Daktari: Watumiaji wa dawa kuzuia hedhi hatarini kupata magonjwa ya MOYO

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,456
Wataalam wa afya wametoa angalizo kwa wanawake wanaotumia dawa za kuzuia hedhi bila kuzingatia ushauri wa daktari kuwa wako hatarini kupata madhara, yakiwamo maradhi ya moyo.

Daktari wa Magonjwa ya Kinamama Hospitali ya Rufani Mkoa wa Njombe, Shomari Masenga ametaja dawa hizo kuwa zimegawanyika katika makundi matatu Primolut Tables, Ergometrine Injection na Combined Oral Contraceptive pill.

Amesema Primolut Tables ni dawa wanazopewa wanawake ambao wanatoka damu nyingi na wamepoteza mpangilio wao wa kuingia hedhi.

"Inatengenezwa na 'component' ya projestine ambayo inafanya kazi ya kupunguza uzito kwenye ukuta wa ndani wa mfuko Wa uzazI ambao ukipungua ndiyo damu inatoka nyingi.

"Madhara ya dawa hizi ni kubadilisha mzunguko wa hedhi, kukosa usingizi, kuongezeka uzito, kizunguzungu, kukosa hisia za kufanya mapenzi na kuwa na hasira," alifafanua.

Kuhusu matumizi ya Ergometrine Injection anasema ni dawa zinazotumiwa na mama mjamzito baada ya kutoka kwa kondo la nyuma na kupoteza damu nyingi na zinatengenezwa kwa 'component ya Ergometrine Maleate.

Hata hivyo, daktari huyo alitoa angalizo kuwa dawa hizo sasa hazitumiki hospitalini kutokana na madhara yaliyobainika.

"Husababisha 'heart attack (shambulio la moyo) kwa mtumiaji, moyo unaweza Ukafa kwa sababu ya kukosa damu, seli za moyo zitashindwa kufanya kazi, kifua kujaa maji hadi kupelekea kifo. Madhara mengine ni kupumua kwa shida," anasema.

Kuhusu Combined Oral Contraceptive Pill, daktari huyo alisema aina hiyo ya dawa ni kwa ajili ya Uzazi wa mpango, akifafanua: "Hii inatumika kuchelewesha siku na kutibu kama unavuja damu nyingi. Dawa hizi zinafanya kazi ya kuzuia kutoka kwa damu ya hedhi, mara nyingi dawa hizi wanapewa ambao wanatoka damu kupitiliza pamoja na wanaotaka kuchelewesha hedhi.

“Zimetengenezwa kwa component aina mbili -- Oestrogen na Progestine. Zinafanya kazi gani? Zinazuia upevushaji wa yai, kusababisha ute wa shingo ya kizazi kuwa mzito na mbegu za kiume kushindwa kupita.

"Madhara yake kiafya ni kwamba zinasababisha kutoka damu kidogo kidogo, shida ya moyo, damu kuganda kwa wenye umri kuanzia miaka 35.

"Madhara mengine ya dawa hizi zote ni makubwa kwa sababu yanasimamisha ufanyaji kazi wa vichocheo katika mwili, wengi wanaotumia dawa hizoni wale ambao wanakuwa na 'matukio'.

"Mtu anakuwa anataka kwenda kwa mpenzi wake au kwenda sehemu yoyote hataki kuwa kwenye hedhi, basi anakunywa dawa hizi ili kuzuia," Dk. Masenga.


Chanzo: Nipashe
 
Duh hatari hii kuna na dawa za kuzuia hedhi tena
My dear hizo dawa zipo na kama nimemwelewa vyema hapo kasemea wale wanaotoka damu nyingi ya hedhi ambayo inapitiliza zile siku tulizozizowea hivyo akienda Hospitali inabidi wapewe dawa ili hiyo hedhi ikate.

Na kwa mfano kuna wale wanaotumia dawa za uzazi wa mpango halafu zikawakataa mfano masindano hayo mara nyingi zinakuwa na maudhi kama hayo ya hedhi isiyokoma.
 
My dear hizo dawa zipo na kama nimemwelewa vyema hapo kasemea wale wanaotoka damu nyingi ya hedhi ambayo inapitiliza zile siku tulizozizowea hivyo akienda Hospitali inabidi wapewe dawa ili hiyo hedhi ikate.

Na kwa mfano kuna wale wanaotumia dawa za uzazi wa mpango halafu zikawakataa mfano masindano hayo mara nyingi zinakuwa na maudhi kama hayo ya hedhi isiyokoma.
Sweetie kwanza hujambo?
Kuna pahala kasema wanazuia hedhi ili akutane na mpenzi wake,, yaani wanaichelewesha ili akigongeshe
 
Kumbe !!!, Mimi siku zote huwa nadhani papuchi haipanukagi
Haipanuki kirahisi ila sio muda wote kuna kitu kimewekwa hapo, mfano mdogo tafuta kitu chenye mpira halafu kipanue muda mrefi utakuta lastic zimelegea na hizo pedi Ni hivyo
 
Sweetie kwanza hujambo?
Kuna pahala kasema wanazuia hedhi ili akutane na mpenzi wake,, yaani wanaichelewesha ili akigongeshe
Mie Alhamdulillah sijambo mwaya. I hope nawe uko mzima pia.

Duuh! Dunia inakwenda sana kasi aisee.
 
Back
Top Bottom