Daktari wa uzazi awadunga mimba mwenyewe wanawake 49 bila ridhaa yao

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Daktari wa uzazi wa kusaidiwa nchini Uholanzi anayeshutumiwa kwa kupandikiza mbegu zake za uzazi kwa waginjwa bila ridhaa yao amethibitishwa kuwa baba wa watoto 49.

Vipimo vya vinasaba -DNA vimefichua kuwa Jan Karbaat, aliyefariki dunia miaka miwili iliyopita aliwapa mimba mama zao katika kliniki yake iliyopo katika eneo la Bijdorp, karibu na Rotterdam.

Vipimo hivyo vilithibitishwa Ijumaabaada ya jaji kuruhusu vitangazwe.

Mmoja wa watoto , kwa jina Joey, alisema "hatimae amefunga ukurasa " sasa anajua Bwana Karbaat alikuwa ndiye baba yake.

"Baada ya uchunguzi wa miaka 11 ninaweza kuendelea na maisha. ninashukuru kwamba hatimae nimeelewa wazi," aliliambia shirika la utangazaji la uholanzi NOS.

Tim Bueters, wakili ambaye aliwawakilisha watoto 49, alisema kuwa ameridhishwa na matokeo ya kesi ya baada ya miaka ya kutokuwa na uhakika.

"Inamaanisha kwamba hatimaeimekuwa wazi kwa watoto ambao wanafanana," aliliambia shirika la utangazaji la NOS.

Bwana Karbaat alipelekwa kwa mara ya kwanza mahakamani mwaka 2017 na kikundi cha watoto wa uzazi wa msaada na wazazi wake baada ya kushuku kuwa walikuwa na uhusiano.

Moja ya kesi hizo ilihusu mtoto wa msaada ambaye alifanana kwa maumbile na daktari , makakama ilimsikiliza.

mali zake zilichukuliwa kutoka kwenye nyumba yake baada ya kifo chake Aprili 2017 akiwa na umri wa miaka 89.

' tuhuma kubwa '

mwaka 2017 jaji aliamuru kuwa vipimo vya vinasaba -DNA vinaweza kuchukuliwa na kuhifadhiwa kwa siri hadi matokeo zaidi ya kesi hiyo yatakapotolewa.

Mwezi February mwaka huu, mahakama ya Wilaya ya Rotterdam iliamua kuwa matokeo ya vipimo yanaweza hatimae kufichuliwa.

Yanaonyesha yanathibitisha "tuhuma kali kwamba Bwana Karbaat alitumia mbegu zake za kiume za uzazi katika kliniki yake ",ilisema taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya kampuni ya sheria ya Rex Advocates.

Bwana Karbaat alijiita "muanzilishi katika fani ya uzazi wa msaada ".

kliniki yake ilifungwa mwaka 2009 wakati yalipokuwa madai kwamba alikuwa na data zisizo sahihi, uchunguzi na maelezo ya yasiyo sahihi kuhusu uzazi wa msaada na ruhusa ya kuruhusiwa kuwa na idadi ya watoto sita kwa kila mtoaji wa mbegu za uzazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa alipiga hesabu kubwa
 
Inabidi tuwasindikize wake zetu wanapokwenda kuonana na ma gynae,hii nikimaanisha mpaka huko ndani kwenye vyumba vya matibabu maana kwa mwendo huu tutakuwa tunawalelea watoto wao...
 
Hahaa sio kwamba kawala bana.. Yaani ukiwa hupandi mtungi ukienda hospitali kupewa msaada basi mkeo anaingizwa artificial insemination.. Sasa kuokoa gharama huyu daktari anatumia mbegu zake tuuu kuzuia complication na kuleta furaha kwa familia zilizokwama kupata watoto... Sasa naona wanashangaa kufanana na daktari kila kitu.. Jamaa alikuwa dorminant gene wa namna yake
 
Aisee, wanaume sisi ni hatari tupu.

Uangalie jamaa anavyofanya mambo
 
Back
Top Bottom