Mpingamkoloni
Member
- Feb 14, 2021
- 13
- 32
Jana usiku nimefika mjini Mbeya nikafikia maeneo ya Igawilo, leo nilikuwa nina appointment na daktari kwa magonjwa yetu ya uzeeni.
Asubuhi hii nimejihimu stendi ili nipate gari niende mjini. Nimeshangaa sana kuona hakuna daladala. Nimepanda bajaji toka Igawilo hadi Kabwe kwa kutoa 1,500/= badala ya Shilingi 400 hadi 500 ambayo ningetoa ningepanda daladala.
Nimemuuliza kijana wa Bajaj kulikoni, mbona daladala sizioni? Akasema huu msimu wao wa kuchuma pesa, wakisusa wao wanakula. Kaniambia daladala hawataki kufanya nao kazi. Ati wanalalamikia Bajaj zinapendelewa. Ati wao hawana njia, bajaj inaruhusiwa kwenda kokote watakako. Wanasimamia kituo chochote watakacho. Kwa siku bajaj kila siku wanatoa 300/= kokote watakokwenda, ila Daladala lazima itoe 2,000/= kwa siku. Anasema bajaj pia zinaingia vituo vikuu, na kutozwa 1,500/=. Bajaj zinasimama sehemu yeyote katikati ya barabara na kuchukua abiria. Bajaj zinapita kwenye mataa hata taa zisipokuwa zawaruhusu na hawafanywi chochote, lakini daladala na magari binafsi yakifanywa hivyo wanapigwa faini.
Nimemwambia kwamba kwetu daladala haziruhusiwi kuingia njia kuu, kulikoni mbona ninyi ni rahisi sana kuzunguka mjini. Kasema wana bahati kuwa Mbeya, maana bajaj nyingi ni za viongozi wa Siasa walioko Mbeya hadi bungeni na pia watu wa vyombo vya ulinzi na Usalama na wanapeleka marejesho ya kukopa au ya kila siku. Jambo linawafanya viongozi wakuu wa Mkoa, pamoja na kufanya kazi vizuri sana iwape doa.
Nadhani kuna namna inapaswa kufanywa ili daladala na bajaj ziendelee kutoa huduma kwa wakazi wa Mbeya. Kwa sasa wananchi wanaumia.
Pia waendesha bajaj wafundishwe kuwa na nidhamu. Wafuate sheria za barabarani. Sheria za vyombo vya moto ziwaguse pia.
Mkuu wa Mkoa unafanya kazi vizuri saana, ila hii kitu inakuharibia sana. Wananchi wanaumia sana.
====
DALADALA MBEYA ZAGOMA ZAIDI YA SIKU NNE
Daladala zimazofanya kazi katika Jiji la Mbeya zimegoma ziidi ya siku nne wakishinikiza Bajajaji kutofanya kazi kama daladala.
Madai yao makubwa ni;
1). Bajaji zisipite njia kuu.
2). Bajaji ziwe na mkanda wa Pembeni unaonesha inapotoka kama ilivyo daladala
3). Wachore namba kuonesha ni bajaji namba ngapi
4). Madereva wa daladala wanataka Bajaji Wasiingie stendi ya Kabwe.
5). Madereva daladala wanataka Bajaji wasichukue abilia vituo vya daladala