#COVID19 Dalili Kuu Nne za Wimbi la Tatu la COVID-19

Huu mzigo ni ngumu Sana kukabiliana nao

Waenda kwa mawimbi:

#1. Vikiwemo vifo bungeni 2020
#2. Vikiwemo vifo vya vigogo mapema 2021
#3. Vikiwemo hivi vifo vya ghafla karibuni

Kila mmoja hata tuliopo leo hasa walume, wenye magonjwa mengine, wazee na wasio chanjwa ni suala la muda tu. Kila mtu kwa wakati wake na wimbi lake atapeleka ripoti kwa kiongozi wa malaika.

Yasemekana mawimbi haya hayana mwisho. Kwamba Japan anacheza sasa na 5g.

Hili si saizi yetu. Tuwasikilize wenye mbavu zao!
 
Unapoambiwa kuna malaria kwa nini hufi kwa woga wakati malaria inaua watu wengi zaidi? Unapoambiwa kuna ukimwi na kutajiwa dalili zake kwa nini hufi kwa woga. Unapoambiwa kuna magonjwa ya moyo, kisukari au kipindupindu kwa nini hufi kwa woga?

Kutambua na kukiri upungufu ni kitendo cha maendeleo. Mbona kazi?
 
Ma
Mabibi na mabwana ugonjwa huu siyo saizi yetu. Kuufanyia mzaha ni kujipalia makaa sawa na mtoto mdogo anayechezea wembe.

Alpha, Beta, Gamma, Epsilon, Delta lugha hizi si za vijiweni na humo ndimo mzaliwa wa Wuhan anamotembea.

Ayajulie wapi hayo babu wa Loliondo, Buza kwa Mpalange au mlingotini bwagamoyo?

=====

Madaktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa upumuaji wamesema kirusi cha wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19, kimekuja na mbinu tofauti na za kificho kutokana na dalili zake kuu nne.

Dar es Salaam.

Dalili hizo zimetajwa kuwa ni mate kukauka mdomoni, kupata vipele mikononi na miguuni, kuharisha na damu kuganda kwenye mishipa ya moyo kunakosababisha oksijeni kutosambazwa mwilini na hivyo kusababisha kifo cha ghafla.

Akizungumza na Mwananchi jana, Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani ya mfumo wa upumuaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Elisha Osati, alisema kuna mabadiliko yanayoonekana katika dalili mbalimbali za Covid-19 ikilinganishwa na wimbi la kwanza na la pili.

Alisema katika maeneo ambayo wimbi la tatu limetokea kuna wagonjwa bado wanapata dalili za mwanzo, lakini kuna dalili mpya zimejitokeza tofauti na homa, kukohoa, kuchoka, kifua kubana au kupumua kwa shida, ingawa bado kuna wagonjwa wanapata dalili hizo.

“Kumekuwa na dalili za wagonjwa wapya, baadhi ya watu wanapata dalili ya kukauka kwa mdomo, unakuwa mkavu sana pamoja na ulimi kwa sababu hata mate yanakuwa hayatoki vizuri kwa sababu kirusi cha corona kimeonekana kinashambulia baadhi ya tishu na misuli inayozalisha mate iliyopo mdomoni,” alisema.

Chanzo: Mwananchi

=====
My take:
Kuukubali uzito wa ngoma ndiyo mwanzo wa kujua namna ya kuicheza.
Madaktari walikua wapi Zama za Mwendazake?
 
Covid ni ngumu sana kupambana nayo sababu ni airborne, plus hii makitu virus wake kuweza hata kuishi kwenye hard surfaces kwa muda mfupi
 
Madaktari Bingwa wa magonjwa ya mfumo wa upumuaji wamesema kirusi cha wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19, kimekuja na mbinu tofauti na za kificho kutokana na dalili zake kuu nne.

Dalili hizo zimetajwa kuwa ni:-

  • Mate kukauka mdomoni,
  • Kupata vipele mikononi na miguuni,
  • Kuharisha na
  • Damu kuganda kwenye mishipa ya moyo kunakosababisha oksijeni kutosambazwa mwilini na hivyo kusababisha kifo cha ghafla.

Katika maeneo ambayo wimbi la tatu limetokea kuna wagonjwa bado wanapata dalili za mwanzo, lakini kuna dalili mpya zimejitokeza tofauti na homa, kukohoa, kuchoka, kifua kubana au kupumua kwa shida, ingawa bado kuna wagonjwa wanapata dalili hizo.
Ugonjwa wa kwenye smartphone na TV
 
Mabibi na mabwana ugonjwa huu siyo saizi yetu. Kuufanyia mzaha ni kujipalia makaa sawa na mtoto mdogo anayechezea wembe.

Alpha, Beta, Gamma, Epsilon, Delta lugha hizi si za vijiweni na humo ndimo mzaliwa wa Wuhan anamotembea.

Ayajulie wapi hayo babu wa Loliondo, Buza kwa Mpalange au mlingotini bwagamoyo?

=====

Madaktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa upumuaji wamesema kirusi cha wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19, kimekuja na mbinu tofauti na za kificho kutokana na dalili zake kuu nne.

Dar es Salaam.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa upumuaji wamesema kirusi cha wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19, kimekuja na mbinu tofauti na za kificho kutokana na dalili zake kuu nne.

Dalili hizo zimetajwa kuwa ni mate kukauka mdomoni, kupata vipele mikononi na miguuni, kuharisha na damu kuganda kwenye mishipa ya moyo kunakosababisha oksijeni kutosambazwa mwilini na hivyo kusababisha kifo cha ghafla.

Akizungumza na Mwananchi jana, Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani ya mfumo wa upumuaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Elisha Osati, alisema kuna mabadiliko yanayoonekana katika dalili mbalimbali za Covid-19 ikilinganishwa na wimbi la kwanza na la pili.

Alisema katika maeneo ambayo wimbi la tatu limetokea kuna wagonjwa bado wanapata dalili za mwanzo, lakini kuna dalili mpya zimejitokeza tofauti na homa, kukohoa, kuchoka, kifua kubana au kupumua kwa shida, ingawa bado kuna wagonjwa wanapata dalili hizo.

“Kumekuwa na dalili za wagonjwa wapya, baadhi ya watu wanapata dalili ya kukauka kwa mdomo, unakuwa mkavu sana pamoja na ulimi kwa sababu hata mate yanakuwa hayatoki vizuri kwa sababu kirusi cha corona kimeonekana kinashambulia baadhi ya tishu na misuli inayozalisha mate iliyopo mdomoni,” alisema.

Chanzo: Mwananchi

=====

My take:

Kuukubali uzito wa ngoma ndiyo mwanzo wa kujua namna ya kuicheza.
Hatununui chanjo, hata kama zinakausha damu, madalali punguzeni njaa
 
Back
Top Bottom