Daktari wa rais Kikwete apanda cheo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daktari wa rais Kikwete apanda cheo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mpita Njia, Oct 22, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone: 255-22-2114512, 2116539
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
  Fax: 255-22-2113425
  PRESIDENT’S OFFICE,
  THE STATE HOUSE,
  P.O. BOX 9120,
  DAR ES SALAAM.
  Tanzania.

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Daktari wa Rais Kikwete awa Profesa

  Daktari Mkuu Binafsi wa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Janabi amepandishwa daraja la usomi wa utibabu na kuwa Profesa wa Chuo cha Utibabu cha South Carolina (MUSC) kitengo cha magonjwa ya moyo nchini Marekani kuanzia Oktoba Mosi, mwaka huu, 2010.

  Dk. Janabi (47) amekubali kupandishwa daraja hilo ambako atakuwa Profesa Mshiriki wa Tiba katika Idara ya Utibabu, Sehemu ya Tiba ya Moyo, kwenye chuo hicho kilichoko mjini Charlestown.

  Hata hivyo, Dk. Janabi ambaye ni mmoja wa Watanzania wachache wenye sifa na ujuzi mkubwa zaidi katika udaktari, anaendelea kuwa Daktari Mkuu Binafsi wa Rais Kikwete.

  MUSC ni chuo kikuu kikubwa zaidi na maarufu zaidi kuliko kingine chochote katika Jimbo la South Carolina na anakuwa Mtanzania wa kwanza kupata utambuzi na heshima ya namna hiyo kwenye chuo hicho ambacho amekuwa nao kikazi tangu mwaka 2003.

  Dk. Janabi alipata Shahada ya Uzamivu (PhD) mwaka 2000 nchini Japan katika fani ya magonjwa ya moyo. Mbali ya kuwa Daktari Mkuu Binafsi wa Rais Kikwete, mtaalam huyo wa magonjwa ya moyo pia ni mtaalam bingwa wa masuala ya moyo kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Mkufunzi wa Heshima katika Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi cha Muhimbili (MUHAS).

  Dk. Janabi pia ni Mwanasayansi Mwandamizi katika Utafiti wa Chanjo ya Ukimwi na Mkurugenzi Mwakilishi (Tanzania) wa Taasisi ya Kimataifa ya Madaktari wa Africa.

  Amekuwa Daktari Mkuu Binafsi wa Rais Kikwete tokea 2006.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.


  22 Oktoba, 2010


   
 2. E

  Edo JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hongera Prof Janabi
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hongera sana Dr Janabi! Ni muhimu ukatuwekea bayana hali ya kiafya ya Kikwete
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Well done!

  Natoa hongera sana kwa Professor huyu, hakika ni mweledi wa juu, japo Mkulu hamwamini sana, anaamua kuchanganya na za kwake, ndio maana maji yanazidi unga akiwa majukwaani!

  Na yule rafiki yangu Dr. Peter Mfisi ndiye Msaidizi wa M.Janabi?
   
 5. Caren

  Caren JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2010
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Congrats Prof. Janabi,
  You are doing a great job monitoring the defective and thinned jugular vein that takes blood to the head of our dear president. Had it not been you and your expertise surely we would be speaking in a different languages now.

  I hope your further research will sufficiently help in ensuring that we have someone healthy upto 2015.   
 6. Caren

  Caren JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2010
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Congrats Prof. Janabi,
  You are doing a great job monitoring the defective and thinned jugular vein that takes blood to the head of our dear president. Had it not been you and your expertise surely we would be speaking in a different languages now.

  I hope your further research will sufficiently help in ensuring that we have someone healthy upto 2015.   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Hongera Professor.....lakini kwa nini client/patient wako anaangukaanguka?....je unatibu pia na familia yake?
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Daktari binafsi?i bana haya mavyeo ya State House yananipaga raha sana..Kuna yule mwingine anagawaga mbuzi na migunia ya mchele wakati wa idd anaitwa MNIKULU sijui nani? yeye hajapandishwa cheo tu
   
 9. p

  pierre JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimefikuta t-shirt na kofia za ccm nyumbani niliporudi jioni.Nilipoziona nikauliza vipi kulikoni n a nguo za rangi za chama,ndipo akaniambia dada aliyepokea kuwa ameleta mjumbe.Akanieleza kuwa alikuwa akigawa kwa watu mbali mbali katika eneo ninaloishi.
  Je hii sio rushwa kama ile aliyopewa askofu dr.mokiwa? Na je nirudishe kwa mjumbe au ninyamaze tu?
  Wapenda maendeleo na wanamageuzi nipeni nini cha kufanya na hii kofia na t-shirt ya hawa mafisadi?
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Moddy Janabi (Dr)... hongera sana..u deserve it..u earned it.
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kama unafunga Mbwa mvalishe, ama sivyo mpe dada afanye dekio! wewe na kizazi chako msijaribu kuvaa mtajipa laana.

  Mch Masa K
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Jamaa akiingia Vingunguti mbuzi wote wanakuja juu wanataka kumtwanga pembe
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hahahaha hahahaha nimeipenda hii comment yako ya kumpongeza daktari wa rais kuwa profesa. ilihali patient wake ni mbishi sana
   
 14. October

  October JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hongera sana Daktari.
  Lakini Kwani client wako anasumbuliwa na nini? Mbona anaanguka mara kwa Mara...?
   
 15. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hongera sana,lakini onyesha weredi wako kwa kumtibu rais wetu!si unajua tena ule ugonjwa wake!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 16. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  So what? I smell a rotten rat in this letter. Personal Doctor to be exaggerated like that?Even if.......................................................................................
   
 17. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #17
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kumbe kikwete ana daktari aliebobea kwenye Tiba, sasa mambo ya kichawi ya nini ? ama kweli jasiri haachi asili.
   
 18. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Muungwana ameshauriwa na 'DR" wake kuwa hewa ya pale Jangwani ni chafu sana ndio maana anaanguka anguka akihutubia pale kwahiyo msijemkashangaa mkutano wake wa mwisho wa kampeni akahamia uwanja wa Taifa!!
   
 19. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #19
  Oct 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  nimepata majibu kwanini mkulu anaangukaanguka: dr wake ana majukumu mengi mno.
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hayo ni matusi ya viatuni we kizee, ha ha ha!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...