#COVID19 Dalili Kuu Nne za Wimbi la Tatu la COVID-19

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Madaktari Bingwa wa magonjwa ya mfumo wa upumuaji wamesema kirusi cha wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19, kimekuja na mbinu tofauti na za kificho kutokana na dalili zake kuu nne.

Dalili hizo zimetajwa kuwa ni:
  • Mate kukauka mdomoni,
  • Kupata vipele mikononi na miguuni,
  • Kuharisha na
  • Damu kuganda kwenye mishipa ya moyo kunakosababisha oksijeni kutosambazwa mwilini na hivyo kusababisha kifo cha ghafla.
Katika maeneo ambayo wimbi la tatu limetokea kuna wagonjwa bado wanapata dalili za mwanzo, lakini kuna dalili mpya zimejitokeza tofauti na homa, kukohoa, kuchoka, kifua kubana au kupumua kwa shida, ingawa bado kuna wagonjwa wanapata dalili hizo.
 
Wametengeneza virus vya kompyuta na kuvi-update/kuvibadilisha badilisha,Sasa wamehamia kutengeneza virus vya binadamu na kuvibadilisha umbo ili wafanye biashara.

Alisikika mlevi mmoja akiropoka
 
Mabibi na mabwana ugonjwa huu siyo saizi yetu. Kuufanyia mzaha ni kujipalia makaa sawa na mtoto mdogo anayechezea wembe.

Alpha, Beta, Gamma, Epsilon, Delta lugha hizi si za vijiweni na humo ndimo mzaliwa wa Wuhan anamotembea.

Ayajulie wapi hayo babu wa Loliondo, Buza kwa Mpalange au mlingotini bwagamoyo?

=====

Madaktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa upumuaji wamesema kirusi cha wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19, kimekuja na mbinu tofauti na za kificho kutokana na dalili zake kuu nne.

Dar es Salaam.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa upumuaji wamesema kirusi cha wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19, kimekuja na mbinu tofauti na za kificho kutokana na dalili zake kuu nne.

Dalili hizo zimetajwa kuwa ni mate kukauka mdomoni, kupata vipele mikononi na miguuni, kuharisha na damu kuganda kwenye mishipa ya moyo kunakosababisha oksijeni kutosambazwa mwilini na hivyo kusababisha kifo cha ghafla.

Akizungumza na Mwananchi jana, Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani ya mfumo wa upumuaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Elisha Osati, alisema kuna mabadiliko yanayoonekana katika dalili mbalimbali za Covid-19 ikilinganishwa na wimbi la kwanza na la pili.

Alisema katika maeneo ambayo wimbi la tatu limetokea kuna wagonjwa bado wanapata dalili za mwanzo, lakini kuna dalili mpya zimejitokeza tofauti na homa, kukohoa, kuchoka, kifua kubana au kupumua kwa shida, ingawa bado kuna wagonjwa wanapata dalili hizo.

“Kumekuwa na dalili za wagonjwa wapya, baadhi ya watu wanapata dalili ya kukauka kwa mdomo, unakuwa mkavu sana pamoja na ulimi kwa sababu hata mate yanakuwa hayatoki vizuri kwa sababu kirusi cha corona kimeonekana kinashambulia baadhi ya tishu na misuli inayozalisha mate iliyopo mdomoni,” alisema.

Chanzo: Mwananchi

=====

My take:

Kuukubali uzito wa ngoma ndiyo mwanzo wa kujua namna ya kuicheza.
 
Kukauka mate mdomoni,kukauka sana mate midokoi,kuota vipere mikononi na miguuni na damu kuganda kutakaposababisha kifo cha ghafla.

Ni upuuzi mtupu akuna corona duniani Bali wanawapa watu hofu ili wachukuwe chanjo zao
 
Ni upuuzi mtupu akuna corona duniani Bali wanawapa watu hofu ili wachukuwe chanjo zao


"Ayajulie wapi hayo babu wa Loliondo, Buza kwa Mpalange au mlingotini bwagamoyo?"

Si sawa na kumweleza kuna sayari yaitwa Neptune?
 
Hivi sahizi kule ulaya corona imeisha ama ndio wamechanja wote? Mana kwenye mashindano ya EURO watu wanajazana na hawavai barakoa na magoli yanafungwa wanashangilia kwa kukumbatiana na kupigana mabusu!
 
Back
Top Bottom