Dalili 13 za kuonyesha mwanamke ana mimba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dalili 13 za kuonyesha mwanamke ana mimba

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jun 13, 2013.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,423
  Likes Received: 4,283
  Trophy Points: 280
  [​IMG]  MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.

  Homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha mabadiliko kadhaa mwili ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya uchunguzi halisi kujua kama una ujauzito au la, anasema Melissa Goist, Profesa na Mtaalamu wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani.

  Maumivu kwenye matiti
  Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata rutuba jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.

  Maumivu mwilini
  Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.

  Kutokwa damu bila kutegemea
  ;Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai," anasema Goist. Anaongeza kwamba iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito.

  Kuchoka
  Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.

  Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi," anasema Goist.

  Chuchu kuwa nyeusi
  Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, Goist anasema: Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite."

  Kichefuchevu
  Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.

  Mwili kuvimba
  Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea, na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito, na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.

  Kwenda haja ndogo mara kwa mara
  Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.


  Tamaa ya vitu mbalimbali
  Kutokana na mwili kuwa na ;mzigo wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka, kwa mfano, aina fulani ya vyakula, au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.

  Kuumwa kichwa
  Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususan katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.

  Kufunga choo
  Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo, hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unaendelea kukua.

  Kuwa na hasira
  Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira, anasema Goist

  Kuongezeka kwa joto mwilini.
  Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna mtoto anakuja
   
  Last edited: Jan 4, 2016
 2. L

  Larusai Mux JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2013
  Joined: Oct 24, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Asante kwa elimu mkuu,
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2013
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu wewe ni mwisho wa maneno,tunafaidika sana kupitia mabandiko yako!
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2013
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,133
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 160
  Huo mstari mzuri
   
 5. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2013
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 14,474
  Likes Received: 2,651
  Trophy Points: 280
  Huo mstari unamaanisha nn?
   
 6. M

  Mgaya.com Member

  #6
  Jun 13, 2013
  Joined: Jun 13, 2013
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunashukuru kwa kutujuza
   
 7. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2013
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,403
  Likes Received: 2,041
  Trophy Points: 280
  Asanye mzizi! ila bado sijakusamehe na links vituko zako za jana zisizofunguka!
   
 8. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2013
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 10,998
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Aminia mkuu MziziMkavu, sasa fanya hisani: tumiminie jamvini dalili za mwanaume aliyetungisha mimba (ambaye amempa mwanamke mimba)
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2013
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,622
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  wewe mkali ndugu!kwani ulivyo mvimbisha shemeji ulijisikiaje?
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,423
  Likes Received: 4,283
  Trophy Points: 280
  MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni

  wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.


  “Homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha mabadiliko kadhaa katika mwili

  wake ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya uchunguzi halisi wa kujua kama mjauzito au la,”

  anasema Melissa Goist, Profesa na Mtalaama wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani.


  Maumivu kwenye matiti

  Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.

  Maumivu mwilini

  Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.

  Kutokwa damu bila kutegemea

  "Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,” anasema Goist. Ambaye anaendelea kusema kwamba iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito..

  Kuchoka

  Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.
  “Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi” anasema Goist.


  Chuchu kuwa nyeusi

  Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, Goist anasema: “Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.”

  Kichefuchefu

  Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.

  Mwili kuvimba

  Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.

  Kwenda haja ndogo mara kwa mara

  Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwa
  mba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.


  Tamaa ya vitu mbalimbali

  Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.

  Kuumwa kichwa

  Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.

  Kufunga choo

  Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.

  Kuwa na hasira

  "Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,” anasema Goist

  Kuongezeka kwa joto mwilini

  Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna “mtoto anakuja”.
   
 11. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 29,181
  Likes Received: 3,389
  Trophy Points: 280
  kuumbee...
   
 12. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2013
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,182
  Likes Received: 7,251
  Trophy Points: 280
  Ahahaha....!!! nice to know...wondering where am going to use this info now! au ndo mpaka ningoje miaka kadhaa ijayo...:angry:
   
 13. mwekundu

  mwekundu JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2013
  Joined: Mar 4, 2013
  Messages: 18,992
  Likes Received: 5,726
  Trophy Points: 280
  Yah u r right thanx for analysis

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 14. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2013
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 28,608
  Likes Received: 5,643
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu eti nina nahii yako ila ninatamani hii hapa
  [​IMG]
   
 15. M

  Mgaya.com Member

  #15
  Jul 3, 2013
  Joined: Jun 13, 2013
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu ndo zile feki zilizokamatwaga magomeni au siyo?
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,423
  Likes Received: 4,283
  Trophy Points: 280
  Bibie Mamndenyi nitakupatia ila sharti unizalie watoto 4 Mapacha kwa mpigo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2013
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 28,608
  Likes Received: 5,643
  Trophy Points: 280
  Hapana masharti ni magumu sana
  daah,
   
 18. kashesho

  kashesho JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2013
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 4,530
  Likes Received: 749
  Trophy Points: 280
  asante kwa somo
   
 19. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2013
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 28,608
  Likes Received: 5,643
  Trophy Points: 280
  Mgaya.com hizi ni za huko huko kwenye dunia.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. appoh

  appoh JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2013
  Joined: Mar 14, 2013
  Messages: 4,923
  Likes Received: 815
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye hasira nilikua namdunda mke wangu kipindi mjazito
   
Loading...