DALDO vs DED halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ndani ya bifu kali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DALDO vs DED halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ndani ya bifu kali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jasho la Damu, Aug 6, 2011.

 1. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni kumeanza kuzuka minyukano ya hatari ndani ya Halmashauri ya wilaya ya ngorongoro. wilaya hii inayoshika nafasi ya pili katika kuchangia pato katika fuko la taifa hali imekuwa ni tete hadi kufikia hatua watumishi wa halmashauri hiyo kuogopana na kutokuaminiana na wengine kujivika vyeo vya upambe wa kupeleka informations zisizo rasmi (majungu) kwa wakuu wa Idara na DED ili wajijengee trust kwao.

  Hali kadhalika wakuu wa idara hasa DALDO nao wamekuwa wakiunda makundi ya kibaguzi ndani ya idara zao ili kupata information za watumishi wanosimama katika ukweli bila kupindisha.

  Bifu kati ya DALDO na DED lilichagizwa kwa kauli ya DED ya kumlaumu DALDO kuwa hawajibiki ipasavyo huku akiwa na nguvu kazi kubwa ya rasilimali watu lakini anashindwa kuitumia, Kauli ya DED ilikuja baada ya DALDO kwenda kuomba fedha za malipo kwa ajili ya kuhudhuria semina iliyokuwa inafanyika katika jiji la Arusha wakati huo huo alikuwa hajamaliza hata wiki ofisini akitoka katika semina nyingine huko huko Arusha.

  Kama kile kinachoonekana sas hivi ni kila mtu kutumia power aliyokuwa nayo kumdefeat mwingine DALDO huyo amekuwa akikumbana na barriers mbalimbali ambazo zinawekwa na DED ili asikamilishe shughuli zake ijapokuwa vikwazo hivyo vinawekwa kwa shughuli zile ambazo DED anaona hazina tija kwa watumishi walioko chini yake na wananchi kwa ujumla.

  Ukweli ni kwamba DALDO huyo hana sifa zozote za uongozi hafai hata kuongoza familia, anapelekwa pelekwa ovyo na watumishi wake ambao yeye anaamin ndio royal subject wake kumbe ni haohao wanamzunguka upande wa pili na kumuharibia, ni mbaguzi wa kabila, dini na jinsia.
   
Loading...