Daladala Mbeya zagoma siku ya tano, mgogoro sugu ulioshindwa kutatuliwa wa bajaji

Mpingamkoloni

Member
Feb 14, 2021
6
45
Jana usiku nimefika mjini Mbeya nikafikia maeneo ya Igawilo, leo nilikuwa nina appointment na daktari kwa magonjwa yetu ya uzeeni.

Asubuhi hii nimejihimu stendi ili nipate gari niende mjini. Nimeshangaa sana kuona hakuna daladala. Nimepanda bajaji toka Igawilo hadi Kabwe kwa kutoa 1,500/= badala ya Shilingi 400 hadi 500 ambayo ningetoa ningepanda daladala.

Nimemuuliza kijana wa Bajaj kulikoni, mbona daladala sizioni? Akasema huu msimu wao wa kuchuma pesa, wakisusa wao wanakula. Kaniambia daladala hawataki kufanya nao kazi. Ati wanalalamikia Bajaj zinapendelewa. Ati wao hawana njia, bajaj inaruhusiwa kwenda kokote watakako. Wanasimamia kituo chochote watakacho. Kwa siku bajaj kila siku wanatoa 300/= kokote watakokwenda, ila Daladala lazima itoe 2,000/= kwa siku. Anasema bajaj pia zinaingia vituo vikuu, na kutozwa 1,500/=. Bajaj zinasimama sehemu yeyote katikati ya barabara na kuchukua abiria. Bajaj zinapita kwenye mataa hata taa zisipokuwa zawaruhusu na hawafanywi chochote, lakini daladala na magari binafsi yakifanywa hivyo wanapigwa faini.

Nimemwambia kwamba kwetu daladala haziruhusiwi kuingia njia kuu, kulikoni mbona ninyi ni rahisi sana kuzunguka mjini. Kasema wana bahati kuwa Mbeya, maana bajaj nyingi ni za viongozi wa Siasa walioko Mbeya hadi bungeni na pia watu wa vyombo vya ulinzi na Usalama na wanapeleka marejesho ya kukopa au ya kila siku. Jambo linawafanya viongozi wakuu wa Mkoa, pamoja na kufanya kazi vizuri sana iwape doa.

Nadhani kuna namna inapaswa kufanywa ili daladala na bajaj ziendelee kutoa huduma kwa wakazi wa Mbeya. Kwa sasa wananchi wanaumia.

Pia waendesha bajaj wafundishwe kuwa na nidhamu. Wafuate sheria za barabarani. Sheria za vyombo vya moto ziwaguse pia.

Mkuu wa Mkoa unafanya kazi vizuri saana, ila hii kitu inakuharibia sana. Wananchi wanaumia sana.

====

DALADALA MBEYA ZAGOMA ZAIDI YA SIKU NNE

Daladala zimazofanya kazi katika Jiji la Mbeya zimegoma ziidi ya siku nne wakishinikiza Bajajaji kutofanya kazi kama daladala.

Madai yao makubwa ni;

1). Bajaji zisipite njia kuu.

2). Bajaji ziwe na mkanda wa Pembeni unaonesha inapotoka kama ilivyo daladala

3). Wachore namba kuonesha ni bajaji namba ngapi

4). Madereva wa daladala wanataka Bajaji Wasiingie stendi ya Kabwe.

5). Madereva daladala wanataka Bajaji wasichukue abilia vituo vya daladala
IMG-20210515-WA0013.jpg
 
solenza

Member
Jan 16, 2014
6
45
Natamani kuwahurumia watu wa daladala lakini kila nikikumbuka walivyozoea kufanya biashara ya usafirishaji kimazoea naona wamepelekea pia kuchangia babaj kushamiri na kuonekana usafiri mbadala kwa abiria.
Palikuwa na desturi mbaya sana kwa daladala mkoani Mbeya, nimesoma na kuishi hapo kwa muda mrefu. Napafaham vizuri.

1) Daladala wao nyakati zote wanachokijali ni kutimiza malengo yao ya kihesabu bila kufikiri kuhusu matakwa ya abiria na uharaka wa safari yake au matumizi ya muda. Unakuta hiace imeshajaza level seat pale Kabwe asubuh na una haraka say ukamjulie hali mgonjwa pale Rufaa hospital, lakini kondakta na dereva watajizungusha ili mrad apate abiria wa ziada watatu wanne wa kusimama ndipo safari ianze.
Mbaya zaidi hiyo hali itaendelea hta ktk vituo vingine visivyokuwa na abiria yeyote anayehitaji kushuka, watasimama na kuanza kuitilia itilia. Kero sana. Kuwahi kote inakuwa kazi bure.

2) Daladala wanamjali abiria pale tu ambapo wanamuhitaji aingie kwny chombo chao cha usafiri. Once ukishaingia hakuna Heshima, adabu, haki, wala lugha za staha katika maongezi na majibizano mle ndani. Kwa kifupi Ile Customer service kwa abiria ni mbovu sana. Hapo hujagusia kero za madirisha kutopitisha hewa safi, uchakavu wa siti, na bugudha ndgo ndgo za siti mates.

Kero zao ni nyingi sana, na ingawa hii haihalalishi utovu wa nidhamu na ukiukwaji wa Sheria za barabarani unaofanywa na watu wa Bajaj, lakini lazima tukubali kuwa kushamiri kwa Bajaj kumeshangiwa Sana na abiria kuchoshwa na Mambo hayo ya Daladala yaliyodumu miaka na miaka
 
KAWETELE

JF-Expert Member
Dec 11, 2015
574
1,000
Bajaji za Tulia Trust..

Bajaji ni chanzo kikuu cha ajali mbeya.. wao sheria na alama za barabarani haziwahusu. Traffic wapo na hawa wagusi kisa wanamuogopa Tulia.

Mbeya barabara classic ina njia tatu.. nayo ya kizushi flani.. sasa Bajaji wao ndio mabingwa wa kuvunja sheria hapo.. hata kama upande wake hamna foleni.. basi ataamua tu kupita katikati wakati siyo muda wake.

Bajaji hazina route maalum wao wanaenda popote.. kwa logic hiyo hiyo basi wangeruhu na daladala zifanye hivyo hivyo.

Solution ya hii ni Kumtoa Mkuu wa mkoa.. ambaye yeye pamoja na Tulia wana miliki Bajaji za kutosha.
 
Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
11,882
2,000
Jana usiku nimefika mjini Mbeya nikafikia maeneo ya Igawilo, leo nilikuwa nina appointment na daktari kwa magonjwa yetu ya uzeeni.

Asubuhi hii nimejihimu stendi ili nipate gari niende mjini. Nimeshangaa sana kuona hakuna daladala. Nimepanda bajaji toka Igawilo hadi Kabwe kwa kutoa 1,500/= badala ya Shilingi 400 hadi 500 ambayo ningetoa ningepanda daladala.

Nimemuuliza kijana wa Bajaj kulikoni, mbona daladala sizioni? Akasema huu msimu wao wa kuchuma pesa, wakisusa wao wanakula. Kaniambia daladala hawataki kufanya nao kazi. Ati wanalalamikia Bajaj zinapendelewa. Ati wao hawana njia, bajaj inaruhusiwa kwenda kokote watakako. Wanasimamia kituo chochote watakacho. Kwa siku bajaj kila siku wanatoa 300/= kokote watakokwenda, ila Daladala lazima itoe 2,000/= kwa siku. Anasema bajaj pia zinaingia vituo vikuu, na kutozwa 1,500/=. Bajaj zinasimama sehemu yeyote katikati ya barabara na kuchukua abiria. Bajaj zinapita kwenye mataa hata taa zisipokuwa zawaruhusu na hawafanywi chochote, lakini daladala na magari binafsi yakifanywa hivyo wanapigwa faini.

Nimemwambia kwamba kwetu daladala haziruhusiwi kuingia njia kuu, kulikoni mbona ninyi ni rahisi sana kuzunguka mjini. Kasema wana bahati kuwa Mbeya, maana bajaj nyingi ni za viongozi wa Siasa walioko Mbeya hadi bungeni na pia watu wa vyombo vya ulinzi na Usalama na wanapeleka marejesho ya kukopa au ya kila siku. Jambo linawafanya viongozi wakuu wa Mkoa, pamoja na kufanya kazi vizuri sana iwape doa.

Nadhani kuna namna inapaswa kufanywa ili daladala na bajaj ziendelee kutoa huduma kwa wakazi wa Mbeya. Kwa sasa wananchi wanaumia.

Pia waendesha bajaj wafundishwe kuwa na nidhamu. Wafuate sheria za barabarani. Sheria za vyombo vya moto ziwaguse pia.

Mkuu wa Mkoa unafanya kazi vizuri saana, ila hii kitu inakuharibia sana. Wananchi wanaumia sana.

View attachment 1785399
Mbeya hawajawahi kuwa na usafiri wa daladala, acha kuongopea watu
 
Lob

JF-Expert Member
Jul 24, 2017
804

Tanzania inatakiwa Kuwa na Taasisi imara ambazo zitafanya kazi kwa nizamu na weledi bila kujali siasa na wanasiasa.
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,141
2,000
Kuna upumbavu sana, unapiga marufuku hiace mjini halafu unaruhusu bajaji?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom