Daladala kuchomewa nondo madirishani, ni sawa kiusalama?

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
7,312
6,770
Jijini Dar es salaam siku hizi daladala nyingi zimechomewa nondo(au bomba za chuma) madirishani kwa ndani, yaani kuanzia nyuma ya gari hadi mbele inakwa mistari miwili au mitatu inawekwa kila upande. Na nimejaribu kudodosa naambiwa eti ni kuzuia abiria wasiegemee vioo vya madirisha eti huwa wanavivunja!

Hivi jamani, haya magari kweli yanaruhusiwa kubeba abiria yakiwa na hali ile, ki usalama inakuwaje?, gari ikipata ajali yale ma-vyuma si yatakuwa ndiyo "kichinjio" kikuu cha kuua abiria??
Sheria za usalama barabarani inaruhusa kweli hali hii? au tunasubiri moto uje uwake kwenye daladala na abiria waungue wote ndiyo mamlaka zinazo husika zije zizuie hatari hii??
 
kiusalama kwa kweli si sahihi kwa mfano moto unaweza kutokea na watu wakajiokoa kwa kupitia madirishani.
 
Ongezea na je kupitia dirishani wakati wa kuingia au kutoka kwenye hilo daladala je ni usalama nao? Tujiulize ni kwanini wameweka nondo hawa watu? Abiria nao ustaarabu hawana kabisa hasa wale wa pande kwenye Arsenal kule
 
kusema kweli Ukiendesha ukaguzi wa madaladala ya Dar es salam, hakika hupati hata madaladala 70 mazima, kweli Trafic na majembe wameng'ang'ana kukagua TLB na Insurance wakati hayo madaladala hayafai hata kubebea nguruwe.
 
Kuchomea nondo au mabomba kiusalama ni hatari sana gari ikiangushwa na ikalalia mlango sijui itakuwaje. Mabasi ya mikoani nayo yalikuwa na tabia hiyo wamiliki wakapewa onyo kali mchezo huo ukaisha.Kamanda Kombe sijui yuko wapi maana bado yanaingia kwenye vituo vya mafuta na abiria wakiwa wamejazana
 
hio ni hatari kubwa sana wakati wa dharula kwani mtu hatoweza kuokoa maisha yake kupitia dirisha au waokoaji wanaweza kupata shida kuokoa watu wakati wa ajali.

wahusika wako wapi kweli hizo dalala zinatakiwa watoe hizo nondo au abiria wewe binafsi kama una jali maisha yako basi usipande dalala za haina hio.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom