwa mpenziwe pamoja na kuwa anampenda sana. Mimi nilishawahi kuwa naitumia hii (sio kutumia tu bali nilikuwa namaanisha) maana vituko alivyokuwa ananifanyia nilikuwa naona ni afadhali kila mtu ashike ustaarabu wake kwani nilikuwa naona kama nampa kero na kumlazimisha kuishi nami wakati hanipendi angekuwa ananipenda kamwe asingekuwa ananifanyia vitu vinavyuoniumiza mara kwa mara na ukimwuliza anakuwa mbogo na hata samahani haombi!. Mimi ninampenda mpaka kesho ingawa ndo ilikuwa hivyo tena.

  So mtu kukwambia kila mara ni afadhali tuachane doesnt necessarily mean hakupendi bali kero na maumivu unayompa anaona afadhali tu mpart
   
 13. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kuna watu wengine wakigundua kwamba unawapenda sana wanakuwa na maringo na kudeka kusiko kuwa na mpango! Kauli hii ni nzuri na ya ukweli ili ajue kwamba pamoja na kwamba unampenda lakini hilo kamwe halimaanishi huwezi kuishi bila yeye!
   
 14. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #14
  Apr 8, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...nakubaliana nanyi, ila, " ...it is not what you say, it is how you say it that's what makes a big difference!"
   
 15. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Hiyo point imenigusa maana niliwahi kuambiwa maneno kama hayo ya kuonyesha kutojali kumpoteza mtu kimapenzi yaani 'tusipotezeane muda,take your time and I will take mine'. Halafu ulikuwa ni ugomvi mdogo sana ila hayo maneno makali na yalinichanganya sana,inawezekana ni mahasira wakati wa majibizano au mtu anamaanisha kiaina!? Ubaya sisahau na ninaandika kwenye diary matukio muhimu yote..
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Belinda tabia mbaya hiyo ya kuorodhesha mabaya, achana nayo haki ya Mungu nakwambia! ...Itakuja kukuletea matatizo sana maishani mwako kwani kila kosa likitokea utashawishika kufungua Diary kuangalia referrence!

  Andika yale mazuri tu, mabaya yaache yapite...
   
 17. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #17
  Apr 9, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Nadhani hilo ni kati ya tatizo nililonalo,ni mtu wa ku-note down vitu fulani yaani inaweza ikapita hata mwezi unamwambia mtu siku fulani uliniambia maneno haya..anashangaa! Siyo siri inanicost sana,itabidi nibaki kuandika good moments only starting mwezi huu..
  Thanks for ushauri Mbu, tatizo langu kubwa nina moyo mgumu linapokuja suala la mahusiano na kusamehe tena najitahidi kiaina siku hizi!
  Cheers!..
   
 18. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #18
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ni kweli tena pole sana, wewe ni dereva wa mawazo yako, ...yaendeshe mawazo yako kwenye kuepuka mambo yatayokuja kukuumiza baadae, mfano hilo la kuweka kumbukumbu mbaya.

  Hakika usipoyaandika, utayasahau,..kwani kila jema/zuri baada ya tukio la kuhuzunisha taratiibu linafuta machungu ya nyuma, ...Lakini ukiweka kumbukumbu ya maandishi, siku ukiwa bored ukapitia hiyo Diary utajikuta unajiharibia siku buree.

  Jinasue kwenye hako katabia...Goodluck!
   
 19. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #19
  Apr 9, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Thank you Mbu!

  Let me work on it, ushauri wako nimeupenda!

  Be Blessed..
   
 20. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #20
  Apr 9, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Jamani hizi dalili mbona zipo upande wa kike tu? Yaani wanaume wote mpo right au nyie huwa hamutendi hivi vitu?
   
Loading...