Daladala zapewa ruhusa ya kusimamisha wanafunzi 4 tu kwa mkoa wa Dar es Salaam

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Pau Makonda ametoa ruksa wanafunzi wanne kusimama kwenye chombo kimoja cha usafiri.

Akihojiwa na kituo cha ITV, RC Makonda amesema:

“Nimeelekeza watu wote wa daladala kuhakikisha wanabeba wanafunzi wasiopungua wanne (4). Kama ni level seat kwa maelekezo tuliyowapatia, wazingatie level seat. Lakini inapokuja point ya wanafunzi, hawana sababu ya kumuacha kwasababu hana pesa ya kulipa kama mtu mzima, kwa maana ya kukaa kwenye kiti.”

“Wanafunzi wanne wakisimama ndani ya daladala hakuna dhambi yoyote ile. Kwahiyo, trafiki muliopo barabarani mukikuta gari limebeba wanafunzi wamesimama wanne kwenye daladala moja, msilikamate. Lakini ukikuta amebeba abiria akasimamisha, huyo ni halali yake kwasababu bado haijatenguliwa masharti ya kuondoka kwa level seat ila pale tu wanafunzi wanapohitaji kupanda usafiri huo ili waweze kuwahi shule na kuendelea na masomo.”
 
Italeta nafuu kidogo watu wakisimama kuliko ile level seat gari zenyewe chache hizi.
 
Mkuu wa mkoa wa Dsm mh Paul Makonda ametoa ruhusa kwa madereva wa daladala kupakia wanafunzi wanne watakaosimama.

Lakini Makonda amewataka askari kumshughulikia dereva yoyote atayesimamisha abiria ambao siyo wanafunzi.

Source: ITV Habari
 
Achilieni msingi na seko vitoto vimenenepeana sana huku majumbani mwisho vitadumaa bure
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom