Dalili kuwa ana mwingine, na namna ya kumrudisha aendelee vema na wewe

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
1,449
574
WAPENZI wasomaji wa safu hii ya urembo, leo nitawaeleza jinsi ya kuuufanya mwili kuwa laini, kwa kutumia tui la nazi lililochanganywa na asali.
Wanawake wengi wanapenda kufanya miili yao kuwa na ngozi nyororo, lakini tatizo linakuja kwenye vipodozi wanavyovitumia.
Unaweza kuepuka matumizi ya vipodozi vyenye kemikali, ambavyo vinaweza kuleta madhara kwa ngozi na mwili wako kwa kutamia njia rahisi na za asili katika kulainisha ngozi yako.
Kujipodoa kwa njia za asili ni vizuri zaidi, kwa vile hakuna kemikali zozote zitakazokusababishia matatizo katika ngozi na mwili wako.
Naamini kila mtu analifahamu tui la nazi, pia asali inafahamika kwani vyote hivyo, vinatumika kama chakula kwa binadamu.

Jinsi ya kufanya
Kuna kipande kimoja cha nazi, kisha weka maji kidogo na kuchuja ili upate tui zito.
Weka tui hilo zito kwenye chombo kisafi na uchukue asali yako, kisha changanya na lile tui.
Changanya huo mchanganyiko mpaka uwe mzito.
Baada ya hapo paka mchanganyiko huo kwenye ngozi yako, huku ukisugua taratibu. Hakikisha hutumii nguvu nyingi.
Kaa muda wa saa moja baada ya kusugua mwili wako kwa kutumia mchanganyiko huo, kisha unaweza kwenda kuoga na kuendelea kupaka mafuta ya aina yoyote ya ngozi, unayopendelea kutumia.
Ukiendelea na zoezi hili kwa muda mrefu utaona matokeo yake.

Chanzo: Njia nyepesi kulainisha ngozi
 
Kazi kwenu
 
Watu wanataka matokeo ya haraka...ulipomalizia uzi kwa kusema ili mtu awe soft inabidi afanye hivyo kwa muda mrefu...nikaona hapa wale wa carolait hawawezi kukuelewa; umekuwa mkweli sana. Lol...
 
Mhhhh,

Title mbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaliii na habari yenyewe haviendan loh, anyway asante!
 
hapo hupande wa nazi mkuu sijakuelewa unasemea maji ya nazi au kipande cha nazi naomba unielekeze vizuri.:msela:
 
Back
Top Bottom