Nina banda la kampuni yangu mle ndani , pamoja na kuweka vifaa vya kisasa na wahudumu bomba lakini naomba nikwambie kitu , mwaka huu ninaziona dalili za kupata hasara kubwa sana na Kiukweli hali ya uchumi kama itakuwa hivi kwa miaka miwili ijayo MAONYESHO YA SABASABA YATAFUNGWA MOJA KWA MOJA , maana hakuna tunachokifanya kule , ni bora kufanya matangazo ya biashara kwa njia nyingine .Miaka ya nyuma maonyesho ya Sabasaba Kilwa Road yalikuwa yanashamiri na kuleta picha Fulani hivi kuhusu uchumi wa mtu mmoja mmoja na makampuni yanayoshiriki.
Lakini mwaka huu kwa karibia ya wiki sasa yamedorora na mbanda mengi hayajafungukiwa na hata wananchi hawana furaha ya kufuatili kwa nini?
Kuna dalili mbaya sana ya mwenendo wa nchi kiuchumi wa watu wake, kila mtu kapigika au tuseme wengi wamepigika na hakuna jitihada ya wazi kulikabili hilo.
Unauhakika waliokuwa wanajaa Kule walikuwa watu wa dili? Mbona wanafunzi, wamama wa nyumbani na wananchi wa kawaida wanaoenda nunua bidhaa ndio walikuwa wengi? Hivi hao nao ni wa dili?Sasa hivi wenye pesa ni wale waliyoipata kihalali kwa jasho ambao huwa wabahili kuitumia hovyo hovyo.
Waliokuwa wanajazana huko sabasaba wengi wao wlikuwa ni wale waliopata mapesa kwa njia za madili haramu yakiwamo ya kuuza unga. Hawa mwaka huu wanaisoma namba.
Nina uzoefu sana na haya maonyesho mkuu , tarehe 7 ni siku ya kuhitimisha shughuli tu , manunuzi , mauzo pamoja na matangazo yote yanafanyika siku kama hizi , ngoja nikuulize kitu , hivi safari hii umesikia tena hata yale matangazo ya NUNUA MOJA PATA TATU BURE ? si kizota wala heineken wala wale wala mdudu kule mole bar , kote kimyaaaaa !!!!Tusubiri tu mkuu mbona trh 7 July haijafika!
Uongo utakusaidia nini ?Maonyesho kawaida sawa na siku zote.Watu wapo wengi tu.Ukute mleta mada hakuwahi kwenda kwenye hayo maonyesha na pengine hayupo hata Dar.Mtajikuta mnakuwa wachawi mwisho wa siku.
Kama ni uzushi basi magazeti ya Leo nayo yamezusha kwa kiwango kikubwa.Maonyesho kawaida sawa na siku zote.Watu wapo wengi tu.Ukute mleta mada hakuwahi kwenda kwenye hayo maonyesha na pengine hayupo hata Dar.Mtajikuta mnakuwa wachawi mwisho wa siku.
Hebu watujibu hilo maana waliponda sana uchumi wa kipindi cha rais mstafu sasa hivi wanajifanya wanakumbuka uchumi we kipindi kileHivi nyinyi BAVICHA mnachosimamia sasa ni kipi? Maana mnatuchanganya sasa wananchi.