Dalili Mbaya Kiuchumi, Hata Maonyesho ya Sabasaba yamedoda!

Mliozoea ela ya wizi,ufisadi, semina,safari ,warsha,makongamano nk.mtapata shida sana awamu hii.
Sisi tuliozoea za halali tumekwenda sabasaba kama kawaida kwa sababu tunaishi kwa bajeti na kupangilia kile tunachokipata cha halali.
 
To be sincere, mwaka huu 77 hali ngumu sana... wananchi wachache sana wanaokwenda.. hata magari ktk parking nje ya 77 grounds machache..!! Naona uchumi wa wananchi umeyumba kidogo..!! Hali si nzuri, lazima niseme ukweli, hali ni tofauti na miaka ya nyuma.. labda tuvumiliane uchumi utakuwa mzuri MUNGU AKIPENDA, maana Rais wetu Magufuli anajitahidi sana, pia anamwomba Mungu sana, tuvumiliane tu..
Kweli mkuu tuvumilie tu Mungu akipenda tutatoboa tu au sio mwana....?
 
Hadi ikiwafikia wao hakika watajua kuwa wananchi wameumia sana
 
Hali mbaya kote,wazee wa payrol ndio wenye nafuu,
Wajiriamali tunaisoma namba vilivyo
 
Kweli mkuu tuvumilie tu Mungu akipenda tutatoboa tu au sio mwana....?

Tatizo umaskini wa NJAA ndio mbaya kuliko wote..!! Mh. Rais inabidi awe makini uchumi uweze kulisha watu walau mara 3 kwa siku..!!
Unajua huwezi ku negotiate na mtu mwenye njaa..!! Atleast Mh. Rais ampambane na serikali yake uchumi uonekane kwa wananchi.. maana hali sio nzuri sasa hv ki ukweli
 
Apewe muda Magu... kaanza kwa kasi kwenda kila upande. Kukosea na kupatia!

Atahukumiwa kwa spidi ya kusahihisha makosa yake kabla hayajaumiza sisi hohehahe sana
 
Nina uzoefu sana na haya maonyesho mkuu , tarehe 7 ni siku ya kuhitimisha shughuli tu , manunuzi , mauzo pamoja na matangazo yote yanafanyika siku kama hizi , ngoja nikuulize kitu , hivi safari hii umesikia tena hata yale matangazo ya NUNUA MOJA PATA TATU BURE ? si kizota wala heineken wala wale wala mdudu kule mole bar , kote kimyaaaaa !!!!
Hahaha......mkuu mbona unatukatisha tamaa kiasi hiki??Me ndio nilikuwa najipanga kuleta kwenye hayo mabanda kuku zangu za kilo 15 kwa 20 kwaajili ya kutanua biashara zangu kumbe mambo sio??
 
Kiuchumi imekaa vizuri mbona, ulikuwa na gari nauli ilikuwa bei kubwa, kwa sababu tank ilikuwa imetoboka hivyo unapofanya marekebisho unashusha bei sasa kwa makondacta wataanza kushaanga kukusanya kidogo kumbe hapo hapo matumizi madogo maana shida ya gari imerekebiswa,watu walizoea kutumia pesa kwa fujo sababu ya madili mengi sasa hakuna,
 
UCHUMI ULIOKUWA KWA WATU KIPINDI CHA JK HAUPO TENA; WATU TUNAHANGAIKIA TUMBO TU KWA SASA, SITE ZA UJENZI ZIMESIMAMA HATUJUI ZITAANZA LINI TENA
Basi mnategemea pesa za wizi acha mzifunge hizo site...
 
Miaka ya nyuma maonyesho ya Sabasaba Kilwa Road yalikuwa yanashamiri na kuleta picha Fulani hivi kuhusu uchumi wa mtu mmoja mmoja na makampuni yanayoshiriki.
Lakini mwaka huu kwa karibia ya wiki sasa yamedorora na mbanda mengi hayajafungukiwa na hata wananchi hawana furaha ya kufuatili kwa nini?
Kuna dalili mbaya sana ya mwenendo wa nchi kiuchumi wa watu wake, kila mtu kapigika au tuseme wengi wamepigika na hakuna jitihada ya wazi kulikabili hilo.
Mwaka huu kuna viingilio hivyo wingi hauwezi kulingana na bure. Uwanja wa Taifa haujawahi kujaa kwa kiingilio hata wacheze Brazil. Angalia mechi ya bure kilichotokea uwanja ulitapika. Hivyo maonesho ya mwaka huu na ya zamani hayafai kulinganishwa kuhusu idadi labda akili ziwe hazikutoshi
 
Mwaka huu watu hawana pesa mana unaweza kupiga stori kwenye banda lako mpaka ukajisahau ka upo sabasaba kuonyesha biashara yako mana raia ni wa kuhesabu
Hao basibwalikuwa wanategemea pesa za wizi!
 
Miaka ya nyuma maonyesho ya Sabasaba Kilwa Road yalikuwa yanashamiri na kuleta picha Fulani hivi kuhusu uchumi wa mtu mmoja mmoja na makampuni yanayoshiriki.
Lakini mwaka huu kwa karibia ya wiki sasa yamedorora na mbanda mengi hayajafungukiwa na hata wananchi hawana furaha ya kufuatili kwa nini?
Kuna dalili mbaya sana ya mwenendo wa nchi kiuchumi wa watu wake, kila mtu kapigika au tuseme wengi wamepigika na hakuna jitihada ya wazi kulikabili hilo.

This country is going to collapse, we need God intervention.
 
Back
Top Bottom