Daktari wa Hospitali ya Amana asomewa mashtaka ya ubakaji, ulawiti

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Dkt. Joseph Mwaipola ambaye ni mtumishi wa Hospitali ya Amana Mkoani Dar es Salaam, leo Septemba 9, 2022 amefikishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matatu yakiwemo kumbaka mtoto wa miaka 17.

Shitaka hilo limesikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Ruboroga ambapo mashitaka yamesomwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Sylvia Mitanto.

Shtaka la kwanza ni ubakaji, Wakili Sylvia amedai mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 2022 katika Hospitali ya Amana.

Shtaka la pili inadaiwa Mei 31, 2022 akiwa katika nyumba ya wageni ya Pazuri iliyoko Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, mshitakiwa alimbaka binti huyo.

Shtaka la tatu ni kulawiti, mshitakiwa anadaiwa alitenda kosa Februari 2022 katika Hospitali ya Amana, ambapo alimlawiti binti huyo.

Mshtakiwa amekana mashtaka, upande wa mashitaka umeeleza kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika na unaomba tarehe ya kumsomea maelezo ya awali.

Hakimu Roboroga ametoa masharti ya dhamana kuwa mshtakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua ya utambulisho pamoja na Vitambulisho vya kura au vya kazi watakaotia saini dhamana ya Tsh. milioni tano.

Mshtakiwa aliweza kutimiza masharti ya dhamana, hivyo yuko nje kwa dhamana, kesi itatajwa Oktoba 5, 2022 kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali (PH).
 
Hiyo kesi ni ngumu na ya kufedhehesha sana pengine LABDA daktari alikua na mahusiano na binti na ikaja kugundulika kwa wazazi wa binti, wakambananisha binti akaongea yote sasa wakaona wamuangushie jumba bovu daktari kwamba alibaka.

Kwa trend hiyo kwamba Kabakwa na kulawitiwa February 2022, mtu huyo huyo karudia tena kubakwa mei 31,2022 tena kabakwa nyumba ya wageni iliyopo temeke. Kwa nini asingeenda kushtaki hiyo hiyo february mara baada ya kubakwa mara ya kwanza? Hapo inawezekana kulikua na makubaliano japo daktari kafanya kosa kubwa sana kula mgonjwa wake
 
But mkuu elewa huyu aliyebakwa ana miaka 17 tu,na kuna uwezekano Dr.ametake advantage kuwa binti huyu ametoka kwenye family yenye challenges nyingi, under 17,raping hii case haina bail
 
Dkt. Joseph Mwaipola ambaye ni mtumishi wa Hospitali ya Amana Mkoani Dar es Salaam, leo Septemba 9, 2022 amefikishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matatu yakiwemo kumbaka mtoto wa miaka 17.

Shitaka hilo limesikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Ruboroga ambapo mashitaka yamesomwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Sylvia Mitanto.

Shtaka la kwanza ni ubakaji, Wakili Sylvia amedai mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 2022 katika Hospitali ya Amana.

Shtaka la pili inadaiwa Mei 31, 2022 akiwa katika nyumba ya wageni ya Pazuri iliyoko Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, mshitakiwa alimbaka binti huyo.

Shtaka la tatu ni kulawiti, mshitakiwa anadaiwa alitenda kosa Februari 2022 katika Hospitali ya Amana, ambapo alimlawiti binti huyo.

Mshtakiwa amekana mashtaka, upande wa mashitaka umeeleza kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika na unaomba tarehe ya kumsomea maelezo ya awali.

Hakimu Roboroga ametoa masharti ya dhamana kuwa mshtakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua ya utambulisho pamoja na Vitambulisho vya kura au vya kazi watakaotia saini dhamana ya Tsh. milioni tano.

Mshtakiwa aliweza kutimiza masharti ya dhamana, hivyo yuko nje kwa dhamana, kesi itatajwa Oktoba 5, 2022 kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali (PH).
Ni MUUGUZI. watanzania siamini kama bado ni wapumbavu mpaka hatujui tofauti za muuguzi na daktari hadi leo 2022. Kazi
 
Hiyo kesi ni ngumu na ya kufedhehesha sana pengine LABDA daktari alikua na mahusiano na binti na ikaja kugundulika kwa wazazi wa binti, wakambananisha binti akaongea yote sasa wakaona wamuangushie jumba bovu daktari kwamba alibaka.

Kwa trend hiyo kwamba Kabakwa na kulawitiwa February 2022, mtu huyo huyo karudia tena kubakwa mei 31,2022 tena kabakwa nyumba ya wageni iliyopo temeke. Kwa nini asingeenda kushtaki hiyo hiyo february mara baada ya kubakwa mara ya kwanza? Hapo inawezekana kulikua na makubaliano japo daktari kafanya kosa kubwa sana kula mgonjwa wake

Huyu ni mtu na mpenzi wake. Walikuwa na mahusiano.

Sheria ndiyo inamfunga huyo daktari kwa kuwa na mahusiano na binti china ya miaka 18 ama mwanafunzi wa shule yoyote ni ubakaji.
 
Hope's mkuu nawe utakuja kuwa mzazi na uzae msichana halafu u comment kama hivi, hakuna sex ya makubaliano na under age

Ipo. Sheria inaruhusu sex na under age kama mmefunga ndoa halali tu.

Sheria ya ndoa imeruhusu binti wa miaka 15 kufunga ndoa kama wazazi wake wameridhia na yeye binti ameridhia. Na asiwe mwanafunzi wa shule yoyote.
 
Back
Top Bottom