figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,480
MHUDUMU wa afya mwandamizi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Paul Ngassa (57) amekamatwa akidaiwa kupokea rushwa ya Sh 40,000 kutoka kwa mgonjwa Edward Tindi aliyefanyiwa upasuaji hospitalini hapo.
Mgonjwa huyo aliyekuwa amelazwa katika hospitali hiyo ni mkazi wa kata ya Masengwa, kijiji cha Bubale.Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Shinyanga, Gasto Mkono, jana alithibitisha tukio hilo na alisema mgonjwa huyo inadaiwa alidaiwa kiasi hicho cha fedha na mhudumu huyo ili asafishwe kidonda.
“Mgonjwa huyo kwa mujibu wa maelezo yake aliombwa Sh 50,000 ili asafishwe kidonda, alidai hana kiasi hicho bali ana Sh 20,000 tu, wazo lilimjia ashirikishe Takukuru ndipo tulipopata taarifa hiyo tukampatia hela hilo.
“Wakati huo, kabla ya kumpa fedha zetu, alimtangulizia Sh 20,000 nyingine alimweleza baadaye na hapo tukampatia fedha zetu akamalizie akampelekea na kuzipokea tukamkuta nazo,” alisema Mkono. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Ntuli Kapologwe alithibitisha tukio hilo na kusema tayari wameandaa barua ya kumsimamisha kazi.
Chanzo: TimesFM