Dalili kwamba unajipendekeza kupita kiasi katika uhusiano….!

Mapenzi = Utegemezi= Kujipendekeza.

Huwezi kutenganisha haya, utataka kufanya biashara badala ya mapenzi.

Suala si kukataa kujipendekeza au kuwa tegemezi.

Suala ni kutafuta mtu anayekufaa kiasi kwamba hata ukijipendekeza kwake na kuwa tegemezi kwake nyote mtafurahi.

mkuu, hebu angalia hiyo dalili ya kwanza. Kuna relationships ambazo mmoja haruhusiwi kudadisi wala kulalamikia lolote. Hata uki-raise hoja, unaishia wewe kuomba msamaha na still it aint good enough. Katika mahusiano ni muhimu kila mmoja akawa na uhuru wa kukubaLiana kutofautiana. Na bila kusahau flexibility kwenye baadhi ya misimamo. Ukiingia kwenye uhusiano ambao wewe ndio unahitaji ku-give up everything ili ufit kwake, hilo ni chaka la miiba. Utegemezi kiasi, mapenzi kwa tele na hapo kujipendekeza hakuhitajiki.
 
hapa mtambuzi kala hasara! Lol. Mi nataka nikuuzi king'asti unipe talaka.

Mwenzio ndo anajua faida hii. Hata dingi aki-RIP leo anajua we are strong enough kumuangalia maza. Tena hata sijui Asprin ajilete kumrithi mjane, tunampiga interview kama ya UN hq atablow mwenyewe.
mpaka uniudhi, kwanza unatakiwa uhakikishe umejipenyeza moyoni mwangu na hata nikikohoa mara moja hutoki. Ila ukinifanya nijiskie najipendekeza kwako, ntakohoa mara 3 na kupiga chafya 2 na utaelea kwenye spit on ur way out.

Haya, kazi kwako, nakufungulia moyo:A S-heart-2:
 
Najua kuna wadau humu watashikwa na kizunguzungu kwa kutoelewa nilichomaanisha
 
mkuu, hebu angalia hiyo dalili ya kwanza. Kuna relationships ambazo mmoja haruhusiwi kudadisi wala kulalamikia lolote. Hata uki-raise hoja, unaishia wewe kuomba msamaha na still it aint good enough. Katika mahusiano ni muhimu kila mmoja akawa na uhuru wa kukubaLiana kutofautiana. Na bila kusahau flexibility kwenye baadhi ya misimamo. Ukiingia kwenye uhusiano ambao wewe ndio unahitaji ku-give up everything ili ufit kwake, hilo ni chaka la miiba. Utegemezi kiasi, mapenzi kwa tele na hapo kujipendekeza hakuhitajiki.

Hujanipata,

Sitetei mzingo wa moyo wala manyanyaso kwa kutumia mgongo wa "mapenzi". La hasha.

Ninachosema ni kwamba, mapenzi si mchele useme utayaweka kwenye mizani na kupima uwiano uwe sawa. Hata hiyo kilo ya mchele inakadiriwa kwa decimal places.

Nasema kwamba, unapotafuta mpenzi, ni bora utafute kwa kujua kwamba mapenzi hayana milinganyo, na kwamba kuna sehemu itabidi ufanye atakavyo mpenzi wako (hata kama na yeye itabidi afanye hivyo hili halisawazishi, kwani hakuna vipimo vya kuhakikisha kadiri inanukuliwa).

Kwa hiyo, ukiingia kwenye mapenzi, ni bora kuingia kwa fikra ya kwamba, ukikutana na mpenzi wako ana allergy ya kula shrimp wakati wewe ndo unapenda sana shrimp, uweze kusema mie nitaacha kula shrimp kwa sababu ya mpenzi wangu, naogopa ku trigger allergy yake.

Ndiyo maana nikasema, "kujipendekeza" na "kutegemea" katika mapenzi hakuepukiki.

Cha kufanya ni kuhakikisha kwamba unayemchagua kujipendekeza kwake, na kumtegemea awe worth the privilege.

Katika dhana nzima ya "kutafuta mtu anayekufaa" kama una akili utatafuta mtu ambaye hata ukijipendekeza kwake, hata abuse privilege hiyo, actually mtakuwa mnashindana kwa kila mtu kutaka kujipendekeza zaidi kwa mwenzake.

Honey umeninunulia zawadi, na mimi nilikuchukulia mkufu huu nilifikiri utaupenda.

Si ndo mapenzi yenyewe hayo?

Kwa kujipendekeza simaanishi janaume linakupiga kila siku mwanamke uwe unang'ang'ania tu, inawezekana ni mapenzi pia, lakini mie sifagilii hayo.
 
Mapenzi = Utegemezi= Kujipendekeza.

Huwezi kutenganisha haya, utataka kufanya biashara badala ya mapenzi.

Suala si kukataa kujipendekeza au kuwa tegemezi.
Suala ni kutafuta mtu anayekufaa kiasi kwamba hata ukijipendekeza kwake na kuwa tegemezi kwake nyote mtafurahi.
Nakubaliana na wewe mkuu 100%, Mtambuzi unasemaje kuhusu hoja hii muhimu?
 
Nakuambia acha kunywa chang'aa ya kayole hunielewi. Njoo buruburu kuna kinywaji swaafi!
King'asti umejuaje ndugu yangu??
Niko hapa external tunagonga chibuku..any wayz ngoja nicheki na dadi yako Mtambuzi aniambie kama supu ya ulimi imeisha kule kwenye pub yake mpya tabata ubaya ubaya..by the way si upo kaunta??
 
Last edited by a moderator:
Hapa hoja ya msingi imelalia hapo kwenye "kupita kiasi" kwa sababu mapenzi sidhani kama yanaweza kutenganishwa na kujipendekeza.

Kwangu hii "kupita kiasi" naitafsiri kama ni kujipendekeza kwa upande mmoja tu. Na hapo sidhani kama tunaweza kusema kuna mapenzi baina yao, labda tuseme mmoja anampenda mwenziwe.
 
Mwenzio ndo anajua faida hii. Hata dingi aki-RIP leo anajua we are strong enough kumuangalia maza. Tena hata sijui Asprin ajilete kumrithi mjane, tunampiga interview kama ya UN hq atablow mwenyewe.
mpaka uniudhi, kwanza unatakiwa uhakikishe umejipenyeza moyoni mwangu na hata nikikohoa mara moja hutoki. Ila ukinifanya nijiskie najipendekeza kwako, ntakohoa mara 3 na kupiga chafya 2 na utaelea kwenye spit on ur way out.

Haya, kazi kwako, nakufungulia moyo:A S-heart-2:

machariti mepesi hivyo, orait, kazi ya kujipendekeza nitaianza soon. Let me talk to Paw kwanza aniambie alipenya penya vipi kwenye hako kamoyo kako.
 
Last edited by a moderator:
Hujanipata,

Sitetei mzingo wa moyo wala manyanyaso kwa kutumia mgongo wa "mapenzi". La hasha.

Ninachosema ni kwamba, mapenzi si mchele useme utayaweka kwenye mizani na kupima uwiano uwe sawa. Hata hiyo kilo ya mchele inakadiriwa kwa decimal places.

Nasema kwamba, unapotafuta mpenzi, ni bora utafute kwa kujua kwamba mapenzi hayana milinganyo, na kwamba kuna sehemu itabidi ufanye atakavyo mpenzi wako (hata kama na yeye itabidi afanye hivyo hili halisawazishi, kwani hakuna vipimo vya kuhakikisha kadiri inanukuliwa).

Kwa hiyo, ukiingia kwenye mapenzi, ni bora kuingia kwa fikra ya kwamba, ukikutana na mpenzi wako ana allergy ya kula shrimp wakati wewe ndo unapenda sana shrimp, uweze kusema mie nitaacha kula shrimp kwa sababu ya mpenzi wangu, naogopa ku trigger allergy yake.

Ndiyo maana nikasema, "kujipendekeza" na "kutegemea" katika mapenzi hakuepukiki.

Cha kufanya ni kuhakikisha kwamba unayemchagua kujipendekeza kwake, na kumtegemea awe worth the privilege.

Katika dhana nzima ya "kutafuta mtu anayekufaa" kama una akili utatafuta mtu ambaye hata ukijipendekeza kwake, hata abuse privilege hiyo, actually mtakuwa mnashindana kwa kila mtu kutaka kujipendekeza zaidi kwa mwenzake.

Honey umeninunulia zawadi, na mimi nilikuchukulia mkufu huu nilifikiri utaupenda.

Si ndo mapenzi yenyewe hayo?

Kwa kujipendekeza simaanishi janaume linakupiga kila siku mwanamke uwe unang'ang'ania tu, inawezekana ni mapenzi pia, lakini mie sifagilii hayo.

Nadhani tutofautishe 'kumpendeza' na kujipendekeza. Kujipendekeza nadhani ni wakati hakuna hiari ama kuna msukumo wa ziada. Mimi naamini mpenzi akiwa anafurahia kupendwa, haihitaji matisho wala shuruti kumfanyia jambo. Actually, when all is over huwa najiuliza hizi nguvu za kufanya yote haya nilizitoa wapi!
 
machariti mepesi hivyo, orait, kazi ya kujipendekeza nitaianza soon. Let me talk to Paw kwanza aniambie alipenya penya vipi kwenye hako kamoyo kako.

Hahaha, Paw usimtegemee akupe siri ya urembo. Hivi unategemea Bhakressa akupe formulae ya azam cola? Kuwa m'bunifu, afu hakikisha huanzi kuniudhi mpaka upenye hadi central core eeh:whip:
 
nishaona nakaribia karibia, nipo kwenye magma nafikiri.
 
Nadhani tutofautishe 'kumpendeza' na kujipendekeza. Kujipendekeza nadhani ni wakati hakuna hiari ama kuna msukumo wa ziada. Mimi naamini mpenzi akiwa anafurahia kupendwa, haihitaji matisho wala shuruti kumfanyia jambo. Actually, when all is over huwa najiuliza hizi nguvu za kufanya yote haya nilizitoa wapi!

Kumpendeza ndo kujipendekeza huko, tatizo kujipendekeza kumechukua a negative connotation.

Mie napenda mpenzi wangu ajipendekeze kwangu, na mie najipendekeza kwake vile vile.

Hakuna aibu kujipendekeza kwa unayempenda, ndo mapenzi hayo.
 
mkuu, hebu angalia hiyo dalili ya kwanza. Kuna relationships ambazo mmoja haruhusiwi kudadisi wala kulalamikia lolote. Hata uki-raise hoja, unaishia wewe kuomba msamaha na still it aint good enough. Katika mahusiano ni muhimu kila mmoja akawa na uhuru wa kukubaLiana kutofautiana. Na bila kusahau flexibility kwenye baadhi ya misimamo. Ukiingia kwenye uhusiano ambao wewe ndio unahitaji ku-give up everything ili ufit kwake, hilo ni chaka la miiba. Utegemezi kiasi, mapenzi kwa tele na hapo kujipendekeza hakuhitajiki.

Mwanangu si hivyo tu, nilianza mada hii na angalizo hili:
Awali kabisa nilisema hivi:
Ni kweli kwamba tunatakiwa kujitolea ili kujenga uhusiano imara na wenzi wetu. Tunaambiwa kwamba ili mapenzi yawe imara na yadumu inatupasa tusichoke kutoa, lakini kutoa huku kusiwe kwa upande mmoja, yaani kila mmoja ajitoe kwa mwenzie na hapo ndipo kila mmoja atakapofurahia uhusiano huo. Lakini pale ambapo upande mmoja ndio unajitolea kupita kiasi (hii huwa inawatokea wanawake) basi ujue huko sio kujitolea tena bali kuna utegemezi mkubwa sana wa kihisia (codependency) ambao niliwahi kuuzungumzia wakati fulani.
\

lakini nashangaa wadau humu wanashikwa na kigugumizi... hebu tujiulize hivi:

Kukwepa kujaribu kutofautiana…… Huu sio utegemezi kweli, yaani mtu aje akudanganye tu, na wewe ukubaliane naye kisa unaogopa kutofautiana naye.... kisa unalinda uhusiano wenu usiingie dosari, lakini wengi hawajui kwamba wapenzi wanaotofautiana na kuweka wazi misimamo yao wanajenga kuheshimiana na kila mmoja anaheshimu msimamo wa mwenzake hata kama hakubaliani naye

Mnagombana kila siku…. Kuna wapenzi au wanandoa ambao wanaishi kama paka na panya, kila siku hawaishi kugombana, kila mmoja anamvizia mwenzake ili kutafuta dosari, na mara nyingi wapenzi wanaoishi kwa mtindo huu, wanakuwa ni watu wa visasi. Kuna haja gani ya kuishi katika uhusano wa aina hii, sasa huu kama si utegemezi ni kitu gani... mtu anayeng'ang'ania uhusiano wa aina hii ni kwamba anaogopa kuanza upya anadhani wanaume wenye muafaka wamekwisha na hawezi kupata mwanaume mwenye sifa azitakazo

Unamuwaza sana pale anapokuwa mbali nawe…! Yaani mpaka mtu anashindwa kuwajibika kazini kwake, sasa huu si utegemezi ni kitu gani

Unashindwa kufurahia pale mnapohudhuria sherehe…Wakati mwingine kutokana na kumganda mume au mpenzi kila mnapotoka outing au mnapokuwa kwenye sherehe, wewe badala ya kujichanganya na watu wengine, lakini umemganda kama luba, unageuka kero hata mwenzi wako hatofurahia jambo hilo....huu ni utegemezi

Unakubali kunyanyasika….Lakini wewe umo tu...
Anakubudili atakavyo na wewe unakubali…. Najua wengi hawakuelewa kipengele hiki, hivi kama mpenzi wako au mwenzi wako anakunywa pombe, anavuta sigara, bangi au anatumia madawa ya kulevya, na wewe si mtumiaji wa vilevi hivyo basi na wewe ndio utumie kisa anataka ufanane naye ili kulinda mapenzi yenu ili asije akakuacha, sasa huu nao sio uegemezi?
 
Sijawahi kupenda, sijapenda na sitapenda, naona watu wanahangaika saana kutafuta wakumoyo mie huwa siamini kwalo, niliamua kuoa basi tu kwa sababu najitaji familia, kiujimla huwa siamini kama kuna mapenzi ya kweli hii karne bali ni wizi mtupu. Ukiona mwanamke anakupenda sana ujue there is a reason behind, hata kama ni mke wa ndoa, hawa wanawake wa hii karne ni tamaa tupu ya fedha hakuna upendo.
 
Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom