Daktari wa Marekani Amlazimisha Mgonjwa wa Akili Ameze Misumari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daktari wa Marekani Amlazimisha Mgonjwa wa Akili Ameze Misumari

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Sep 8, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Saturday, August 29, 2009 4:01 PM
  Daktari katika hospitali ya watu wenye matatizo ya akili nchini Marekani amefikishwa mahakamani baada ya kumpa mgonjwa mmoja wa akili misumari minne na kumlazimisha aimeze. Athena Marie Sidlar, 28, mtaalamu wa magonjwa ya akili kwenye hospitali ya Allentown State Hospital,Pennsylvania nchini Marekani alikiri kumpa mgonjwa wa akili misumari minne na kumlazimisha aimeze.

  Mahakama ilimuona Athena ana hatia ya kuhatarisha maisha kufuatia kitendo chake hicho cha kizembe na huenda akahukumiwa kwenda jela miaka miwili.

  Polisi walisema kwamba mwezi januari mwaka huu, Athena alimuonyesha mgonjwa wa akili wa kike mwenye umri wa miaka 18 jinsi ya kumeza misumari.

  Mgonjwa huyo alimeza misumari minne na ilibidi madaktari wafanye kazi ya ziada kuiondoa misumari hiyo toka tumboni mwake.

  Athena alijitetea kuwa mgonjwa huyo alikuwa na tabia ya kumeza misumari na vitu mbali mbali vidogo vidogo vya chuma.

  Kesi hiyo iliahirishwa na Athena atasomewa hukumu yake tarehe nane mwezi oktoba.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2945986&&Cat=2
   
Loading...