Daladala kuondoka Dar taratibu mabasi ya mwendo kasi yatakapoanza kufanya kazi

The Wolf

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
9,396
20,631
Taarifa ikufikie kwamba mabasi hayo yatakapoanza daladala zote zitatoka na alielithibitisha hilo March 29 2016 ni meneja mawasiliano wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) David Mziray wakati akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu kukosekana vituo kwenye barabara ya Morogoro.

>>>’huu mradi wa mabasi yaendayo haraka utakapoanza mabasi ya daladala yote yatatoka, ndio maana utaona mabasi mengi yanayotumia barabara hizi za mchanganganyiko kwa maana magari ya kawaida na mabasi, hakuna vituo vya daladala kwa kuwa hiki ni kipindi cha mpito, yakishaanza haya mabasi ya mwendo wa haraka, huduma hizi za mabasi ya kawaida zitasimama’

NB: Naombeni ufafanuzi,

1. Huu mradi wa DART kuna kipindi tulisikia kuna majadiliano kati ya uongozi na madereva wa DSM, je wamejumuishwa katika umiliki?

2. Mradi unamilikiwa na serikali kwa asilimia ngapi?

3. Ina maana vipato vyote vya wananchi wamiliki wa dala dala vinahamia kwa mtu(kampuni) mmoja?kama sivyo je hawa wadau serikali ina mpango gani nao?
 
Mkuu Daladala zitatafuta njia.
Ni mradi mkubwa saana,
Wenye Daladadala lazimaa njaa iingie,na ndio maana kila ukimgusa mmiliki wa daladala anakuambia anaiuza,
Tena zinauzwa bei chee kweli siku hizi.

Daladala zitahama routes na kuingia nje ya mji,ambapo nyingi zitashindwa maana zitajikuta zoote zipo kwenye soko moja la vichochoroni.

Hapo Hekma ya Meya Mpya na jopo lake inasubiriwa,maana Bodaboda wanamsikilizia,na Daladala pia wanamsikilizia kwa sasa
 
Zoezi hilo litakuwa Na challenge nyingi...lkn ztazoeleka Na mambo yataenda kma kawaida
 
Nilikua najiuliza sana kuhusu vituo Ktk hizi barabara zao coz daladala wanakera sana wakisimama pale kituoni! Kuuuuuumbe!
 
Najiuliza tu
Kama huu mradi unakaribia anza kwanini Sumatra wanatoa vibali kwa gari mpya kuingia ruti za barabara ya morogoro?
Kwanini wasizizuie huko huko mapema kabisa
 
inawezekana kweli ndio maana daladala hazina pa kushusha na kupandisha abiria sehemu nyingine
 
Kamradi ka kinafiq katajifia baadae kama wafavyo wanafiq wote.time will sema
 
Hao watu wa daladala wacha watolewe waende wanakojua,wananyanyasa sana wav wakat wa jioni,wanafika kituoni halafu wanakwambia hawapakii,akina mama watu wazima wanahangaika hovyo kukimbilia magari,wakiamua kuwa panya road basi mapanga yapo,petrol ipo,matairi yapo,viberiti vipo na mawe yapo,kadhalika jela zipo
 
Taarifa ikufikie kwamba mabasi hayo yatakapoanza daladala zote zitatoka na alielithibitisha hilo March 29 2016 ni meneja mawasiliano wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) David Mziray wakati akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu kukosekana vituo kwenye barabara ya Morogoro.

>>>’huu mradi wa mabasi yaendayo haraka utakapoanza mabasi ya daladala yote yatatoka, ndio maana utaona mabasi mengi yanayotumia barabara hizi za mchanganganyiko kwa maana magari ya kawaida na mabasi, hakuna vituo vya daladala kwa kuwa hiki ni kipindi cha mpito, yakishaanza haya mabasi ya mwendo wa haraka, huduma hizi za mabasi ya kawaida zitasimama’

NB: Naombeni ufafanuzi,

1. Huu mradi wa DART kuna kipindi tulisikia kuna majadiliano kati ya uongozi na madereva wa DSM, je wamejumuishwa katika umiliki?

2. Mradi unamilikiwa na serikali kwa asilimia ngapi?

3. Ina maana vipato vyote vya wananchi wamiliki wa dala dala vinahamia kwa mtu(kampuni) mmoja?kama sivyo je hawa wadau serikali ina mpango gani nao?
Pia naamini bei za nauli zitakua rafiki kwa kipato cha mtanzania wa chini
 
Back
Top Bottom