Dalili kuu 7 zinazoonyesha mtu ambaye atachelewa sana kufanikiwa

Eddy Tarimo

Member
Nov 27, 2016
27
38
1. Siku zote ana pesa za kununua vocha na kuweka vifurushi, ana pesa za kununua nguo lakini hana pesa za kununua kitabu kitakachomuongezea maarifa.

2. Siku zote ana muda wa kuchart watsapp, kuangalia movie, kusoma magazeti na kupiga stori za mpira ama za wasanii lakini hana muda wa kusoma kuhusu taaluma yake ama mambo ya kumuongezea ujuzi.

3. Siku zote akiona waliofanikiwa anawatuhumu aidha wameiba, ni freemason ama wana bahati katika maisha. Huwachukia na hataki kujifunza kwao.

4. Siku zote hupenda kuhalalisha kufeli kwake kwa kujitetea, kulaumu uchumi, wazazi, serikali au amerogwa.

5. Siku zote hujiona anajua kuliko mtu yeyote yule na hapendi kujifunza kwa wengine. Huongea sana kuliko kusikiliza.

6. Kila anachoingiza anatumia, ukimwambia kusave ama kuwekeza anasema ngoja nipate cha ziada nitaanza kesho.

7. Anajua mambo mengi sana, anajua stori za mafanikio, anasoma vitabu lakini hafanyii kazi ama anafanyia kazi kidogo sana katika kile anachokijua.

Je Unayo dalili mojawapo kati ya hizo? Amua kubadilika ishi au fanya ukijua kesho ipo.
 
Unachokisema kinaweza kuwa na mahusiano kwa kiasi flani ila mafinikio hayana mpango maalumu unaweza ukawa umesoma vyuo vyote na mavyeti kibao lakini usiwe na mafanikio yoyote lakini unaweza mkuta tajiri mkubwa ameishia la saba tu au hata kujua kusoma alikuwa hajui ila amejifundisha kusoma baada ya kuwa tajiri
 
mhm , mafanikio ni nyota ya mtu ndugu, na wala hayana formula, pamoja na porojo zoote sijui vitabu , mafunzo ya ujasilia mali, huyo huyo anayecht unaweza kukuta huko face book akapata mchongo akauajiri na wewe

Ni kweli mafanikio hayana formula wala kanuni maalum lakini kuna vitu usipoviacha vinakupelekea kutokufanikiwa.

Mtoa mada hajapinga kutumia mitandao wala Facebook, shida ni pale unapopoteza muda wako wote huko bila malengo. Kwa utandawazi ulivyo sasa hivi hauwezi kukwepa Facebook, Twitter, blogs n.k lakini ukiwa teja wa hivyo vitu na kutumia muda wako wote huko hata kwa vitu visivyo na msingi otakuchukua muda sana kufikia malengo yenye tija.
 
1. Siku zote ana pesa za kununua vocha na kuweka vifurushi,ana pesa za kununua nguo lakini hana PESA za kununua kitabu kitakachomuongezea maarifa.

2. Siku Zote ana muda wa kuchart watsapp, kuangalia Movie, kusoma magazeti na Kupiga stori za mpira ama za wasanii lakini hana MUDA wa Kusoma kuhusu taaluma yake ama mambo ya kumuongezea ujuzi.

3. Siku zote akiona waliofanikiwa anawatuhumu aidha wameiba, ni freemason ama wana bahati katika maisha. Huwachukia na hataki kujifunza Kwao.

4. Siku zote hupenda kuhalalisha kufeli kwake kwa kujitetea, kulaumu uchumi, wazazi, serikali au amerogwa.

5. Siku Zote Hujiona anajua Kuliko Mtu Yeyote Yule na hapendi Kujifunza kwa wengine. Huongea sana Kuliko Kusikiliza.

6. Kila anachoingiza anatumia, ukimwambia kusave ama kuwekeza anasema ngoja nipate cha ziada nitaanza kesho.

7. Anajua mambo mengi sana, anajua stori za mafanikio, anasoma vitabu lakini hafanyii kazi ama anafanyia kazi kidogo sana katika kile anachokijua.

Je Unayo dalili mojawapo kati ya hizo?
Amua kubadilika ishi au fanya ukijua kesho ipo ....
Mara hasomi vitabu...mara anasoma....
 
Lakini akiweka vocha hiyo namba moja si anajifunza pitia mitandao mbalimbali kuliko kuwa na kitabu kimoja?

Ukiweka vocha ukasoma vitabu au ukajifunza vitu vya kukuongezea uelewa haupo kwenye hill kundi mkuu.
 
Ushauri mzuri! Lakini hoja Namba 1&7 zinapingana zenyewe
1. Siku zote ana pesa za kununua vocha na kuweka vifurushi,ana pesa za kununua nguo lakini hana PESA za kununua kitabu kitakachomuongezea maarifa.



7. Anajua mambo mengi sana, anajua stori za mafanikio, anasoma vitabu lakini hafanyii kazi ama anafanyia kazi kidogo sana katika kile anachokijua.
HIZI HOJA ZAKO MBILI ZINAPINGANA ZENYEWE
 
Mara hasomi vitabu...mara anasoma....

Hata Mimi niliingia kwenye huo mtego, hasa baada ya kusoma 1,2 na 7. Lakini hizi ni tabia ambazo ukiwa na mojawapo katika hizi, unahitaji kujirekebisha.

Namba 7 inaongelea wale wanaosoma vitabu lakini hawafanyii kazi wanayoyasoma au kujifunza, pia ni kundi la watu wanaojua vitu vingi kinadharia lakini hawajawahi kufanya kitu chochote kulingana na kiwango cha upeo wa uelewa wao.

Namba 1 na 2 zimejikita kwenye wale ambao hawana muda wa kutafuta vitabu au hata wakiwa na fursa ya kuvipata, hawatafuti muda wa kuvisoma.

Cc mswangilishi
 
asante mkuu kwa mjadala natumai nawe uko vizuri kiuchumi kwa jinsi ulivyodadavua hizo points..tunazifanyia kazi tutafika inshallah
 
Very true na vitabu vinasaidia pia kama huamini kamuulize bill gert atakwambia wakati wa mapumziko huwa anafanya nini.
 
Ungetuwekea hapa yale uliyofanikiwa wewe kwanza ili tujifunze kwa vitendo kupitia kwako
 
Back
Top Bottom